Taarifa ya kufunguliwa kesi mbili; Kuomba kutenguliwa kwa zuio la jeshi la polisi na bunge live

MahakamaCCM katika kesi iliyofunguliwa na UKAWA dhidi ya Serikali ya kidikteta itoe maamuzi in favour of UKAWA? I doubt it.
Tena Jaji Wambali ehehehehe
Lkn at least UKAWA wametimiza majukumu yao!Wameionyesha serikali kama wanafikiria vyema
 
Jamss

Wakati kakujibu kutokana na comment yako ukitaka kufananisha siasa za uk na tz basi vyama vyote h@avina tofauti. Tangu thatcher aache ngazi Conservative imebadilisha zaidi ya viongozi 5 mpaka Cameron akashinda lakini CUF na CDM bado wale wale ndiyo ilikua maana ya mtoa
comment

Kwani ccm wanatokaga hata kama ndani ya miaka mitano kuna wizi umefanyika wa rasilimali za taifa na visibitisho vipo na bado anapewa agombee tena mingine mitano na wizi wa kura juu halafu unataka mdogo aoneshe mfano ikiwa mkubwa ndo unaongoza kwa maovu halafu mnakuja et chadema wafanye hayo aliepewa mamlaka ya kutetea maslah ya taifa hawez kila kukicha raia wasio na hatia wanapoteza maisha kwa ukosefu wa huduma za msingi kwa upuuz wa kundi flani lilohodhi madaraka.
 
Hii kesi kwa upande wa serikali angekuwapo Dk Tulia angeikata fasta kama ya mita 200
Wakati mwingine chadema nashindwa kuwaelewa,unaenda mahakamani kisa umenyimwa kufanya maandamano au kuoneshwa live
 
Donald Cameron aliwaahidi wananchi Wa Uingereza iwapo atachaguliwa ataitisha kura ya maoni ili kujua wananchi bado wanatamani / wanaona umuhimu Wa EU kwao.

Pamoja na ahadi aliwasihi kubakia kwenye umoja huo kwani unafaida kubwa. Baada ya kura majuzi kuamua chama chake na yeye kama kiongozi alitangaza kujiuzuru ili kupisha mawazo mapya( uongozi wenye nguvu),


Ccm imekuwepo serikalini miaka 52, hakuna maji safi na salama mashuleni,hakuna umeme,hakuna madawati mashuleni,rushwa na ufisadi ndo usiseme ccm na viongozi wao hawakuwahi kwa utashi kujiuzuru!

Ccm inaishi kwa kuvunja sheria,ikidhani watu inaowaongoza wao hawavunja sheria jitakaseni.

Chadema inatoa picha( dira ) kuwa hatutatwaa madaraka kwa damu Bali sheria zitazingatiwa kuufikia ukweli( freedom).

Ccm tunaitaka ijue kuwa huwezi kuleta maendeleo gizani,wakati unazuia vyama kufanya siasa unaandaa kaburi la unaosaidiana nao kutawala wakuhujumu kisawasawa.

Uongozi Wa kiimla haujawahi kuleta tija duniani. Nani asiyejua USA,Ujerumani,Uingereza,na ufaransa inauhuru Wa kisiasa lakini inaitawala Dunia?

Ccm imekata pumzi
mwenyekiti wa chadema mbowe inabidi ajiuzulu kwa kushindwa kuiweka chadema madarakani katika vipindi vitatu vya uchaguzi mkuu!! hii nayo ni democracy
 
KUHUSU KUFUNGULIWA KWA KESI MBILI; KUOMBA KUTENGULIWA KWA ZUIO LA JESHI LA POLISI NA BUNGE LIVE

Taarifa inatolewa kwa umma kuwa Baraza la Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Katibu Mkuu wa Chama, wamefungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam (main registry) kuiomba mahakama hiyo itengue uamuzi wa Jeshi la Polisi nchini kupiga marufuku, mikutano na maandamano ya vyama vya siasa nchi nzima.

Katika shauri hilo la madai namba 43, 2016, wadai hao wanaiomba Mahakama Kuu kufuta/kutengua zuio la mikusanyiko/mijumuiko ya kisiasa ya vyama vya siasa kwa kipindi kisichojulikana lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), kwa sababu;

Halikuwashirikisha.
Halikuwapatia haki ya kusikilizwa.
Ni uonezi.
Linaua demokrasia nchini.
Halina mipaka wala sababu za msingi kisheria na kimantiki.
Limezidi mamlaka ya polisi kisheria.

