Taarifa ya kamati ya uchunguzi wa tuhuma za maovu hospitali ya mkoa mtwara. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya kamati ya uchunguzi wa tuhuma za maovu hospitali ya mkoa mtwara.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Yona F. Maro, Nov 12, 2008.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Nov 12, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  TAARIFA YA KAMATI YA UCHUNGUZI WA TUHUMA ZA MAOVU HOSPITALI YA MKOA MTWARA.


  UTANGULIZI
  Mheshimiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Mkoa
  Waheshimiwa Wajumbe wa Bodi ya Hospitali ya Mkoa
  Tunamshukuru sana Mungu kuwa Ametulinda,ametuongoza,ametupa hekima na kutushindia mengi katika kazi hii nzito ambayo Bodi yako ilitukabidhi tarehe 23 Oktoba 2007.Katika kikao cha kawaida cha Bodi yako.
  Mheshimiwa Mwenyekiti,
  Kazi hii ilikuwa ni nzito,pana na ndefu tena yenye gharama kubwa ya muda,vifaa,chakula,usafiri.
  Ilitulazimu kufanya kazi polepole na kujiandaa kwa kila hatua.Tunakiri kazi ilikuwa ngumu sana ugumu huo ulitokana na baadhi ya haya yafuatayo
  1. Pale ambapo tulijikuta kama tumejituma baada ya kukosa hata maji ya
  Kunywa tulipoambiwa hakuna bajeti.
  2. Baadhi ya watenda kazi walikuwa wakali na kukataa kutupatia ushirikiano wowote kufanikisha kazi hii nzuri(Km Muuguzi Mkuu)Kamati ilijiuliza kulikoni? Mashaka hofu zinatoka wapi?
  3. Mahali pengine tulianza kutoa taarifa tukajifunza majibu yanaandaliwa yanayofanana kabisa ili yanakosa tafsiri zinazofanana.Km Wagonjwa kufia kwenye foleni 1. Mgonjwa hufia njiani.
  2. Mgonjwa hufia kitandani kwa kuchelewa kupata
  Huduma ya daktari kwasababu ya uchache
  Madaktari.
  4. 3.Ikiwa huna waganga wa kutosha unatazamia
  5.
  Hali hii iliifanya kamati yangu ianze kufanya ziara za kushtukiza ili kupata ukweli si ukweli wa kuchonga.
  Pamoja na mazingira hayo naomba nichukue fursa hii kukushukuru wewe Mwenyekiti pamoja na Bodi yako kwa kutupa fursa hii ili tujifunze. Hadi hapo tuna kila sababu ya kukiri kuwa KAZI TULIYOTUMWA TUMEJARIBU KUIFANYA NA KUIKAMILISHA.
  Katika taarifa hii tumejitahidi sana kutotoa majina ya wagonjwa,Wananchi na Viongozi, Waganga,Wahudumu,Madaktari waliotuambia ukweli.
  Tumefanya hivyo ili kulinda UMOJA,USIRI,MAZINGIRA ili taarifa itusaidie kuona ukweli unaoonekana katika taarifa hii bila kujengeana fitina nk.
  Tumeweka bayana yale yaliyoonekana moja kwa moja KWETU ambayo Kamati inaridhika kuwa ni udhaifu na tuna uthibitisho na tunaweza kujibu mtu akitaka mafafanuzi.
  Nachukua fursa ya mwisho kuwashukuru waheshimiwa wajumbe wa kamati hii
  1. Rev Lucas Mbedule Mwenyekiti
  2. Mr. Mnali
  3. Rev Fr Chilamula
  4. Mr Mbunda
  5. Mr Mtumika

