Taarifa ya jumuiya ya madaktari kuhusu maamuzi ya serikali kufuatia hotuba ya rais

..... hivyo basi Madaktari Bingwa tumeamua kuacha kufanya kazi ambayo haiendani na kiapo cha Madaktari mpaka hapo Serikali itakapo kubali kurejesha interns wote na kufungua meza ya Majadiliano yenye nia ya dhati ya kumaliza mgogoro......

Mh Rais wa jamhuri ya Muugano .... Tafadhali rudi mezani na hawa watu!

66% ya vikao vyote vya huko nyuma walijadilisi si masilahi yao bali, Uboreshwajwi wa mfumo mzima wa tiba. Was this very difficulty to acknowledge?
 
madaktari wanazungumzia suala la ubora wa huduma ya afya inayotolewa kwa watazanzania kuwa ni miongoni mwa sababu za kugoma kwao.

Raisi wa jamhuri anaeleza kuwa madaktrai wanagoma na hasa shinikizo lao kubwa ni ongezeko kubwa lisilowezekanika la mishahara na kueleza kuwa kwa kuwa serikali haiwezi na haitaweza kulipa hakuna haja ya kugombana na mwajiri ni bora tu anayeona hawezi aache kazi na wala asimlazimishe mwajiri kumwachisha.

Wagonjwa kwa upande wao wanakufa na kutaabika kwa maumivu na mateso makubwa sana huko hospitalini kwa kukosa huduma.

ukiangalia kwa kiasi kikubwa mvutano huu una athari kubwa sana kwa wananchi ambao ndiyo wanaoumia kwa kukosa huduma. Nadhani pande mbili hizi zinapaswa kuacha kulumbana kwani inaonesha kuwa hakuna madhara makubwa ya moja kwa moja yanayoweza kutokea kwa upande wao hata kama mgomo huu utaendelea kwa kipindi kirefu bali madhara ni kwa wananchi
 
Please hapa yanahitajika maombi kwa pande zote mbili.. Maana naona humo ndani kuna taarifa 2. Ya 1.Kamati ya Jumuiya ya Madaktari .Ya 2. Taarifa ya madaktari bingwa kwenye HITIMISHO.
 
"KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA
02.07.2012

PRESS RELEASE

TAARIFA YA JUMUIYA YA MADAKTARI KUHUSU MAAMUZI YA SERIKALI KUFUATIA HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YAWA TANZANIA TAREHE 1 JULAI 2012 JUU YA MGOGORO KATI YA SERIKALI NA MADAKTARI

Utangulizi

Jumuiya ya madaktari imepokea kwa masikitiko hotuba ya Serikali kuipitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ifahamike kuwa mgogoro huu umedumu kwa takribani miezi saba bila kupatikana kwa suluhu ya dhati baina ya pande mbili.

Kutokana na Hotuba iliyotolewa na Mhe Rais ya tarehe 01.07.2012 kwa wananchi wa Tanzania kupitia vyombo vya habari ,Kamati ya Jumuiya ya Madaktari inapenda kutoa ufafanuzi katika mambo yafuatayo:

Ni wazi ikafahamika kuwa mjadala juu ya hoja /madai ya Madaktari kwa mara kadhaa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umekuwa ukizuiwa na Mhe,Spika wa Bunge kwa kigezo kuwa suala hilo liko mahakamani ,je ni sahihi Serikali kutoa maamuzi juu ya suala hilo?

Pia,kuhusu suala la kutekwa ,kupigwa na kuumizwa kikatili kwa Dr.Ulimboka Stephen, Serikali kupitia Jeshi la polisi, lilitangaza kuwa Tume imeundwa ili kuchunguza suala hilo. Mpaka sasa hakuna mwenye uwezo wa kuthibitisha kuwa Serikali haijahusika moja kwa moja, je ni sahihi kwa Mhe,Rais kutamka waziwazi kuwa Serikali haihusiki kwa namna yeyote ile hata kabla ya tume kutoa ripoti yake ya uchunguzi? Hii itatoa uhuru kwa tume ambayo kimsingi imeundwa na Serikali?

