Taarifa ya kufunguliwa kesi mbili; Kuomba kutenguliwa kwa zuio la jeshi la polisi na bunge live

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
KUHUSU KUFUNGULIWA KWA KESI MBILI; KUOMBA KUTENGULIWA KWA ZUIO LA JESHI LA POLISI NA BUNGE LIVE

Taarifa inatolewa kwa umma kuwa Baraza la Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Katibu Mkuu wa Chama, wamefungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam (main registry) kuiomba mahakama hiyo itengue uamuzi wa Jeshi la Polisi nchini kupiga marufuku, mikutano na maandamano ya vyama vya siasa nchi nzima.

Katika shauri hilo la madai namba 43, 2016, wadai hao wanaiomba Mahakama Kuu kufuta/kutengua zuio la mikusanyiko/mijumuiko ya kisiasa ya vyama vya siasa kwa kipindi kisichojulikana lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), kwa sababu;

Halikuwashirikisha.
Halikuwapatia haki ya kusikilizwa.
Ni uonezi.
Linaua demokrasia nchini.
Halina mipaka wala sababu za msingi kisheria na kimantiki.
Limezidi mamlaka ya polisi kisheria.

Shauri hilo limetajwa leo Juni 27, 2016, mbele ya Jaji Kiongozi Prof. Ferdinand Wambali ambapo upande wa Serikali utatakiwa kuleta hati ya kiapo kinzani, Juni 30, mwaka huu, kabla mahakama hiyo haijakaa kuanza kusikiliza maombi madogo (leave) Julai 1, saa 8 mchana mbele ya Jaji Kiongozi ambapo uamuzi unatarajiwa kutolewa Julai 4, mwaka huu.

Wakati huo huo, Chama kinapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kwa ujumla kuwa katika jitihada za kuhakikisha nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya katiba na sheria, kimewatafutia mawakili wananchi walioamua kufungua kesi ya Kikatiba, Mahakama Kuu wakipinga kuminywa kwa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge (Bunge Live).

Wadai hao; Azizi Himbuka, Perfect Mwasilelwa, Moza Mushi, Hilda Newton, Penina Nkya, Rose Moshi, Kubra Manzi, Andrew Mandari, Ben Rabiu Saanane, Juma Uloleulole na Ray Kimbito, wamefungua kesi hiyo ya Kikatiba namba 13, 2016 wakidai kuwa;

Wanayo haki ya kikatiba kupata habari na kushiriki moja kwa moja au kupitia wawakilishi wao katika shughuli zote za uongozi na kuisimamia serikali. Kutokana na kuwepo kwa mminyo huo wa matangazo ya bunge, wananchi hao wanashindwa kuona moja kwa moja namna ambavyo Serikali inawajibika ili waweze kutoa maelekezo stahiki kwa wabunge wao.

Katika kesi hiyo iliyotajwa leo Juni 27, mbele ya Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali, wadai hao wanasema kuwa kutokana na mminyo huo wa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge, wanashindwa kujua wabunge wao wanasimamia vipi serikali ili waweze kujua na kutathmini uwakilishi wao bungeni.

Aidha wadai hao wanasema kuwa kwa kuangalia mahitaji ya utawala bora na uwazi katika zama za maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, matangazo ya moja kwa moja ni sehemu muhimu ya haki ya kupata habari ambayo ni haki ya kikatiba.

Kesi hiyo nambari 13 ya mwaka huu itasikilizwa mbele ya Majaji watatu; Jaji Kiongozi Wambali, Jaji Kihiyo na Jaji Munisi, ambapo Julai 15, mwaka huu asubuhi, ndipo itaamriwa siku ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, baada ya upande wa serikali kuwa umeleta hati ya utetezi Julai 11 kama ulivyotakiwa na Mahakama hiyo leo.

Hatua hiyo ya CHADEMA kuwasaidia wananchi hao kupata mawakili ni mwendelezo wa juhudi za chama kuchangia mapambano ya demokrasia na kulinda utawala bora unaozingatia katiba na sheria za nchi ili kuwapatia wnaanchi haki na matumaini katika nchi yao ambayo ndiyo msingi imara ya amani na utulivu wa kweli katika jamii.

