Taarifa ya kupotea kwa ndugu Fakhru Issa Abeid (maarufu Osama)

sharafu

Member
Jun 1, 2020
78
75
TAARIFA YA KUPOTEA KWA NDUGU FAKHRU ISSA ABEID (MAARUFU OSAMA)

TAARIFA KWA KUPOTEA NDUGU FAKHRU ISSA ABEID WA DAR ES SALAAM (AL MAARUFU OSAMA) BWANA FAKHRU ALIYEPOTEA KATIKA MAZINGIRA TATANISHI MAENEO YA VIGWAZA TSN PETRO STATION KITUO CHAKE CHA KAZI ,

SIKU YA ALKHAMIS 04/06/2020 MAJIRA YA SAA NNE ASUBUHI MKOA WA PWANI WILAYA YA CHALINZE KIJIJI CHA VIGWAZA ,

HIVYO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA TUNAOMBA ATUPIGIE SIM 0754 616731 / 0677 838934 AU ATOE TAARIFA KITUO CHOCHOTE CHA POLICE (VIG/RB/212/2020 YA 05/06/2020)

FAKHRU.png
 
Duuu kupotelewa na ndugu au mtoto afu usimpate inaleta ukakasi sana.kila siku utakuwa unawaza uko alipo ana hali gani!! Bora afe unazika unasahau kuliko apotee asirudi
 
Alikuwa mzima. Inavyosemekana na mtoa taarifa kuna watu walikuja kumchukua katika eneo lake la kazi (Petrol Station), tangu hapo hakuonekana tena
Walimchukua katika mazingira yapi,kukamatwa,kutekwa au kuondoka naye kwa hiyari?

Yote kwa yote binaadam tuna mambo mengi sana sirini,unawezakuta jamaa yuko zake polisi huko wanayajenga kwa msala fulani mzito nyinyi hamjui.
 
Alikuwa mzima. Inavyosemekana na mtoa taarifa kuna watu walikuja kumchukua katika eneo lake la kazi (Petrol Station), tangu hapo hakuonekana tena

Poleni sana. Kama ndio hivyo atakuwa anahojiwa mahali. Huwenda serikali ilipata fununu ndugu yenu alikuwa akishirikiana na watu waovu kwa namna moja ama nyingine.

Kuweni na subila kama hatokuwa na kosa atarudi tu bila shida yoyote.
 
Poleni sana. Kama ndio hivyo atakuwa anahojiwa mahali. Huwenda serikali ilipata fununu ndugu yenu alikuwa akishirikiana na watu waovu kwa namna moja ama nyingine..

Kuweni na subila kama hatokuwa na kosa atarudi tu bila shida yoyote..
Kama scenario yako ya kwamba yupo anahojiwa ipo sahihi, huyu mtu hata akirudi atarudi na shida mbalimbali.

Atarudi na shida ya kutembea, vidonda, makovu, trauma and a lost dignity. But wait there's more!!

Akiuawa bahati mbaya. Atatupwa sehemu, utampata ndugu yako, dead, ila hutajua haswa ni nani alihusika.

Zinatokea sana Marekani kutokana na namna yao ya kudeal na ugaidi.
 
Back
Top Bottom