Taarifa ya jumuiya ya madaktari kuhusu maamuzi ya serikali kufuatia hotuba ya rais

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
"KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA
02.07.2012

PRESS RELEASE

TAARIFA YA JUMUIYA YA MADAKTARI KUHUSU MAAMUZI YA SERIKALI KUFUATIA HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YAWA TANZANIA TAREHE 1 JULAI 2012 JUU YA MGOGORO KATI YA SERIKALI NA MADAKTARI

Utangulizi

Jumuiya ya madaktari imepokea kwa masikitiko hotuba ya Serikali kuipitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ifahamike kuwa mgogoro huu umedumu kwa takribani miezi saba bila kupatikana kwa suluhu ya dhati baina ya pande mbili.

Kutokana na Hotuba iliyotolewa na Mhe Rais ya tarehe 01.07.2012 kwa wananchi wa Tanzania kupitia vyombo vya habari ,Kamati ya Jumuiya ya Madaktari inapenda kutoa ufafanuzi katika mambo yafuatayo:

Ni wazi ikafahamika kuwa mjadala juu ya hoja /madai ya Madaktari kwa mara kadhaa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umekuwa ukizuiwa na Mhe,Spika wa Bunge kwa kigezo kuwa suala hilo liko mahakamani ,je ni sahihi Serikali kutoa maamuzi juu ya suala hilo?

Pia,kuhusu suala la kutekwa ,kupigwa na kuumizwa kikatili kwa Dr.Ulimboka Stephen, Serikali kupitia Jeshi la polisi, lilitangaza kuwa Tume imeundwa ili kuchunguza suala hilo. Mpaka sasa hakuna mwenye uwezo wa kuthibitisha kuwa Serikali haijahusika moja kwa moja, je ni sahihi kwa Mhe,Rais kutamka waziwazi kuwa Serikali haihusiki kwa namna yeyote ile hata kabla ya tume kutoa ripoti yake ya uchunguzi? Hii itatoa uhuru kwa tume ambayo kimsingi imeundwa na Serikali?

Nini dhamira ya Madaktari katika kusuluhisha Mgogoro huu:

Kwa kuamini kuwa Madaktari ni upande muhimu katika kufikia suluhu ya dhati, tulishiriki katika meza ya Majadiliano kwa takribani miezi mitatu,na jumla ya vikao sita vilifanyika, katika vikao hivyo takribani vikao vine kati ya vikao sita (asilimia 66% ya vikao na muda wa vikao) tulijadiliana juu ya Uboreshaji wa huduma ya afya kwa Watanzania. Ni masikitiko yetu kuwa Ripoti ya Ufafanuzi juu ya Hoja/Madai ya Madaktari ya tar 31 Juni 2012, Taarifa ya Mhe. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Taarifa ya Waziri Mkuu ndani ya Bunge na hata hotuba ya Rais haikuzungumzia chochote ni kwa jinsi gani serikali itaboresha huduma za afya kwa Watanzania.

Pia tulijadiliana kuhusu Uboreshaji wa Mazingira ya Kazi, ambapo tuliishauri Serikali kupitia kamati ya Majadiliano kuwa ni muhimu kurejesha motisha kwa watumishi wa sekta ya afya kwa kurudisha posho mbalimbali ambazo ziliondolewa.

Kuhusu suala la mshahara, tulishauri serikali iwe wazi kuhusu uwezo wake wa kulipa mishahara. Cha kushangaza ni kwamba, Serikali imekuwa ikitoa taarifa tofauti juu ya ongezeko hilo mfano, Mhe.Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii amelihutubia Bunge kuwa ongezeko ni 15%, hotuba ya Mhe. Rais metoa ongezeko la 20%. Ripoti ya Wataalamu iliyotokana na Kamati ya Waziri Mkuu ilitoa pendekezo la 25%. Je nia ya Serikali iko wapi?

Wakati viongozi wa Serikali wakitoa taarifa zinazotofautiana, Ripoti ya Ufafanuzi wa madai/hoja ya Madaktari iliyotoka na Majadiliano sisi tukiwa wajumbe haikutoa pendekezo(ofa) yoyote juu ya ongezeko la mshahara.

HITIMISHO

Kwa kuwa kuendelea kufanya kazi katika mazingira haya ndugu zetu Watanzania wazalendo wengi wamepoteza maisha kutokana na ukosefu wa vifaa tiba na madawa.
Na kwa kuwa tumefanya kwa miaka mingi sana tukishuhudia haya tunadhani muda umefika wa kubadilisha hali hii na kuwasaidia ndugu zetu Watanzania.
Na kwa kuwa Serikali imeshindwa kuweka mazingira ya kazi kuwa bora na kuwezesha huduma bora kwa wananchi na watoa huduma, hivyo basi Madaktari Bingwa tumeamua kuacha kufanya kazi ambayo haiendani na kiapo cha Madaktari mpaka hapo Serikali itakapo kubali kurejesha interns wote na kufungua meza ya Majadiliano yenye nia ya dhati ya kumaliza mgogoro.

Kamati ya Jumuiya ya Madaktari

Imesainiwa na
"Katibu Jumuiya ya Madaktari."
 
haya sasa liwalo na liwe,haya tuone mwisho,mwishowe wananchi tutagoma kwenda maofisi kwa sababu lolote likitokea hauwezi tibiwa hapo sasa
 
Ni hicho tu madaktari hadi mama wajawazito wanakufa na ujauzito wao,naugu wanakosa hata panado ambazo walikuwa wanapata na zinawasaidia,
Ludini kazini huo sio uzalendo hata kidogo,ni uuwaji.
SIONO KILICHAWAFANYA MUGOME,

MMEACHA KUFANYA KAZI,MMEACHA KUFANYA KAZI,AU MMEACHA KAZI.