Nini dhamira ya Madaktari katika kusuluhisha Mgogoro huu:

Kwa kuamini kuwa Madaktari ni upande muhimu katika kufikia suluhu ya dhati, tulishiriki katika meza ya Majadiliano kwa takribani miezi mitatu,na jumla ya vikao sita vilifanyika, katika vikao hivyo takribani vikao vine kati ya vikao sita (asilimia 66% ya vikao na muda wa vikao) tulijadiliana juu ya Uboreshaji wa huduma ya afya kwa Watanzania. Ni masikitiko yetu kuwa Ripoti ya Ufafanuzi juu ya Hoja/Madai ya Madaktari ya tar 31 Juni 2012, Taarifa ya Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Taarifa ya Waziri Mkuu ndani ya Bunge na hata hotuba ya Rais haikuzungumzia chochote ni kwa jinsi gani serikali itaboresha huduma za afya kwa Watanzania.

Pia tulijadiliana kuhusu Uboreshaji wa Mazingira ya Kazi, ambapo tuliishauri Serikali kupitia kamati ya Majadiliano kuwa ni muhimu kurejesha motisha kwa watumishi wa sekta ya afya kwa kurudisha posho mbalimbali ambazo ziliondolewa.

Kuhusu suala la mshahara, tulishauri serikali iwe wazi kuhusu uwezo wake wa kulipa mishahara. Cha kushangaza ni kwamba, Serikali imekuwa ikitoa taarifa tofauti juu ya ongezeko hilo mfano, Mhe.Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii amelihutubia Bunge kuwa ongezeko ni 15%, hotuba ya Mhe. Rais metoa ongezeko la 20%. Ripoti ya Wataalamu iliyotokana na Kamati ya Waziri Mkuu ilitoa pendekezo la 25%. Je nia ya Serikali iko wapi?

Wakati viongozi wa Serikali wakitoa taarifa zinazotofautiana, Ripoti ya Ufafanuzi wa madai/hoja ya Madaktari iliyotoka na Majadiliano sisi tukiwa wajumbe haikutoa pendekezo(ofa) yoyote juu ya ongezeko la mshahara.

HITIMISHO

Kwa kuwa kuendelea kufanya kazi katika mazingira haya ndugu zetu Watanzania wazalendo wengi wamepoteza maisha kutokana na ukosefu wa vifaa tiba na madawa.
Na kwa kuwa tumefanya kwa miaka mingi sana tukishuhudia haya tunadhani muda umefika wa kubadilisha hali hii na kuwasaidia ndugu zetu Watanzania.
Na kwa kuwa Serikali imeshindwa kuweka mazingira ya kazi kuwa bora na kuwezesha huduma bora kwa wananchi na watoa huduma, hivyo basi Madaktari Bingwa tumeamua kuacha kufanya kazi ambayo haiendani na kiapo cha Madaktari mpaka hapo Serikali itakapo kubali kurejesha interns wote na kufungua meza ya Majadiliano yenye nia ya dhati ya kumaliza mgogoro.

Kamati ya Jumuiya ya Madaktari

Imesainiwa na
"Katibu Jumuiya ya Madaktari."
Ndugu dactari kumbuka wewe ni Mtanzania ulie toka kule shinyanga, kagera, mara, sumbawanga na kwingineko kwingi ambako leo hii bado mtanzania wa hali ya chini mtoto wake anakwenda shule ya msingi hata secondary bila viatu kwa ajili ya ugumu wa maisha, pia kumbuka mtanzania huyu ndie kodi yake unaidai wewe upewe gari mshahara milion tatu na marupurupu kubao, sidhani kama ni busara, "from what i know there is some one behind you" DOCTOR kumbuka kabla hujawa dactari ulipitia uanafunzi, ambako ulifundishwa na walimu, je ulisha hoji wanalipwa mshahara Tsh. ngapi? ukitajiwa unaweza kushika mdomo, kama sio kulia kabisa.
Hebu fikiria wewe bila walimu ungewezaje kuwa dactari? fikiria wao wangegoma wakati wewe ukiwa mwanafunzi ungeweza kufikia malengo yako?. Sambamba na hili mkataba wa ajira ulijaza ukiwa umefumba macho, vip leo unakuwa kigeu geu, RUDISHA UZALENDO, MNAUWA WATU WASIO NA HATIA, "MATATIZO YOTE HAYA KAYATAKA NYERERE"

si muache kabisa kazi? Kuweni wawazi ni mazingira gani mnataka yaboreshwe? Milion 7.7?