  HADIDU ZA REJEA
  1. Wagonjwa kufia kwenye mangojeo
  2. Kuwepo kwa viashiria vyaMadaktari kupokea rushwa
  3. Lugha mbaya na huduma dhaifu Ward ya Frelimo
  4. Ukosefu wa Dawa Hospitalini
  5. Uhusiana wa madaktari na maduka ya maduka ya madawa(kumiliki na kuuza kwa bei kubwa.
  6. Upendeleo katika huduma.
  Watu waliohojiwa na KAMATI
  1. Uongozi wa Hospitali
  2. Viongozi wa Idara na taasisi za Hospitali
  3. Wagonjwa hospitalini
  4. Ndugu za wagonjwa
  5. Wananchi wa kawaida
  6. Viongozi wa Serikali
  7. Viongozi wa Mashirika binafsi na Taasisi.
  8. Watumishi wa kawaida wa Hospitali.
  1.WAGONJWA KUFA KABLA YA KUPATA HUDUMA.
  Kwa ujumla jambo hilo lilionekana kuwa kuna ukweli mkubwa kuwa wagonjwa mara kadha wamekufa hospitalini kabla hawajapata matibabu. Si kweli kuwa wagonjwa hufa wakiwa kwenye foleni nje, bali huwa kwenye foleni ya ndani. Maana kupata huduma yaani ucghunguzi wa ugunjwa,na hatimaye kutibiwa huchukuwa mudamrefu na ndipo penye dalili ya rushwa na viashiria vya rushwa ili mgonjwa ahudumiwe.
  Taarifa iliyoandikwa inachukuliwa kwa tafsiri ya upande wa pili si ile inavyo someka kuwa hufia kwenye foleni. Bali imebainika kuwa kadha wamefia hospitalinbi na kwa kuwa Hati ya kifo hutolewa na Daktari kwa hiyo si rahisi kujua kuwa Wagonjwa hufia hosipitalini bila kupata tiba. Majina ya waliotoa taarifa hii………
  2. KUKITHIRI KWA RUSHWA HOSPITALINI.
  Uchunguzi na mahojiano yanaonyesha dhahiri kuwa vipo vitendo vya kuomba na kupokea rushwa, vitendo ambavyo hufanywa na baadhi ya Madaktari. Jambo hili limethibitishwa na maelezo ya pande zote yaani Uongozi wa Hospitali , watumishi,wagonjwa wanachi wa kawaida na viongozi baadhi ya mifano.Viongozi wengi waliohojiwa na kamati yangu wote walikiri kuwa RUSHWA ipo hasa ikizingatiwa kuwa na TAASISI kubwa sana Hospitali hii na kuwa kuwa watumishi wengi na wananma na tabia tofauti. Wote waliofika kwa kamati kutoa maelezo walikiri kuwerpo isipokuwa kukosa ushahidi wa kukamata mtoaji na mpokeaji ni vigumu kwakuwa jambo hili mara ningi hutendwa na watu wawili siriniu na kwa makubaliano ya usiri. Hata watu wanaoombwa rushwa hawapo tayari kutoa ushirikiano wao na vyombo hivyo. Lakini utafiti wa Kamati umeonyesha kuwa wanachi wamepoteza imani na utendaji,usiri, na nia ya watumishi katika vyombo hivyo muhimu ndiyo sababu wanaishia kunung’unika nmitaani.
  Kamati imebaini baadhi ya tabia au vishawishi vitumiwavyo na Wauguzi kushawishi wagonjwa wytoe rushwa ni, kucjelewa kufungua milango ya vyumba vyao, kuingia na kutoka nje mara kwa mara bila kuita mgonjwa yeyote hali ambayo huwashawishi wagonjwa wahisi muuguzi kuhitaji faragha.
  Wagonjwa walioombwa rushwa mf………………………………………………..
  Kamati yangu imebnaini pia kuwa wakati mwingine wagonjwa wenyewe huanza tabia na hamu ya kutoa fedha au rushwa kwa wauguzi.
  ………binti mmoja amefijka hapa anajingojea yeye aliniita na kutaka kunipa fedha Tsha 2,000 ili nimhudumie, mimi nilikataa na kumwambia hiyo ikamsaidiue yeye mwenyewe, mimi sihitaji.
  Mazingira haya yako pande mbili inawezekana kweli mgonbjwa huyu alianza kuhonga tu au pengine aliona hafikiwa na Muuguzi kumjulia hali na mgonjwa akapata nafasi ya kujieleza. Pengine alidhani hii ni njia pekee ya kupata fursa ya kumwona muuguzi. Ni vigumu kutambua hili.
  Hali hiyo Kamati hii ilibaini kwenye Jengo la maabara tarehe,Vitendo vya Mhudumu wa zamu kwenye Chumba cha Maabara kujifungia ndani zaidi ya Saa moja bila kuita mgonjwa yeyote kinatupa maswali mengi. Ambayo kwa watu wa kawaida huwapa majibu mengi mengi