Shauri hilo limetajwa leo Juni 27, 2016, mbele ya Jaji Kiongozi Prof. Ferdinand Wambali ambapo upande wa Serikali utatakiwa kuleta hati ya kiapo kinzani, Juni 30, mwaka huu, kabla mahakama hiyo haijakaa kuanza kusikiliza maombi madogo (leave) Julai 1, saa 8 mchana mbele ya Jaji Kiongozi ambapo uamuzi unatarajiwa kutolewa Julai 4, mwaka huu.

Wakati huo huo, Chama kinapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kwa ujumla kuwa katika jitihada za kuhakikisha nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya katiba na sheria, kimewatafutia mawakili wananchi walioamua kufungua kesi ya Kikatiba, Mahakama Kuu wakipinga kuminywa kwa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge (Bunge Live).

Wadai hao; Azizi Himbuka, Perfect Mwasilelwa, Moza Mushi, Hilda Newton, Penina Nkya, Rose Moshi, Kubra Manzi, Andrew Mandari, Ben Rabiu Saanane, Juma Uloleulole na Ray Kimbito, wamefungua kesi hiyo ya Kikatiba namba 13, 2016 wakidai kuwa;

Wanayo haki ya kikatiba kupata habari na kushiriki moja kwa moja au kupitia wawakilishi wao katika shughuli zote za uongozi na kuisimamia serikali. Kutokana na kuwepo kwa mminyo huo wa matangazo ya bunge, wananchi hao wanashindwa kuona moja kwa moja namna ambavyo Serikali inawajibika ili waweze kutoa maelekezo stahiki kwa wabunge wao.

Katika kesi hiyo iliyotajwa leo Juni 27, mbele ya Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali, wadai hao wanasema kuwa kutokana na mminyo huo wa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge, wanashindwa kujua wabunge wao wanasimamia vipi serikali ili waweze kujua na kutathmini uwakilishi wao bungeni.

Aidha wadai hao wanasema kuwa kwa kuangalia mahitaji ya utawala bora na uwazi katika zama za maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, matangazo ya moja kwa moja ni sehemu muhimu ya haki ya kupata habari ambayo ni haki ya kikatiba.

Kesi hiyo nambari 13 ya mwaka huu itasikilizwa mbele ya Majaji watatu; Jaji Kiongozi Wambali, Jaji Kihiyo na Jaji Munisi, ambapo Julai 15, mwaka huu asubuhi, ndipo itaamriwa siku ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, baada ya upande wa serikali kuwa umeleta hati ya utetezi Julai 11 kama ulivyotakiwa na Mahakama hiyo leo.

Hatua hiyo ya CHADEMA kuwasaidia wananchi hao kupata mawakili ni mwendelezo wa juhudi za chama kuchangia mapambano ya demokrasia na kulinda utawala bora unaozingatia katiba na sheria za nchi ili kuwapatia wnaanchi haki na matumaini katika nchi yao ambayo ndiyo msingi imara ya amani na utulivu wa kweli katika jamii.

Imetolewa leo Jumatatu Juni 27, na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

TUMESHINDWA KUJIHALALISHA KWA WATANZANIA KISERA BAADA YA KUKENGEUKA NA KUTOKA KATIKA MISINGI TULIYOSIMAMIA YA KUPAMBANA NA UFISADI NA KUSIMAMIA UTAWALA BORA NA KUANZA KUKUMBATIA SERA ZA KIFISADI. SASA TUNATAFUTA KILA NJIA YA KUBAKIA KWENYE MIDOMO YA WANANCHI..... HAHAHAHAHAHA..... Kuna msemo maarufu usemao "Unaweza kupumbaza watu wote Mara moja NA Baadhi ya watu Mara zote, Lakini hawezi kupumbaza watu wote Mara zote" ... Watanzania wanaona, wanasikia na wanafuatilia kinachotendeka ndani ya siasa za nchi..... Upizani sasa Unatapatapa..,, Sera kwisha umebaki ubabaishaji tuuu......
 
