Taarifa ya IMF: Mamlaka za Tanzania zimegoma kutoa kibali cha kuchapisha data za uchumi

Dalili zote zinaonesha nchi inayumba...

Ukianza kwa ngazi ya mwananchi hadi juu..
Uchumi ulikuwa unakua kwa kasi ya kupungua na si kuongezeka hilo tu linaonesha kuwa uchumi ulikuwa unashuka...

Hizo zote ni projections/ makadirio ila serikali inajua fika report ya IMF itaathiri vipi uwekezaji maana hakuna muwekezaji kichaa atategemea kuwekeza Tanzania kwa kutumia data za serikali tu yaani ni lazma wachukue na data za mashirika ya nje..
 
Bahati mbaya JIWE hajui hilo.

Anamuiga Kagame kufanya mauaji lakini ameshindwa kumuiga namna ya kuishi na hawa watu.

Tumekuwa taifa la wapumbavu, tulishafanya mambo 1961 yakabuma lakini leo tena 2019 tunafanya vile vile huku wakubwa wakichekelea wakiamini tunaenda vizuri.

- Tulishazinguana na hawa IMF/WB yakatukuta makubwa tena wakati tuna Rais Genious, leo tuna takataka. Sijui.

- Serikali ilifeli kufanya biashara wakati wa Rais Genious, eti leo takataka inajidai inajua how business works !!

Na tunaelekea kaburi refu sana
Serikali imebore sana hasa pale ilipoanza kuuza hata pen kwenye taasis zake haitaki watu binafsi kufanya hiyo kazi.
 
IMF YAILAUMU TANZANIA KWA KUTOCHAPISHA MATOKEO YA UTAFITI

Mnamo Machi 18/2019, Bodi ya Shirika la Fedha Duniani(IMF) ilifanya kikao cha mashauriano kuhusu hali ya uchumi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Hata hivyo IMF imeeleza kuwa Mamlaka za Tanzania hazijachapisha taarifa ya kikao hicho ili Umma ufahamu

Aprili 10, 2019, IFM ilitoa taarifa ya tathmini ya ukuaji wa Uchumi wa Tanzania na kueleza kuwa Uchumi utakuwa kwa 4% mwaka huu na 4.2% mwaka 2020

Taarifa hiyo ilikinzana na makadirio ya Serikali ya Tanzania iliyoeleza kuwa inatarajia Uchumi utakuwa kwa 7.3%


Statement on the 2019 Article IV Consultation with the United Republic of Tanzania Staff Report
April 17, 2019

On March 18, 2019, the Executive Board of the International Monetary Fund concluded the consideration of the 2019 Article IV Consultation with the United Republic of Tanzania.

Under Article IV of its Articles of Agreement, the IMF has a mandate to exercise surveillance over the economic, financial and exchange rate policies of its members in order to ensure the effective operation of the international monetary system. The IMF’s appraisal of such policies involves a comprehensive analysis of the general economic situation and policy strategy of each member country. IMF economists visit the member country, usually once a year, to collect and analyze data and hold discussions with government and central bank officials. Upon its return, the staff submits a report to the IMF’s Executive Board for discussion. The Board’s views are subsequently summarized and transmitted to the country authorities.

The authorities have not consented to publication of the staff report or the related press release.

IMF Communications Department
MEDIA RELATIONS
PRESS OFFICER:
LUCIE MBOTO FOUDA
PHONE: +1 202 623-7100
EMAIL: MEDIA@IMF.ORG

Haipendezi mtu binafsi (an individual) kuwa na tabia ya kuongopa. Je, taifa la watu waongo linakuwa vipi? Tujue kuwa serikali inapandikiza vimelea vya utamaduni wa kuongopa.
 
Mwalimu Nyerere alizinguana na hawa hawa jamaa kupitia ile SAP, ikatucost big time mpaka akalazimika kung'atuka.

Sijui kwanini Magufuli ameamua kufuata njia za mtu aliyeshindwa kuendesha nchi na kutuharibia uchumi..

Namuamini sana jiwe ila kukopi failed policies za JK Senior ndipo anapokwama.
Nyerere alichukua policy ya ujamaa na kuileta Tanzania na SAP ilikuwa kinyume na misimamo yake. Kama uliisoma SAP na kuielewa bhasi ungejua kwa nini jombaa aling'atuka kabla ya kuona CV yake ikichafuliwa, alifanya right move

Kwa sasa soko huria ndio notion na haliepukiki na kwa uchumi wa nchi yetu ambao public sector imefeli kulihimili soko then private sector ni muhimu zaidi.. Impact kubwa ya hii move ni kuondoa ujasiri kwa wawekezaji wa nje maana risk itakuwa kubwa zaidi
 