MUWE WAZI,MMEACHA KAZI AU HAMFANYI KAZI,

BASI WOTE WALIOZIDIWA KAMA DR ULI WAPELEKENI NJE KAMA NYIE NI BINADAMU KWELI NA MNAHASIRA NA SERIKALI NA SIO WALALA HOI.
 
Sasa mnadai interns warudi na mazungumzo yaendelee! Wtf! Nyie madaktari mna-behave kama sio wasomi, full ujinga!
 
Mhmh hawa mafahali wawili wanazidi kuvutana na inaonekana we have a long way to go maana kila mmoja anatunisha misuli...

Babu wa Loliondo na watoa vikombe wengine hebu rudisheni huduma maana nyie ndio mtakuwa kimbilio kwa siku za usoni, iiteni mizimu yenu ku re-charge battery kama charge imeisha
 
MHESHIMIWA KATIBU... MBONA HUJAONGELEA SUALA LA MSHAHARA WA TSHS. 3,500,000/=MNAODAI ULIPWE WA KUANZIA KWA MHITIMU WA DEGREE YA KWANZA PALE MUHAS? Naona hapa ndio mliingia porini vibaya na Mh. Raisi akapata kitu cha kuongelea na kuwaponda vibaya. Kwa mshahara huo mnajionesha kabisa mlivyo wabinafsi na mnavyotaka kujinufaisha kibinafsi.
 
serikali irudi kwenye meza ya mazungumzo na iache propaganda
 
Ni hicho tu madaktari hadi mama wajawazito wanakufa na ujauzito wao,naugu wanakosa hata panado ambazo walikuwa wanapata na zinawasaidia,
Ludini kazini huo sio uzalendo hata kidogo,ni uuwaji.
SIONO KILICHAWAFANYA MUGOME,

MMEACHA KUFANYA KAZI,MMEACHA KUFANYA KAZI,AU MMEACHA KAZI.

MUWE WAZI,MMEACHA KAZI AU HAMFANYI KAZI,

BASI WOTE WALIOZIDIWA KAMA DR ULI WAPELEKENI NJE KAMA NYIE NI BINADAMU KWELI NA MNAHASIRA NA SERIKALI NA SIO WALALA HOI.

we si ticha kama unavyojinadi nahisi we nimlevi mmoja tu ,umelewa matapu tapu ya 300 huoni maana ya kudai ongezeko la mshahara wa Dr ama we ni mwalimu uliye soma memkwa.
 
si muache kabisa kazi? Kuweni wawazi ni mazingira gani mnataka yaboreshwe? Milion 7.7?
 
Ile button ya 'like' itabidi tuipiganie iwekwe hapa JF, nimeitafuta nimeikosa kabisa! Basi ngoja tu niseme 'I LIKE THIS'
si muache kabisa kazi? Kuweni wawazi ni mazingira gani mnataka yaboreshwe? Milion 7.7?
 
ila nyie madoct sijui mmetok nch gan, unashindw kuwa wazalend , kuwa nahuruma, anaye sapot uo mgom ngoja aumwd mama yak ndio atajua raha yake, so stupid wao na ndug zao wanatibiw viongoz wote na ndug zao wanatibiw nje , wanamkomoa nani , Endeleni ila tambuen ualimu na uuguzi ni wito, naungan na Dokt Jakay kama mnaona hamuwez achen kaz
 
Vitabu vya Mungu vinasema kuwa, siku za mwisho upendo utapoa kati ya ndugu na ndugu, watu watakuwa wabinafsi, wenye kujipenda nafsi zao, wenye kupenda pesa, maradhi yasiyotibika n.k. Tupige magoti na kumuomba Mungu atuponye na majanga haya yanayotokea katika nchi yetu. Zaidi ya yote amani.
 
ila nyie madoct sijui mmetok nch gan, unashindw kuwa wazalend , kuwa nahuruma, anaye sapot uo mgom ngoja aumwd mama yak ndio atajua raha yake, so stupid wao na ndug zao wanatibiw viongoz wote na ndug zao wanatibiw nje , wanamkomoa nani , Endeleni ila tambuen ualimu na uuguzi ni wito, naungan na Dokt Jakay kama mnaona hamuwez achen kaz
Kaka jelome, sijui kama jina lako au la, maana unakosea hata kuliandika; Udokta wa kupewa hauna raha kama wa kusomea
 
Last edited by a moderator:
Ile button ya 'like' itabidi tuipiganie iwekwe hapa JF, nimeitafuta nimeikosa kabisa! Basi ngoja tu niseme 'I LIKE THIS'
ARV nadhani umeathirika na huu ugonjwa mpya. Kwa mwendo huu utapenda hadi vinyesi
 
Last edited by a moderator:
Ni hicho tu madaktari hadi mama wajawazito wanakufa na ujauzito wao,naugu wanakosa hata panado ambazo walikuwa wanapata na zinawasaidia,
Ludini kazini huo sio uzalendo hata kidogo,ni uuwaji.
SIONO KILICHAWAFANYA MUGOME,

MMEACHA KUFANYA KAZI,MMEACHA KUFANYA KAZI,AU MMEACHA KAZI.

MUWE WAZI,MMEACHA KAZI AU HAMFANYI KAZI,

BASI WOTE WALIOZIDIWA KAMA DR ULI WAPELEKENI NJE KAMA NYIE NI BINADAMU KWELI NA MNAHASIRA NA SERIKALI NA SIO WALALA HOI.
Ticha najua unatumia vyeti visivyokuwa vyako, ndio maana unaridhika na kamshahara kako. Kama wewe unalipwa stahili yako, waache wenye thamani kubwa watafute thamani yao.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom