Taarifa ya kukuosekana Umeme kwa baadhi ya maeneo katika mkoa wa kinondoni kaskazini

hakuna shida

Member
Dec 16, 2015
25
5
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO YA MKOA WA KINONDONI KASKAZINI.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa line ya Packers imezimwa saa 3 asubuhi hii leo February 12, 2016 kwa ajili ya matengenezo kwenye njia hiyo. Maeneo ambayo yanakosa umeme ni Mbezi Beach, Rainbow, sehemu ya Kilongawima, Whitesands, Jangwani Beach na eneo la Zena Kawawa. Wateja wote walijulishwa kupitia vyombo vya habari. Umeme utarejeshwa saa 11 jioni baada ya matengenezo hayo.

NIA YA MATENGENEZO HAYO NI KUONDOA KERO YA UMEME KUKATIKA MARA KWA MARA.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu.
 
Back
Top Bottom