Taarifa ya Ikulu dhidi ya gazeti la Tanzania daima..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya Ikulu dhidi ya gazeti la Tanzania daima.....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PapoKwaPapo, Jan 27, 2012.

 1. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Gazeti laTanzania Daima la jana, Jumatano, Januari 25, 2012, kwenye ukurasa wake wakwanza limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Ndege ya JK utata:Iko nje kwa miezi miwili. Serikali yakwama kuilipia.”

  Miongoni mwa yaliyoandikwa kwenye habari hiyo ni pamoja na “Ukata unaiokabili Serikali umesababisha kukwama kuilipia ndege hiyo maalum ya Rais…Ndege ya Rais mahususi kwa ajili ya safari za namna hiyo imezuiliwa nje baada ya Serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo yake…Kutokuwepo kwa ndege hiyo, kumesababisha Rais Kikwete na ujumbe wake wa watu 14, ulioondoka nchini jana kwenda Davous, nchini Sweden kuhudhuria mkutano wa dunia wa uchumi, kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Qatal”.

  Limeendelea Gazeti hili la Tanzania Daima kudai kuwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa ndege hiyo ya Rais gharama za safari hiyo ya Rais zimeongezeka na ziara hiyo ya Raisya siku nne kuhudhuria mkutano huo itagharimu kiasi cha shilingi milioni 300.Aidha,Gazeti hili linadai kuwa mkutano huo hauna tija kwa taifa, kwamba Rais Kikweteamehudhuria mikutano hiyo mara nyingi lakini hakuna faida iliyopatikana kwataifa.

  Kwa hakika,maandishi na kauli hizi za ovyo na zisizokuwa za kweli za Gazeti la TanzaniaDaima zinalenga kuupotosha umma wa Tanzania bila sababu za msingi na hivyokuusababishia umma chuki isiyokuwa na msingi kwa Rais. Katika kuuelezea ummaukweli wa safari hiyo ya Mheshimiwa Rais Kikwete tunapenda kutoka ufafanuziufuatao:

  Kwanza, kama tulivyoeleza, kwa usahihi, katika taarifa yetu kwa vyombo vya habari janajioni, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekwenda katika mji/kijiji chaDavos, nchini Uswisi kuhudhuria Mkutano wa World Economic Forum (WEF) unaoanzaleo. Rais Kikwete hakuwenda katika mji wa Davous, nchini Sweden kamalinavyosema Gazeti hili. Aidha, Rais Kikwete na ujumbe wake umesafiri kwa ndegeya Shirika la Ndege la Qatar na siyo Qatal kama linavyoripoti Tanzania Daima.

  Pili,Serikali haijakwama, kwa sababu zozote zile, kulipia matengenezo ya kawaida (routinemaintenance) ya Ndege ya Rais. Hili limefafanuliwa vizuri na ipasavyo naMtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Rubani Kennan Paul Mhaiki jana.Isipokuwa nivyema kuongeza kuwa matengenezo ya ndege hiyo yalimalizika juzi tu, Jumatatu,Januari 23, mwaka huu, wakati ndege hiyo ilipofanyiwa safari ya majaribio (testflight) kule Savannah, Georgia, Marekani na wala siyo miezi miwili iliyopitakama linavyodai Tanzania Daima. Hivyo, madai kuwa ndege hiyo imezuiliwa nje kwamiezi miwili sasa kwa sababu ya Serikali kushindwa kulipia gharama zamatengenezo ni porojo tu zisizokuwa na msingi.

  Tatu, nivigumu kujua Gazeti la Tanzania Daima limepata wapi habari kuwa safari hiyo yasiku nne inagharimu kiasi cha sh. milioni 300. Ukweli ni safari ya MheshimiwaRais Kikwete na ujumbe wake ni ya siku nane, kama tulivyoeleza jana, ambakoatahudhuria mikutano ya WEF na ule wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU)mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili Jumamosi, Januari 28, 2021.

  Hivyo, sikweli kwa Gazeti hili kudai kuwa nauli tu na matumizi ya safari ya MheshimiwaRais ni shilingi milioni 300 kwa siku nne tu.Nne, TanzaniaDaima linadai kuwa safari za Mheshimiwa Rais mjini Davos hazina tija na walafaida yoyote. Huu pia ni uongo mwingine wa dhahiri wa Gazeti hili.

  Tunapendakukumbusha faida chache tu zilizotokana moja kwa moja na Mheshimiwa RaisKikwete kushiriki mikutano ya WEF kama ifuatavyo:(a)Moja, ni kubuniwa na kupitishwa kwa Mpango Kabambe wa Uendelezaji Kilimokatika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania wa Southern Agricultural Growth Corridorof Tanzania (SAGCOT) uliozinduliwa wakati wa WEF mwaka jana.