Hivi kwanini mnakuwa wabinafsi sana nyie Ma-DR, kama mnataka mazingira bora ya kazi kwa nini msidai na ya walimu, wahandisi, wahasibu, maendeleo ya jamii n.k ambao pia wangependa mazingira bora ya kazi?

Kuna kitu sielewi, hv kwa nini wanadai suala la maslahi na madai yao lijadiliwe na bunge? Kwani wao ni wabunge au wameweka watu gani kule wa kuwatetea au ndo mmetumwa na baadhi ya wabunge ambao watawatetea suala likijadiliwa na bunge?

Let us be fair Dr's kwa watumishi wengine pia wanayatamani
 
Hakuna haja ya kulia lia hapa kwani hiyo mil 7.7 itapatikana humu?? acha kazi basi.... unaziba nafasi za wengine wapo wanaohitaji huo mshahara unaougomea wewe... Mmeprove ubinafsi wenu na mpo kimaslahi zaidi vueni hayo makoti mkagombee majimboni mtapata zaidi ya 7.7
 
MHESHIMIWA KATIBU... MBONA HUJAONGELEA SUALA LA MSHAHARA WA TSHS. 3,500,000/=MNAODAI ULIPWE WA KUANZIA KWA MHITIMU WA DEGREE YA KWANZA PALE MUHAS? Naona hapa ndio mliingia porini vibaya na Mh. Raisi akapata kitu cha kuongelea na kuwaponda vibaya. Kwa mshahara huo mnajionesha kabisa mlivyo wabinafsi na mnavyotaka kujinufaisha kibinafsi.

pitia vizuri tamko la madaktari kuhusu kipengere cha mshahara: kama sikosei tamko lineainisha kuwa serikali haina uwezo, madaktari wakaitaka serikali iseme inauwezo gani, hapo ndo serikali ikatoa viwango tofauti: waziri wa afya; 15%, PM; 20%, pres 25%. Kwahiyo serikali haina tamko la pamoja
 
additional point.. government yenyewe inajichanganya ikiwa inahutubia kuhusu mgomo...
 
Ni hicho tu madaktari hadi mama wajawazito wanakufa na ujauzito wao,naugu wanakosa hata panado ambazo walikuwa wanapata na zinawasaidia,
Ludini kazini huo sio uzalendo hata kidogo,ni uuwaji.
SIONO KILICHAWAFANYA MUGOME,

MMEACHA KUFANYA KAZI,MMEACHA KUFANYA KAZI,AU MMEACHA KAZI.

MUWE WAZI,MMEACHA KAZI AU HAMFANYI KAZI,

BASI WOTE WALIOZIDIWA KAMA DR ULI WAPELEKENI NJE KAMA NYIE NI BINADAMU KWELI NA MNAHASIRA NA SERIKALI NA SIO WALALA HOI.

Kama kweli wewe ni mwalimu na kuna waalimu wengine wa aina yako basi tumekwisha!
 
Jibu la mgogoro huu wa Madaktari na Serikali wanalo Watanzania kwa ujumla wao.
Ni bahati mbaya tu kwamba Serikali yao haisikilizi wanasema nini kuhusu mgawanyo wa Raslimali zao kwa raia wake kulingana na vipau mbele vyao na badala yake raslimali hizo zinagawiwa kwa watu wasiostahili na Serikali bila kujali matakwa ya Wananchi.Mfano tu mmoja haiingii akilini kukusanya watu na kuwaita Wakuu wa Wilaya bila kujua kazi zao ni zipi na kuwalipa Mishahara minono na masurufu lukuki pasipo kuwa na tija na ukawaacha Madokta wanaofanya watu wote wawe na uwezo wa kufanya kazi zao kwa ufanisi.
 