  3.LUGHA MBAYA ZA WAGANGA KWA WAGONJWA* Ward ya Wazazi
  Kamati imefanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa hali hiyo ipo kwa baadhi ya Wauguzi, Wagonjwa walidai kuwa hii ipo inatokana na baadhi ya wagonjwa kutokuwa tayari kutii maelekezo ya wauguzi km usafi,kujiandaa, hasa wakati wa kuzaa.
  Kwa njia hii ya kuwa na Lugha mbaya kwa Wagonjwa na tena kutukaniwa kwa kuhusianisha na Hali ya Uja uzito kuna wakwaza wagonjwa.
  Wazazi kutohudumiwa kwa wakati, Maelezo ya Kiongozi wa Ward ya wazazi aliiambia Kamati kuwa hii inatokamna na
  1. Uhaba wa vifaa km vitanda,na vifaa vya kuzalishia.
  2. Upungufu wa Wauguzi(Wakunga)
  Jambo ambalo wagonjwa hawalitambui huona kuwa wanacheleweshwa tu,kwa namna tu au njia ya wauguzi kutaka cjhochote ili wahudumiwe.

  4.UKOSEFU WA DAWA HOSPITALINI
  Uongozi unakiri kuwa mara kadha hujitokeza upungufu wa dawa Fulani kwenye chumba cha dawa, na hivyo wagonjwa kuelekezwa kwebda maduka ya madawa kujinunulia. Hoja hapa iliyojitokeza si kununua dawa bali ni
  1, Kushurutishwa kwenda kununua dawa kwenye maduka Fulani
  2.Maduka hayo huwa na madawa yaleyale na bei kubwa
  3,Kuhamishia wagonjwa toka hospitali binafsi na kuwaleta kwenye hospitaliu ya Mkoa
  Hali hii inatafsirika vibaya kabisa na wagonjwa na jumuia ya wananchi, Kitendo cha kukosekana kwa Dawa na dawa hizo kupatikana kwenye Maduka yaliyopo ambayo hudhaniwa kuwa ni ya Baadhi ya Madaktari waliopo.
  Kwa sababu hiyo wananchi na wagonjwa waliiambia Kamati ni vigumu kwao kuamini kuwa Dawa hazipatikani hospitalini bali huamini kuwa dawa zinahamishwa toka Hospitalini na kupelekwa kwenye maduka ya Waganga hao.
  Kamati ilipata manung’uniko toka kwa watu wengi wakiwemo viongozi wa Serikali na makundi ya kiraia.
  Katika taarifa ya IPP MEDIA kufuata na dondoo hii kamati imepata uhakika kutoka vianzo vya ndani ya Hospitali kwa masharti ya kutotajwa majina na Wengine walikuwa tayari kutaja majina yao bila woga ili kuhakikisha kile wanachokisema kuwa hawakipendi.

  Kamati imebaini kuwa ukosefu au uhaba wa dawa mara nyingi hutokea kwenye zamu z baadhi ya Madaktari, maana yake ni kuwa ikiwa Daktari Fulani ni zamu yake basi siku hiyo dawa hazitapatikana ila wagonjwa wataelekezwa kwenye duka la madawa( SAJORA,SOMO) Kamati inapendekeza uchunguzi ufanyike wa kina kujua maduka haya yanavyohusiana na malalamiko ya wagonjwa Hospitalini.


  5.UHUSIANO WA MADAKTARI NA MADUKA YA DAWA, ZAHANATI
  Jambo hilo limejitokeza na kulalaminkiwa na wagonjwa wengi, wahudumu na wanachi kuwa, linachangia kwa kiwango kikubwa kutowajibika kwa madaktari ambao hutumia muda wa kazi pia kwa kwenda kutoa huduma za kiu taalamu kwenye hospitali zao , na kuacha hgospitali bila wahudumu wa kutosha.
  Hali hiyo inasababisha p[oia Madaktari kutumia mwanya hio kuhamisha wagonjwa hospitalini kuonyesha kuwa dawa hazipo hospitalini.