Kwanini nchi nyingi Africa inakuwa vigumu sana kuamini watalaam wake? tuna miaka Zaidi ya 50 bado hatuna uwezo wa kujifanyia tathimini wenyewe na kutoa report kwa Taasisi mbalimbali just for certification? , mambo ya fedha ( exchange rate) kila nchi duniani kote ni mambo ya nchi husika, ndio maana kila siku marekani wanapigana na china kuhusu haya mambo, hata marekani huwezi kupata data zao za uchumi kabla ya serikali au chombo husika kutoa report, ni kawaida. Ila kwa kuwa sisi hatujiamini data zikitoka utasikia wanasiasa wanaongea hili mara lile wakati huo hata utalaam wa fedha/uchumi hawana, hata kama ni IMF lazima waje nchini washirikiane na taasisi zetu, wapo nchini kupata taarifa na mwenendo wa uchumi nchini , hata kama wakiwa na data zinaweza kupokelewa na kujadiliwa au kukataliwa, sio kila kitu IMF wamesema IMF wamesema IMF blabla basi sisi tunakubali tu.
Mkuu Wo Shi Niubi kama 40% ya bajeti yako yote ya mwaka ni tegemezi, IMF huwezi kuwakwepa kwa sababu unapoenda kuwapigia magoti wanakutathmini kwanza halafu ndiyo unapewa hiyo hela na hapo ndiyo inabidi wajue hela Yao inatumikaje?
Pili IMF wamesema wanafanya zoezi hilo kila mwaka kwa nchi wanachama hivyo kama Tanzania ni mwanachama nashauri tutoe tu ushirikiano kwa kuwa kama vile ndoa haya tuliyajua kabla.
Mapendekezo kuondokana au kupunguza fedheha hii ni kutokuwa na bajeti tegemezi. China na USA ulizozitaja hawana udhaifu tulio nao. Kwa nchi Africa Mashariki ni Kenya peke yake haina bajeti tegemezi. KRA inakusanya Ksh. 1.6tr kwa mwezi kati ya hizo Ksh. 1tr zinatumika kwa matumizi ya kawaida na zilizobaki kwa ajili ya maendeleo.
Tuna cha kujifunza toka kwa watani zetu.
 
Magu ndiye mtu pekee duniani anayenunua ndege kwa CASH, yaani hakuna nchi inafanya kitu kama hicho alafu analaumu hela ya Tanzania kushuka thamani? Kwa nini isishuke thamani kama serikali inamwaga mablioni IN CASH kununua ndege.
Thamani ya hela inashuka kukiwa na sellers wengi kuliko buyers kwenye market, hela yote ya bongo tunayogeuza to USD kununua hizi ndege sio pesa ndogo, ongeza na matumizi mengine yanayolipwa in usd toka Magu aingie huu ni mwanzo tu. Huyu jamaa akipewa mitano mingine ataiacha bongo pabaya sana, serikali itaown almost kila kitu huku wananchi wengi watakua wanakufa njaa. System anayotumia huyu jamaa haijawahi fanikiwa toka binadamu aanze kurecord history, chungulia venezuela kinachoendelea.
 
Tanzania ijitoe uanachama wa IMF ili iweze kupika data zake vile wanavyopenda.
Wanasema nambari hazidanganyi.

Wacha mwenyekiti na chama waendelee kutugawia umasikini kwa mwendokasi.

Kitaa maisha ni magumu kweri kweri.
IMF wanasema uchumi unakua kwa asilimia 4, sasa wapika data hawataki wanataka za kwao kuwadanganya watanzania
 
Hii kweli inaleta tabu sana, mpaka hawataki kuruhusu taarifa kuchapishwa inamaana kuna vitu wanaficha ambavyo ni ukweli kuwa uchumi unakuwa kwa kwa asilimia ndogo sana.
 
Good. Waweke tu uozo wote humu mitandaoni. Washamba kupewa nchi imekuwa tabu kila kona. Na bado wanajitutumua wakati nchi imewashinda.
 
Mwisho wa utawala wa ccm ni 2020. Tanzania Kwa sasa ni kama jangwa ambalo uoto wake wa asili ni nyasi. Jangwa hili limepigwa na jua Kali kiasi kwamba nyasi zote zimekauka. Yeyote atakaetupa kishungi cha moto jangwa lote litashika moto ambao kuuzima kwake hauwezekani. 2020
 
Dalili zote zinaonesha nchi inayumba...

Ukianza kwa ngazi ya mwananchi hadi juu..
Uchumi ulikuwa unakua kwa kasi ya kupungua na si kuongezeka hilo tu linaonesha kuwa uchumi ulikuwa unashuka...

Hizo zote ni projections/ makadirio ila serikali inajua fika report ya IMF itaathiri vipi uwekezaji maana hakuna muwekezaji kichaa atategemea kuwekeza Tanzania kwa kutumia data za serikali tu yaani ni lazma wachukue na data za mashirika ya nje..

Hao wawekezaji na wahisani wasiisahau report ya CAG.
 
Hebu waende kwa wachina wakachukue hizo taarifa then wapike waje na za kwao. We are tired of being scapegoat ktk kuwafurahisha mabwanyeye, yaani wanatutoa kafara kupitia hizo habari zao za kupika then wanatuachia tuingie mwituni kama mbuzi wa kafara huko wao wameshajiosha dhambi kama vile wayahudi walipo waachia mbuzi kuingia mwituni wakiamini dhambi zao zimeenda.


Kwahiyo walipotoa ripoti inayoonyesha Tanzania inafanya vizuri 2016, hatukuwa scapegoat? Ninapowashangaa watanzania wenzangu ni tabia ya kutaka kuambiwa tu yale tunayopenda kusikia ila tukiambiwa ukweli mchungu tunaanza kurusha vijembe na kejeli. Tunapenda kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa tu. Let's grow up please!

Hatuwezi kusonga mbele kwa kuficha kichwa mchangani kama mbuni, ukweli hautabadilika kamwe! Tuanze kwa kujitathmini tumefikaje hapa sio kurusha madongo.
 
Back
Top Bottom