Ndugu dactari kumbuka wewe ni Mtanzania ulie toka kule shinyanga, kagera, mara, sumbawanga na kwingineko kwingi ambako leo hii bado mtanzania wa hali ya chini mtoto wake anakwenda shule ya msingi hata secondary bila viatu kwa ajili ya ugumu wa maisha, pia kumbuka mtanzania huyu ndie kodi yake unaidai wewe upewe gari mshahara milion tatu na marupurupu kubao, sidhani kama ni busara, "from what i know there is some one behind you" DOCTOR kumbuka kabla hujawa dactari ulipitia uanafunzi, ambako ulifundishwa na walimu, je ulisha hoji wanalipwa mshahara Tsh. ngapi? ukitajiwa unaweza kushika mdomo, kama sio kulia kabisa.
Hebu fikiria wewe bila walimu ungewezaje kuwa dactari? fikiria wao wangegoma wakati wewe ukiwa mwanafunzi ungeweza kufikia malengo yako?. Sambamba na hili mkataba wa ajira ulijaza ukiwa umefumba macho, vip leo unakuwa kigeu geu, RUDISHA UZALENDO, MNAUWA WATU WASIO NA HATIA, "MATATIZO YOTE HAYA KAYATAKA NYERERE"

unajua neno uzalendo linatumika tofaut kabisa,,,kwanin raia tunahubiriwa UZALENDO????wakat hawa wadau wa huko juu hawana uzalendo????what kind of uzalendo unaaongelewa hapa,,,,,,?wa kufanya kazi mazingira magumu,wa kutembelea vx,wa kupata ujira mdogo???wa kuiba mali ya umma,nani anapaswa kuonesha uzalendo kwanza,mwananchi au kiongozi ????au nani????kati yangu na mbunge au waziri au rais nani anapaswa kuwa mzalendo???mwalim akifa na jaa huku akiwa darasan ndo mzalendo????au mbunge anayekufa akiwa bungen tena kifo kinamzoa akiwa anasinzia????tujiulize haya maswali,,,maana watawala wanahubiri uzalendo,ila nadhan hawaujui
 
Ni hicho tu madaktari hadi mama wajawazito wanakufa na ujauzito wao,naugu wanakosa hata panado ambazo walikuwa wanapata na zinawasaidia,
Ludini kazini huo sio uzalendo hata kidogo,ni uuwaji.
SIONO KILICHAWAFANYA MUGOME,

MMEACHA KUFANYA KAZI,MMEACHA KUFANYA KAZI,AU MMEACHA KAZI.

MUWE WAZI,MMEACHA KAZI AU HAMFANYI KAZI,

BASI WOTE WALIOZIDIWA KAMA DR ULI WAPELEKENI NJE KAMA NYIE NI BINADAMU KWELI NA MNAHASIRA NA SERIKALI NA SIO WALALA HOI.

Madaktari haoni kazi ya kufanya hata kama wakiingia kazi maana katika mahospitali ya serikari kila kitu hamna. Na viongozi wanalifahamu hilo ndio maana familia zao hata zikipata mafua tu haraka sana wanakodi ndege ng'ambo. Kwa maana hiyo naunga mkono "HOJA YA MADAKTARI"
 
ww ni mmoja wa wale mnaofikirishwa na upuuzi wa magamba hakuna sehemu madr wamengangania mshahara wa milion 3,wao madr hoja ya msingi ni kurekebishwa kwa mazingira ya kufanyia kazi ili waweze kuwahudumia watanzania kwa ufanisi ,au kwa kua ww pamoja na hao mafisadi wako unaowatetea hua mnatibiwa ulaya pamoja na mahawala zenu ndo maana mnatetea dhuluma wanaofanyiwa madr wetu
 
naunga mkono mgomo wa wa DR kwa sababu wanatupigania tupewe haki ya kutibiwa kwa vifaa bora wale wanaopinga ni mafisadi na vibaraka wao ambao hua wanapelekwa ulaya wakiugua pumbafu zenu wote ambao hamuungi mkono madr
 