  …Daktali fulani akiwa zamu wagonjwa wote wakisha toka chumbani kwake hawarudi dirishani kupata dawa, hilo tumeliona, na tunataka liondolewe tatizo hilo.
  Maduka ya SAJORA,SOMO yamelalamikiwa sana kuhusika kwa njia Fulani na upungufu wa dawa hospitalini, na pia inaonekana kun aq uhusiano Fulani wa Waganga na maduka hayo labda wa faida au vinginevyo.
  Jambo hilo pia limeonekana kuleta maswali hata kwa baadhi ya Wauguzi na Wananchi kwa ujumla. Kamati inafurahi pale ambapo manung’uniko yanakuwepo pande zote.
  Ki msingi hilo ni Tatizo Bodi iliangalie jinsi ya kuliweka ili lisiwe kwazo kwa Waganga wenye Maduka ya madawa au Wananchi wanaohudumiwa.

  6.UPENDELEO KATIKA KUTOA HUDUMA KWA WAGONJWA.
  Kamati ilipata fursa ya kujifunza na kutafuta ukweli wa tuhuma hii Yaliyojitokeza yalionyesha ukweli kuwa hali ya upendeleo ipo, watu watu ambao bila sababu za msingi hufika hospitalini na kupokelewa na waganga na kuhudumiwa bila kuzingatia wale waliowahi. Utafiti umeonyesgha kuwa hao watu mara nyingi ni wale wenye uwezo kifedha zaidi, hutazamwa kipekee.
  Jambo hili linakuwa kero kwa wagonjwa waliowahi kufika kwa huduma.Katika utafiti wa Kamati ilijifunza kuwa Wagonjwa wanajua fika kuwa wapo watu wenye shughuli maalum hao ni lazima wahudumiwe mapema ili waendelee na kazi zao pia wagonjwa mahtuti au vilema. Lakini wanachokilalamikia inaonekana kuwa wapo watu ambao hawana TITLE yeyote lakini hupokelewa na kupewa huduma kasha wengine kuendelea kubaki vitini.


  7.UUZAJI WA DAMU HOSPITALINI.
  Jambo hili limelalamikiwa na wananchi wengi sana kuwa tabia hii mbaya ipo, Wagonjwa hudaiwa kutoa fedha ndipo mgonjwa wao ahudumiwe huduma ya kuongezewa damu.Upo ushahidi mkubwa wa Jambo hilo kutendeka. Sehemu ya maabara kwa muda mrefu imefanya dhambi hii ya kuwauzia wagonjwa damu.
  Mara nyingine mgonjwa alipotaka kuleta mtu wake achangie damu alitishiwa kuwa atalazimika kupimwa ukimwa, nk na kupewa Ushauri nasaha na uchunguzi mkubwa ndipo atoe damu.
  Kwa kuwa watu wengi wanejengwa na hofu ya upimaji wa afya zao hilo lilitosha kuwafanya wakubali kutoa fedha ili waamalize tatizo la damu.
  Mifano halisi…………………………………….

  8.UCHELEWAJI WA WAGANGA KUFIKA HOSPITALINI.
  Kamati imebaini tabia hii ya mWaganga kuchelewa kufika hospitalini mara nyingi na kusababisha mrundikano wa wagonjwa usio na sababu km tarehe za Uchunguzi.
  1.
  2.
  3.
  9.UDHAIFU WA UTAWALA WA HOSPITALI
  Kamati imegumduka kuwa kuna udhaifu sana katika deski la Utawala, kiasi wafanyakazi kila mmoja anafanya atakavyo kana kwamba haluna (job description) Kwamba mtumishi anaingia muda gain kazini na anafanyaje kazi muda huo na kuwa anaondoka muda gain. Ki msingi hakuna fall up kwa watumishi kuwa amefika kazini amafanya nini sau anafanya nini.
  Ilifika na kukaa nje zaidi ya masaa 2 bila kuonekana mgonjwa anayeingia humo au anayetoka au aliyemo ndani ya chumba hicho.
  Malalamiko ya wagonjwa kufika mapema kabla ya wahudumu yamejitokeza sana, inadaiwa kuwa tena baada ya kufika kwa kuchelewa huitishana vikao na ambavyo huchukua muda mrefu hali wagonjwa wako kwenye mangojeo.
  Waganga waliokutana na kamati walikiri kuwepo kwa vikao hivyo muda huo mara kadhaa ambapo nao wakakiri kuwa wao huitwa na wakubwa.