Imetolewa leo Jumatatu Juni 27, na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
 
Asante sana kamanda makene kwa kutujulisha habari njema za ukombozi wa pili wa taifa letu
 
Donald Cameron aliwaahidi wananchi Wa Uingereza iwapo atachaguliwa ataitisha kura ya maoni ili kujua wananchi bado wanatamani / wanaona umuhimu Wa EU kwao.

Pamoja na ahadi aliwasihi kubakia kwenye umoja huo kwani unafaida kubwa. Baada ya kura majuzi kuamua chama chake na yeye kama kiongozi alitangaza kujiuzuru ili kupisha mawazo mapya( uongozi wenye nguvu),

Ccm imekuwepo serikalini miaka 52, hakuna maji safi na salama mashuleni,hakuna umeme,hakuna madawati mashuleni,rushwa na ufisadi ndo usiseme ccm na viongozi wao hawakuwahi kwa utashi kujiuzuru!

Ccm inaishi kwa kuvunja sheria,ikidhani watu inaowaongoza wao hawavunja sheria jitakaseni.

Chadema inatoa picha( dira ) kuwa hatutatwaa madaraka kwa damu Bali sheria zitazingatiwa kuufikia ukweli( freedom).

Ccm tunaitaka ijue kuwa huwezi kuleta maendeleo gizani,wakati unazuia vyama kufanya siasa unaandaa kaburi la unaosaidiana nao kutawala wakuhujumu kisawasawa.

Uongozi Wa kiimla haujawahi kuleta tija duniani. Nani asiyejua USA,Ujerumani,Uingereza,na ufaransa inauhuru Wa kisiasa lakini inaitawala Dunia?

Ccm imekata pumzi
 
Nilidhani unawashauri viongozi wako wajiuzulu baada ya kushindwa ktk uchaguzi mkuu mwakajana. Kiongozi wa chama cha labour nchini UK aliposhindwa uchaguzi aliiachia ngazi sasa hii demokrasia gani?
 
mahakama inaweza kutoa haki kama tu haiko mfukoni mwa bhana nkubwa mwenye kifua chake
Wakienda kinyume watatumbuliwa Majipu na kupelekwa Mahakama za kawaida lazima wamfurahishe aliyewateua , njia pekee ikiyosalia ni kumwomba Mungu awape ujasiri wa kutenda haki pasipo kuogopa kutenguliwa Kama mama Anna kilango .
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hawa ufipa kila siku kesi na maandamano, lini watawaletea wananchi maendeleo. Lazima tuwakate 2020
 
KUHUSU KUFUNGULIWA KWA KESI MBILI; KUOMBA KUTENGULIWA KWA ZUIO LA JESHI LA POLISI NA BUNGE LIVE

Taarifa inatolewa kwa umma kuwa Baraza la Wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Katibu Mkuu wa Chama, wamefungua shauri Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam (main registry) kuiomba mahakama hiyo itengue uamuzi wa Jeshi la Polisi nchini kupiga marufuku, mikutano na maandamano ya vyama vya siasa nchi nzima.

Katika shauri hilo la madai namba 43, 2016, wadai hao wanaiomba Mahakama Kuu kufuta/kutengua zuio la mikusanyiko/mijumuiko ya kisiasa ya vyama vya siasa kwa kipindi kisichojulikana lililotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), kwa sababu;

Halikuwashirikisha.
Halikuwapatia haki ya kusikilizwa.
Ni uonezi.
Linaua demokrasia nchini.
Halina mipaka wala sababu za msingi kisheria na kimantiki.
Limezidi mamlaka ya polisi kisheria.

Shauri hilo limetajwa leo Juni 27, 2016, mbele ya Jaji Kiongozi Prof. Ferdinand Wambali ambapo upande wa Serikali utatakiwa kuleta hati ya kiapo kinzani, Juni 30, mwaka huu, kabla mahakama hiyo haijakaa kuanza kusikiliza maombi madogo (leave) Julai 1, saa 8 mchana mbele ya Jaji Kiongozi ambapo uamuzi unatarajiwa kutolewa Julai 4, mwaka huu.

Wakati huo huo, Chama kinapenda kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na umma wa Watanzania kwa ujumla kuwa katika jitihada za kuhakikisha nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya katiba na sheria, kimewatafutia mawakili wananchi walioamua kufungua kesi ya Kikatiba, Mahakama Kuu wakipinga kuminywa kwa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge (Bunge Live).