Ni hicho tu madaktari hadi mama wajawazito wanakufa na ujauzito wao,naugu wanakosa hata panado ambazo walikuwa wanapata na zinawasaidia,
Ludini kazini huo sio uzalendo hata kidogo,ni uuwaji.
SIONO KILICHAWAFANYA MUGOME,

MMEACHA KUFANYA KAZI,MMEACHA KUFANYA KAZI,AU MMEACHA KAZI.

MUWE WAZI,MMEACHA KAZI AU HAMFANYI KAZI,

BASI WOTE WALIOZIDIWA KAMA DR ULI WAPELEKENI NJE KAMA NYIE NI BINADAMU KWELI NA MNAHASIRA NA SERIKALI NA SIO WALALA HOI.

wewe huna VISION.nitafatilia sana comment zako ili nikuelewe vizur.
 
Ni hicho tu madaktari hadi mama wajawazito wanakufa na ujauzito wao,naugu wanakosa hata panado ambazo walikuwa wanapata na zinawasaidia,
Ludini kazini huo sio uzalendo hata kidogo,ni uuwaji.
SIONO KILICHAWAFANYA MUGOME,

MMEACHA KUFANYA KAZI,MMEACHA KUFANYA KAZI,AU MMEACHA KAZI.

MUWE WAZI,MMEACHA KAZI AU HAMFANYI KAZI,

BASI WOTE WALIOZIDIWA KAMA DR ULI WAPELEKENI NJE KAMA NYIE NI BINADAMU KWELI NA MNAHASIRA NA SERIKALI NA SIO WALALA HOI.

Labda hujawaelewa na huelewi mgogoro mzima uliopelekea mgomo wa Madr.

Wanasema kuwa hawawezi kuendelea kuona ndugu zao Watanzania wanapoteza maisha kwa kukosa huduma iliyo bora, kukosa vifaa, madawa, na mashine za vipimo.

Serikali inatumia pesa nyingi sana kuwapeleka viongozi kutibiwa nje, kitu ambacho kinawezekana kwani pia Tanzania tuna madr bingwa, kule nje wanafuata vipimo na huduma bora. Ile pesa kwa nini wasinunue vifaa na kuweka katika hospitali zetu ili wote tunufaike.

Kumbuka pesa inayowatibia viongozi nje ni ya kwako na yangu, labda kama wewe hulipi kodi za serikali hapo utakuwa uhusiki na ile pesa.

KWa nini basi na sisi tusipelekwe wote nje kutibiwa kaw pesa ya serikali???

Watumishi wa afya wanafanya kazi katika mazingira magumu, fikiria hakuna mtu anayependa kumuona binadamu mwenzie anapteza maisha kwa sababu eti amekosa msaada mdogo ambao upo ndani ya uwezo.

Hotuba ya rais ya juzi imekaa kisiasa mno kuliko ubinadamu.

Na wote mnaoshabikia serikali katika suala hili linalogusa maisha yetu wote mpo katika hali ya kisiasa.

BADILIKENI TUIKOMBOE TANZANIA.

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Madaktari haoni kazi ya kufanya hata kama wakiingia kazi maana katika mahospitali ya serikari kila kitu hamna. Na viongozi wanalifahamu hilo ndio maana familia zao hata zikipata mafua tu haraka sana wanakodi ndege ng'ambo. Kwa maana hiyo naunga mkono "HOJA YA MADAKTARI"

hapo kwenye red...........
well said - na mimi NAUNGA MKONO HOJA YA MADAKTARI.
 
jk ni mhongo anatengeneza uongo ili apate sapot ya wananchi akifikili ya kwamba wanchi bado ni mazuzu. hapo amepotea
 
Back
Top Bottom