  10.UPUNGUFU WA MADAKTARI NA WATAALAMU
  Hali hiyo nikweli ilijitokeza ipo lakini swali la msingi hao wachache wanawajibika kwa kiwango gain katika shughuli zao za kila siku, na wanepangwaje kulingana na uchache huo

  11.MADAKTARI KUHUDHURIA SEMINA, NA TAASISI AU VITENGO VINGINE
  Kamatio ilibaini kuwa uchaba wa Madaktari upo ni kweli lakini pia hakuna utaratibvu wa kutratibu ushiriki wa mihadhara,semina na mikutano inayotokea. Km utaweza kukuta madaktari watatu wote wanatawanyika kwenda Semina na hospitali inabaki bila Madaktari. Sababu hiyo inachangia malalamiko yaluiyojitokeza ya wagonjwa kufa kabla ya kuhudumiwa na Madaktari.
  Jambo hiloi limelalamikiwa na Watumishi wa Hospitali na pia Wagonjwa wengi.
  Hata kamati teule ilipoikuywa katika uchunguzi wake ilikuta Dr kiongozi hayupo yuko kwenye semina taarifa ambayo hata madaktari wenzake hawakuwa nayo. Huu ni udhaifu wa kiutawala unaosababisha matatizio kwa wagonjwa,Ikumbulwe kuwa Hospitali ni mahala pa wagonjwa wa nafsi na mwili pia wanaohitaji kuwa na Waganga muda wote.

  Waganga wengi wamelalamikia kitendo cha Semina zisizo na utaratibu pamoja na kuwa zina maslahi makubwa kwa MGANGA mwenywe maadili ya KIGANGA si vizuri kuacha wagonjwa wanakufa na wewe kwenda SEMINA.

  Mara tatu kamati yangu imebaini jambo hilo kuwa hakuna viongozi tliowahitaji wako SEMINA vibaya kabisa hata Wasaidizi wao hawajui.
  Baadhi ya Waganga wanalalamikia pia upewndeleo katika kuhudhuria Semina hizo kuwa hakuna usawa kuna harufu ya Upendeleo.

  12.TARATIBU ZA RUFAA KWA WAGONJWA NA WAPI HOSPITALI YA MKOA HUPASWA KUWAPELEKA
  Ilijitokeza tatizo la kuwa wagonjwa hufika hospitalini na baada ya kushindikana huduma hapo huelekezwa kwenda SAJORA,SOMO,BAKWATA nk
  Kamati ilipotaka kujua taratibu za rufaa ilkiwa Hospitali imeshindwa ilielezwa kuwa ni MUHIMBILI,KCMC,MBEYA RUFAA,
  Daktari kiongozi Alifafanua kuwa rufaa wakati mwingine ina mambo kadhaa yaweza kuwa rufaa ya……. Kupelekwa mahali kwenye vifaa vya kisasa kuliko LIGULA
  ……. Kupelekwa mahali kwenye Daktari Bingwa wa Ugonjwa husika.
  Kamati ilijifunza kuwa wagonjwa wanaona picha ya biashara katika mtindo unaotumika,kwani huonekana uhusiano wa zaidi uliojificha katika rufaa hizo.


  13.UKOSEFU WA VIFAA HOSPITALINI
  Baadhi ya watumishi wa Idara walipotakiwa kueleza kwa nini maeneo yao yanaLALAMIMKIWA? Walitoa sababu kuwa, mojawapo ya mambo amboyo yanalalamikiwa ni ucheleweshwaji wa huduma hii ina toka na upungfu wa vifaa
  Mf FRELIMO Uhaba wa Vitanda Mapungufu Vitanda 4
  Mashine kwa upasuiaji Upungufu ni Mashine 3
  Wauguzi

  Maabara Upungufu --- Wanne
  Darubini ---- 3

  Hata hivyo pamoja na sababu ya upungufu wa vifaa huo isingekuwa sababu ya kuwa na mapungufu ya lugha mbaya kwa wagonjwa hilo si wote bali wanasemwa baadhi ya wauguzi.
  Mgangha Mkuu wa Hospitali alipotakiwa kutoa maelezo alisema yeye ameanza kazi hivi karibuni na hivyo anajiweka sawa katika nafasi hiyo. Na kamati yangu ilikubali mtazamo huo kwa kuzingatia kuwa nikweli kamati imeingia mara mbili katika ofisi hiyo kwa nyakati mbili na kukutana na watu wawili tofauti.

  Lakini hata hivyo kamati ingeona si vema mtu akikabidhiwa ofisi asindwe kutoa maelezo kwa kisingizio kuwa yeye ni mgeni. Twatumaini kuwa baada ya kuingia ofisi ni kupanga MARA MOJA MIKAKATI yake si kushangaa ugeni. Na hii ndiyo asili ya viongozi kukosa mwelekeo na kupotoshwa kwani kiongozi anakuwa hana Kitu chake.

  14HALI YA MAWODI KWA UJUMLA
  Mawodi yote na kuona kuwa kwa kiwango hali ya mawodi inaridhisha kiasi, kuna mapungufu makubwa ya KUKOSA VITANDA,MATANDIKO,MASHUKA CHAKAVU,KUKOSA NETI ZA VITANDANI NA MADIRISHANI.
  Vyumba vingine vitanda vingi ni vichakavu sana kiasi cha kuhatarisha afya na usalama wa wagonjwa.
  15.HALI YA MAZINGIRA YA HOSPITALI KWA UJUMLA
  Kwa ujumla viwanja kwa upende wa usoni ni vizuri lakini upende wan yum,a si salama
  16,WATUMISHI KUFANYA KAZI MUDA MREFU WAKIWA WENYEJI
  Jambo hili limelalamikiwa sana na wananchi wanasena ndiyo asili ya vitendo viovu na uzembe kwa baadhi ya wauguzi, wamekuwa wenyeji kupita kiasi hata kusahau wajibu na kuwajibika.
  Na hili linawaletea kutoheshimu mamlaka zilizopo. Na wakati mwingine kutaka mamlaka ziwe chini yao. Hili lilichukuwa uzito kwa Wauguzi wengi wanaona hili ni tatizo kubwa linalopelekea pia kumathiri kiutendaji Mganga Mkuu wa Mkoa.Kamati yangu haipingi mtu kufanyia nyumbani kwake, inachosema hata kama mtu yuko kwake atii,afuate sheria,taratibu,miongozo ya kazi na uwajibikaji wa kila siku.
  Kila mtumishi atambiue mipaka yake ya utendaji wa kila siku.
  17. WANANCHI KUTOJUA TARATIBU ZA HUDUMA.
  Kamati yangu imejifunza kuwa wakati mwingine wananchi wamelalamika mambo mengine kwa tu kutojua taratibu za huduma.
  Km 1. Tofauti ya huduma hospitalini Jumamosi,Jumapili,Sikukuu.
  2. Taratibu za Kuchukua maiti chumba cha maiti.
  3. Taratibu za kufuata hadi kumwona Dr ni zipi
  4. Taratibu za kupata damu ya ndugu yako.
  5. Malipo ya dawa yanatolewa wapi
  6. Huduma za wazee zinatolewaje.
  7. Nini uhusiano kati ya ward ya FRELIMO,TB,MACHO ,MCH,BABKI YA DAMU nk.
  18. MAONI NA MAPENDEKEZO YA WAGONJWA
  19. MAONI NA MAPENDEKEZO YA WAGANGA
  20. MAONI NA MAPENDEKEZO YA WANANCHI
  21. MAONI NA MAPENDEKEZO YA KAMATI
   
 2. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Samahani mkuu waweza kuweka Mapendekezo ya kamati kwa tatizo hili?
   
 3. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Je kamati iliitishwa na nani? Na pili,nini kilitokea hadi kupelekea jambo hili la uundwaji wa tume hiyo? Ni hayo tu..
   
Loading...