Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,299
- 33,079
Wapenzi wa BBC, ndugu, jamaa na marafiki,
Tunawaarifu kuwa ibada ya kumuaga ndugu yetu mpendwa Fred Mtoi, kwa walioko Uingereza itafanyika Jumamosi tarehe Mosi Disemba 2012 katika Kanisa la St. Anne's Lutheran mjini London kuanzia saa tano kamili asubuhi.
Anwani ya Kanisa ni:
St Anne's Lutheran Church,
Gresham Street,
London
EC2V
Safari ya kuupeleka mwili wa marehemu Dar es salaam nchini Tanzania itakuwa Jumatatu tarehe 3 Disemba 2012 jioni kwa ndege ya Shirika la British Airways na kuwasili huko Jumanne saa moja asubuhi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Shukran za dhati kwa Shirika la BBC kwa kushughulikia na kugharamia mipango yote ya kuusafirisha mwili wa marehemu Fred hadi Tanzania.
Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kadri zinavyojitokeza kuhusu mipango ya msiba huu mpaka mwili utakaposafirishwa kwenda nyumbani Tanzania.
Idhaa ya Kiswahili ya BBC
Kwa maelezo zaidi wasiliana
na Zawadi Machibya +44 795 260 7038