Wadai hao; Azizi Himbuka, Perfect Mwasilelwa, Moza Mushi, Hilda Newton, Penina Nkya, Rose Moshi, Kubra Manzi, Andrew Mandari, Ben Rabiu Saanane, Juma Uloleulole na Ray Kimbito, wamefungua kesi hiyo ya Kikatiba namba 13, 2016 wakidai kuwa;

Wanayo haki ya kikatiba kupata habari na kushiriki moja kwa moja au kupitia wawakilishi wao katika shughuli zote za uongozi na kuisimamia serikali. Kutokana na kuwepo kwa mminyo huo wa matangazo ya bunge, wananchi hao wanashindwa kuona moja kwa moja namna ambavyo Serikali inawajibika ili waweze kutoa maelekezo stahiki kwa wabunge wao.

Katika kesi hiyo iliyotajwa leo Juni 27, mbele ya Jaji Kiongozi Ferdinand Wambali, wadai hao wanasema kuwa kutokana na mminyo huo wa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge, wanashindwa kujua wabunge wao wanasimamia vipi serikali ili waweze kujua na kutathmini uwakilishi wao bungeni.

Aidha wadai hao wanasema kuwa kwa kuangalia mahitaji ya utawala bora na uwazi katika zama za maendeleo ya teknolojia ya habari na mawasiliano, matangazo ya moja kwa moja ni sehemu muhimu ya haki ya kupata habari ambayo ni haki ya kikatiba.

Kesi hiyo nambari 13 ya mwaka huu itasikilizwa mbele ya Majaji watatu; Jaji Kiongozi Wambali, Jaji Kihiyo na Jaji Munisi, ambapo Julai 15, mwaka huu asubuhi, ndipo itaamriwa siku ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo, baada ya upande wa serikali kuwa umeleta hati ya utetezi Julai 11 kama ulivyotakiwa na Mahakama hiyo leo.

Hatua hiyo ya CHADEMA kuwasaidia wananchi hao kupata mawakili ni mwendelezo wa juhudi za chama kuchangia mapambano ya demokrasia na kulinda utawala bora unaozingatia katiba na sheria za nchi ili kuwapatia wnaanchi haki na matumaini katika nchi yao ambayo ndiyo msingi imara ya amani na utulivu wa kweli katika jamii.

Imetolewa leo Jumatatu Juni 27, na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
wanachadema hiyo ndoo namna ya wachache kula fedha ya ruzuku. kama si ziara za kufanya maandamano yasiyokua na tija ila kuzalisha uvunjifu wa sheria basi kesi zinatafutwa kwa tochi ili mradi fedha ya ruzuku inaliwa na wachache.
 
Swali ambalo CHADEMA watatakiwa kulijibu ni hili, Katiba inasema kupata taarifa au kupata taarifa 'live'. Maana seikali sio kama hainoeshi Bunge, kilichobadilika ni kutokuonesha 'live' mikutano yote.
 
Nilidhani unawashauri viongozi wako wajiuzulu baada ya kushindwa ktk uchaguzi mkuu mwakajana. Kiongozi wa chama cha labour nchini UK aliposhindwa uchaguzi aliiachia ngazi sasa hii demokrasia gani?

Hapa pa kujiuzuru pana wahusu sana viongoz wa ccm twiga wanapanda ndege mtu yupo tu escrow wapo tu nchi imebak shamba la bibi watu wapo tu ndo kwanza wanakwambia ile ile huko migodini ni mashimo tu michanga na dhahabu vinakwenda europe
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nilidhani unawashauri viongozi wako wajiuzulu baada ya kushindwa ktk uchaguzi mkuu mwakajana. Kiongozi wa chama cha labour nchini UK aliposhindwa uchaguzi aliiachia ngazi sasa hii demokrasia gani?
Iliyominywa na CCM
 
Wakienda kinyume watatumbuliwa Majipu na kupelekwa Mahakama za kawaida lazima wamfurahishe aliyewateua , njia pekee ikiyosalia ni kumwomba Mungu awape ujasiri wa kutenda haki pasipo kuogopa kutenguliwa Kama mama Anna kilango .
Jaji sio mwanasiasa akisha teuliwa na kuapishwa hawezi kutenguliwa kirahisi kama mkuu wa mkoa. inaundwa tume ya kijaji kumchunguza. tume hiyo ikiridhika na kosa na kupata ushahidi wa kutosha ndipo uteuzi wake waweza kubatilishwa
 
Back
Top Bottom