Taarifa ya Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya kwa vyombo vya habari tarehe 04.12.2014

Mapengo 17

R I P
Mar 28, 2014
1,232
609
Mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha lyeselo wilayani Chunya aliyefahamika kwa jina la Gibson Mlawaya (80) anashikiliwa na Jeshi hilo akiwa na silaha (bunduki) moja aina ya gobole pamoja na gololi na baruti zinazotumika katika silaha hiyo.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 03.12.2014 majira ya saa 10:00 asubuhi katika msako uliofanyika huko katika Kitongoji cha Lyeselo, Kata ya Lupa, Tarafa ya kipembawe, Wilaya ya Chunya, mtuhumiwa ni muwindaji haramu, taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.

Katika tukio la pili mtu mmoja mkazi wa Kijiji cha Wanzani Wilayani Chunya aliyefahamika kwa jina la Gibson Morice Philipo (34) mfanyabiashara anashikiliwa na Jeshi hilo akiwa na pombe kali (viroba) zilizopigwa marufuku nchini aina ya ridder paketi 10 akiuza katika kibanda chake.

Mtuhumiwa alikamatwa tarehe 03.12.2014 majira ya saa 11:00 asubuhi katika msako uliofanyika huko katika kijiji cha wanzani, kata ya mbuyuni, tarafa ya songwe, wilaya ya chunya, mkoa wa mbeya. mtuhumiwa ni muuzaji wa pombe hizo, taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.

Kamanda wa polisi mkoani humo, kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Mhmed Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kujimilikisha silaha kinyume cha sheria na badala yake wafuate taratibu za umilikaji wa silaha kupitia mamlaka husika.

Aidha anatoa wito kwa yeyote anayemiliki silaha kinyume cha sheria asalimishe silaha hiyo/hizo kabla ajakamatwa na vyombo vya dola.

Pia anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia pombe kali zilizopigwa marufuku kwani ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
 

Attachments

  • Mbeya..docx
    94.4 KB · Views: 99
Back
Top Bottom