Taarifa ya kubadilisha combination kwa kidato tano na kozi za vyuo vya ufundi

Elisha Sarikiel

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
889
1,515
Taarifa muhimu kwa Wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne, mwaka 2020

Waziri Jafo ametangaza utaratibu wa wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2020 kubadilisha Tahasusi(Combination) za Kidato cha Tano na Kozi za Vyuo vya Elimu ya Ufundi kwa njia ya mtandao kwenye mfumo wa Kieletroniki wa uchaguzi wa Kidato cha Tano na vyuo mwaka 2021.

Amesema Waziri Jafo Zoezi hili litafanyika kuanzia tarehe 29/03/2021 hadi tarehe 11/04/2021 saa sita usiku. Hivyo, wanafunzi wanaotaka kufanya mabadiliko wanatakiwa kuingia kwenye mfumo wa uchaguzi wa wanafunzi unaopatikana katika anuani ya selform tamisemi


Mwisho ni kutangazwa kwa Tahasusi mpya zilizoanzishwa kwa wanafaunzi wa kidato cha Tano, mwaka 2021 kama ifuatavyo:-
1. Physics, Mathematics, Computer studies (PMC) watasoma shule ya sekondari Dodoma ni wasichana na Shule ya sekondari ya ufundi Iyunga ni wavulana.

2. Kiswahili, French, Chinese (KFC) watasoma sekondari ya Morogoro ni wasichana na wavulana watasoma sekondari ya Usagara.

3. Kiswahili, English ,Chinese(KEC) watasoma sekondari ya Morogoro ni wasichana na wavulana watasoma sekondari ya Usagara.

4. Physical Education,Biology, Fine Arts (PBF) watasoma wasichana shule ya sekondari Makambako na wavulana wao ni sekondari ya Kibiti. Pia, shule ya sekondari ya Mpwapwa ni kwa ajili ya wasichana na wavulana kwa tahasusi ya PBF !

5. Physical Education, Geography,Economics (PGE) watasoma wasichana shule ya sekondari Makambako na wavulana wao ni sekondari ya Kibiti. Pia, shule ya sekondari ya Mpwapwa ni kwa ajili ya wasichana na wavulana kwa tahasusi ya PGE !


1617011062142.png



Kwa msaada wa kuifundi au tatizo lolote wasiliana na dawati la msaada
Simu: 0262323609 au 0262320028 au andika barua pepe: helpdesk@tamisemi.go.to

 
Serikali imesema lengo la kufanya mabadiliko ya tahasusi ni kuwawezesha wanafunzi kubadilisha machaguo yao kulingana na ufaulu wao kwenye matokeo ya mtihani wa Kidato cha nne.

Mhe.waziri Jafo anafafanua kuwa serikali imetoa fursa kwa wahitimu kubadili machaguo yao ili kuwawezesha wanafunzi kusoma fani au tahasusi itakayowandaa kuwa na utaalam katika maisha yao; “ Baadhi ya wanafunzi hawakujaza kwa uhakika tahasusi au kozi kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo waliyachagua , hivyo kwa sasa wanafahamu masomo waliyofaulu vizuri na wanaweza kuchagua tahasusi au fani za kusomea” amesisistiza Waziri Jafo.

Hata hivyo Waziri Jafo amesema kutokana na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia kumekuwa na uhitaji wa wataalam wa fani mbalimbali viyo Serikali imeanzisha tahasusi mpya tano kwa ajili ya wanafunzi wanaoingia kidato cha tano mwaka huu ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa wataalam nchini.
 
PMC nafikiri ichangamkiwe na vijana wanao enda kidato cha tano kwa muhula mpya pia kulingana na wigo mpana wa biashara baina ya china na tanzania nafikiri KFC ichangamkiwe napata shaka kama mkazo utatiliwa kwenye izi taasusi mana ni ngeni lakini kwenye mabadiliko aya sijasikia somo la historia ya tanzania au ndo mchakato bado unaendelea na lenyewe walipaswa kuelezea kua wanafunzi watao anza kidato cha tano wajiandae ki saikolojia
 
PMC nafikiri ichangamkiwe na vijana wanao enda kidato cha tano kwa muhula mpya pia kulingana na wigo mpana wa biashara baina ya china na tanzania nafikiri KFC ichangamkiwe napata shaka kama mkazo utatiliwa kwenye izi taasusi mana ni ngeni lakini kwenye mabadiliko aya sijasikia somo la historia ya tanzania au ndo mchakato bado unaendelea na lenyewe walipaswa kuelezea kua wanafunzi watao anza kidato cha tano wajiandae ki saikolojia
Hilo somo nadhani ni la lazima sio la kuchagua.

All in all PMC nimeikubali sana.
 
Nadhani Computer ianze form one. Tena iwe ni programming na Data Science.
Tumechelewa mnoooo
Programming itakuepo lazima ila haitakua deep kama chuo. Data science sidhani!!

Atleast tutakua na wanafunzi wa CS au CE wenye background nzuri ya computer sio mtu unaanza degree ya computer engineering hujui hata HTML ni nini!!
 
Sijui ni lini watakuja na wazo la kuwafanya wanafunzi wa specialize toka shule za awali.

Ninaamini watoto wanapoteza sana nuru yao kwa kusoma masomo mengi ambayo huwa then wanayadrop wanapoelekea elimu ya juu,
Mfano hapa, combinations ina masomo matatu tu , kwa nini huyu mtoto alisoma masomo zaidi ya saba akiwa primary na secondary?
 
Sijui ni lini watakuja na wazo la kuwafanya wanafunzi wa specialize toka shule za awali
Ninaamini watoto wanapoteza sana nuru yao kwa kusoma masomo mengi ambayo huwa then wanayadrop wanapoelekea elimu ya juu,
Mfano hapa, combinations ina masomo matatu tu , kwa nini huyu mtoto alisoma masomo zaidi ya saba akiwa primary na secondary?
Lengo la elimu ni nini? Tuanzie hapo kwanza. Kama lengo ni kumwezesha binadamu kuyaelewa mazingira yake katika upana wake wa jumla ni muhimu sana kumpa mtoto mwangaza mzima wa mambo yalivyo katika ulimwengu japo kwa juu juu. Ndicho kinachofanyika karibu duniani kote katika miaka ya mwanzo mwanzo. Kumpa binadamu angalau fununu tu ya ulimwengu huu ulivyo; na akishaipata fununu hiyo basi achague mwenyewe ni wapi anataka kuelekea.

Ukikazana watoto waspecialize tangu shule za awali utatengeneza taifa la wajinga ambao watakuwa wanajua tu kaeneo kao kadogo walikosomea na kujibana tangu awali. Ningekuelewa sana kama ungesema pengine tunachelewa mno kuwapa watoto nafasi ya kuspecialize na tungeweza kuanzia kidato cha tatu huko wakishafanya mtihani wa kidato cha pili lakini kusema kuwa waanzie kuspecialize tangu shule za awali au msingi hapana. Na sijui kama kuna taifa hapa duniani ambalo linafanya hivyo.
 
Kunana siku niliona kwenya Mtandao kua karibuni Waafrika tutalazimishwa kusoma Kichina. Kama Kiswahili Baada ya Miaka zaidi 50 ya kujitawala na Makabila mengine wanashindwa kuongea kiswahili fasaha, sijui kichina itakuwaje?
 
Back
Top Bottom