Kwani ccm wanatokaga hata kama ndani ya miaka mitano kuna wizi umefanyika wa rasilimali za taifa na visibitisho vipo na bado anapewa agombee tena mingine mitano na wizi wa kura juu halafu unataka mdogo aoneshe mfano ikiwa mkubwa ndo unaongoza kwa maovu halafu mnakuja et chadema wafanye hayo aliepewa mamlaka ya kutetea maslah ya taifa hawez kila kukicha raia wasio na hatia wanapoteza maisha kwa ukosefu wa huduma za msingi kwa upuuz wa kundi flani lilohodhi madaraka.
Hiyo haina maana kuwa anatakiwa awaige wezi. Halafu kuna nani msafi katika wanasiasa wa Tanzania? Tatizo kubwa mnapata mihemko bila kuangalia kuwa hao jamaa walio huko upinzani wasikwenda kama mikate yao haingetiwa mchanga watu waliapa kabisa kutoondoka ccm na wengine walikua wanapiga marimba kusemana kuwa wengine ni wezi angalia hii video hapo chini kabla ya kuwa kama hao unaowasema wa buku saba kama utataka nitakupatia na transcript yake

sasa wewe na akili zako utamfuata mtu kama huyu?

hawa ni vinyonga kama waliyemfuata

Ukiwa mpenzi wa kitu huwezi badilika hata kama ujifanye upo smart, hapa kahamasisha wanaccm wenzake wawapigie wabunge lakini urais apewe kafanya kama Nyerere alipokua anampigia kampeni Mkapa, baadaye yeye anasema kaibiwa kura hakujua kama aliwaambia waipigie CCM? Video ushahidi
 
Mahakama tendeni haki

Hiyo haina maana kuwa anatakiwa awaige wezi. Halafu kuna nani msafi katika wanasiasa wa Tanzania? Tatizo kubwa mnapata mihemko bila kuangalia kuwa hao jamaa walio huko upinzani wasikwenda kama mikate yao haingetiwa mchanga watu waliapa kabisa kutoondoka ccm na wengine walikua wanapiga marimba kusemana kuwa wengine ni wezi angalia hii video hapo chini kabla ya kuwa kama hao unaowasema wa buku saba kama utataka nitakupatia na transcript yake

sasa wewe na akili zako utamfuata mtu kama huyu?

hawa ni vinyonga kama waliyemfuata

Ukiwa mpenzi wa kitu huwezi badilika hata kama ujifanye upo smart, hapa kahamasisha wanaccm wenzake wawapigie wabunge lakini urais apewe kafanya kama Nyerere alipokua anampigia kampeni Mkapa, baadaye yeye anasema kaibiwa kura hakujua kama aliwaambia waipigie CCM? Video ushahidi

Wachafu wapo ccm huko kila leo unasikia jipu linatumbuliwa ni mwanasiasa yupi wa upinzani yupo mahakaman akijibu shutuma za rushwa na unadhirifu? Huwez ukatuambia et hakuna mwanasiasa msafi wakat huko magambani hela za mboga wanawavimbia tume ya maadili huko kujiuzuru narudia tena kulitakiwa kuwe kwa ccm pia ukiweka video zako kuonesha kuwa hao jamaa walichokuwa wanakiongea kina ukweli mi siwez kuusemea moyo wa mtu mtu anaongea hichi anatenda kile.
 
Swali ambalo CHADEMA watatakiwa kulijibu ni hili, Katiba inasema kupata taarifa au kupata taarifa 'live'. Maana seikali sio kama hainoeshi Bunge, kilichobadilika ni kutokuonesha 'live' mikutano yote.
Hatutaki taarifa zilizo editiwa tunataka tuedit wenyewe.
Idiot
 
Hapa sipendi kabisa kulilaumu jeshi la polisi. Kwani wao ni askari, na kanuni kuu ya askari ni kutii amri tu na si vingenevyo. Na utii huo huonyesha matokeo baada ya jambo kutekelezeka.

Hapa tukumbuke baadhi ya amri ambazo zimeacha uchungu na vidonda kwa baadhi ya watanzania. Mfano: tukio la Paulin Zombe kuwapa amri askari na kuua ndugu zao wasio na hatia lakini pia tukikumbuka tukio la kifo cha mwangosi.

Hoja na ushauri wangu kwa raisi, ajaribu kutenda majukumu yake kwa mujibu wa kikatiba. Maana hiyo ndio aliyoiapa kuifuata, kipindi akikabidhiwa ngao na mkuki.
Vinginevyo ni kulitafutia taifa letu laana.

Kwa sababu upinzani ndio umeweza kutufunilia na kuona maendeleo au udhaifu wa serikali.
 
Back
Top Bottom