Taarifa ya kuuaga na kuusafirisha mwili wa Fred Mtoi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,041

Wapenzi wa BBC, ndugu, jamaa na marafiki,

Tunawaarifu kuwa ibada ya kumuaga ndugu yetu mpendwa Fred Mtoi, kwa walioko Uingereza itafanyika Jumamosi tarehe Mosi Disemba 2012 katika Kanisa la St. Anne's Lutheran mjini London kuanzia saa tano kamili asubuhi.

Anwani ya Kanisa ni:
St Anne's Lutheran Church,
Gresham Street,
London
EC2V

Safari ya kuupeleka mwili wa marehemu Dar es salaam nchini Tanzania itakuwa Jumatatu tarehe 3 Disemba 2012 jioni kwa ndege ya Shirika la British Airways na kuwasili huko Jumanne saa moja asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Shukran za dhati kwa Shirika la BBC kwa kushughulikia na kugharamia mipango yote ya kuusafirisha mwili wa marehemu Fred hadi Tanzania.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kadri zinavyojitokeza kuhusu mipango ya msiba huu mpaka mwili utakaposafirishwa kwenda nyumbani Tanzania.

Idhaa ya Kiswahili ya BBC

Kwa maelezo zaidi wasiliana
na Zawadi Machibya +44 795 260 7038
 
Jamani kweli inafurahisha kusikia kwamba BBC wamegharimia gharama zote za kumsafirisha kijana wetu Fred Mtoi. Mungu awazidishie BBC kwa moyo wao huo wa kiungwana
Nasi tunawaombe wasafiri salama na wafike Dar es salaam, Tanzania salama na amani ya Bwana wetu YESU kristo
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake libarikiwe
 
R.I.P Fred Mtoi!

121117122320_bbc_swahili_304x171_bbc_nocredit.jpg
 
jamani huyu mtangazaji kumbe alikufa???? I was out of news ................

May God comfort all those who have been touched by this sad demise - including myself!!!
 
Rest In Peace Fred Mtoi na mwanga wa milele Bwana umwangazie na hata apumzike mikononi mwako Bwana milele!
 
huyu jamaa nilipa taarifa za kifo chake zaidi ya wiki 2 zilizopita na nilidhani tayali ameshazikwa kumbe bado hata hajasafilishwa, na tarehe 3 dec ndo anafika dsm bila shaka moshi atafika tar 4. Hiv kwanini tunatesa marehem wetu kwa kuchelewa kuwahifadh mape,a. R.i.p mtoyi
 
Masuala ya kukabidhiwa mwili wa marehemu toka hospitali na kusafirisha uk yanachukua muda sana ...paperwork uk ndio wenyewe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom