Taarifa ya kubadilisha combination kwa kidato tano na kozi za vyuo vya ufundi

Taarifa muhimu kwa Wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne, mwaka 2020

Waziri Jafo ametangaza utaratibu wa wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2020 kubadilisha Tahasusi(Combination) za Kidato cha Tano na Kozi za Vyuo vya Elimu ya Ufundi kwa njia ya mtandao kwenye mfumo wa Kieletroniki wa uchaguzi wa Kidato cha Tano na vyuo mwaka 2021.

Amesema Waziri Jafo Zoezi hili litafanyika kuanzia tarehe 29/03/2021 hadi tarehe 11/04/2021 saa sita usiku. Hivyo, wanafunzi wanaotaka kufanya mabadiliko wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi unaopatikana katika anuani ya selform tamisemi


Mwisho ni kutangazwa kwa Tahasusi mpya zilizoanzishwa kwa wanafaunzi wa kidato cha Tano, mwaka 2021 kama ifuatavyo:-
1. Physics, Mathematics, Computer studies (PMC) watasoma shule ya sekondari Dodoma ni wasichana na Shule ya sekondari ya ufundi Iyunga ni wavulana.

2. Kiswahili, French, Chinese (KFC) watasoma sekondari ya Morogoro ni wasichana na wavulana watasoma sekondari ya Usagara.

3. Kiswahili, English ,Chinese(KEC) watasoma sekondari ya Morogoro ni wasichana na wavulana watasoma sekondari ya Usagara.

4. Physical Education,Biology, Fine Arts (PBF) watasoma wasichana shule ya sekondari Makambako na wavulana wao ni sekondari ya Kibiti. Pia, shule ya sekondari ya Mpwapwa ni kwa ajili ya wasichana na wavulana kwa tahasusi ya PBF !

5. Physical Education, Geography,Economics (PGE) watasoma wasichana shule ya sekondari Makambako na wavulana wao ni sekondari ya Kibiti. Pia, shule ya sekondari ya Mpwapwa ni kwa ajili ya wasichana na wavulana kwa tahasusi ya PGE !
View attachment 1737742

Kwa msaada wa kuifundi au tatizo lolote wasiliana na dawati la msaada
Simu: 0262323609 au 0262320028 au andika barua pepe: helpdesk@tamisemi.go.to

1619083591172.png

Wakuu bado kuna changamoto ya kupata michepuo mipya tajwa juu pichani; hata kwa wenye sifa wanapojaribu kuomba "KFC, KEC, PGE,PBF" ! NANI AMEFANIKIWA ?
 
Back
Top Bottom