  Mpango huuutakaotekelezwa kwa pamoja na sekta binafsi na sekta za umma kwa kushirikishaSerikali ya Tanzania, Mashirika ya Kimataifa, Makampuni ya Kimataifa unalengakuleta faida zifuatazo:
  (i) Uwekezaji wa kiasi cha dola za Marekanibilioni 3.4 katika kilimo cha Tanzania na kuongeza uzalishaji wa kilimo hichomara tatu katika miaka 20 ijayo.
  (ii)Kuchochea uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara kwenye eneoya hekta 350,000.
  (iii)Kutengeneza kiasi cha ajira 420,000 za kudumu.
  (iv)Kuwatoa kwa namna ya kudumu kiasi cha watu milioni mbili katikaumasikini.
  (v)Kuleta usalama wa kudumu wa chakula kwa kuhakikisha kinapatikana chakulacha kutosha kwa Tanzania na nchi za jirani.
  (vi)Kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, barabara, reli, nishati na bandarikatika eneo lote la Mradi wa SAGCOT.(vii) Kuwahakikishia wakulima masoko ya mazao yao,kuwawezesha kupata dhana za kisasa, na kuwaanzishia mifumo ya kisasa yaumwagiliaji.
  (viii)Kuingizia wakulima mapato ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.2 kilamwaka. (Kiasi cha dola za Marekani milioni 50 zinaendeleakuingizwa katika mfuko wa uanzishwaji wa Mpango wa SAGCOT utakaotelekezwa kwakuanzia katika maeneo ya Sumbawanga (Rukwa), Ihemi na Ludewa (Iringa),Kilombero (Morogoro), Mbarali (Mbeya), na Rufiji (Pwani)(b)

  Pili, ni uwekezaji kabambe wa kiasi cha dolaza Marekani milioni 20 katika mfumo wa upakuaji wa mbolea kwenye Bandari ya Dares Salaam unaofanywa na Kampuni ya Yara International, moja ya makampunimakubwa zaida ya uzalishaji wa Kampuni ya Yara International, moja yamakampuni makubwa zaida ya uzalishaji wa mbolea duniani.
  Yara International ni mmoja wa washirika wakubwakatika SAGCOT na uwekezaji wake unalenga kuhakikisha kuwa Tanzania na hatamajirani wanapata mbolea ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha kilimo.

  (c)Tatu, mikutano ya WEF ni shughuli moja inayomwezesha Kiongozi wa Nchikukutana na kufanya mazungumzo na wakubwa wote duniani – wawe wa siasa, wabiashara, wa uchumi, wa uwekezaji, wa kijamii – katika jitihada zake zakuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha uwekezaji.

  Katika sikutatu zijazo, kwa mfano, Mheshimiwa Kikwete miongoni mwa watu wengine atakutanana Bwana Bill Gates wa Bill&Bellinda Foundation, Naibu Waziri wa Uchumi,Nishati na Kilimo wa Marekani Bwana Robert Hormats, Rais wa Benki ya DuniaBwana Bob Zoellick, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Australia Bwana Kevin Ruud, Mkuuwa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani Bwana Raj Shah, MtendajiMkuu wa Benki ya ABSA Bi. Maria Ramos, na Waziri Mkuu wa Thailand Bi. YingluckShinawatra.

  Tunapendakumalizia kwa kusisitiza, kwa mara nyingine tena, kuwa ni vyema Gazeti laTanzania Daima lijiridhishe na usahihi na habari zake kabla ya kuzichapishakama inavyoelekeza misingi mikuu ya uandishi wa habari na weledi wa kazi hiyo.Uandishi wa habari za uongo unaleta hofu na kuanzisha uzushi usiokuwa na sababuzozote miongoni mwa wananchi na hiyo siyo kazi ya uandishi wa habari.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasilianoya Rais,
  Ikulu, DAR ES SALAAM.
  25 Januari, 2012
   
 2. Titans

  Titans JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 868
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 180
  mmh..hivi wamesema sasa hiyo safari itagharimu kiasi gani??ama ni kiasi kikubwa sana zaidi ya gazeti ilichotaja??
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Kama wameona kuna makosa na hakuna ukweli kwa nini wasilifungie gazeti au wawapeleke mahakamani ? Hizi porojo za akina Salva za hovyo .Kukosea Swiss na kuandika Sweden ni typo mbona ikulu imekuwa inatoa maandiko yamejaa makosa kibao na hovyo kwa hovyo why wanashangaa mtu kusema Sweden leo ?

  CCM bwana .
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,505
  Likes Received: 2,745
  Trophy Points: 280
  Mbona hawasemi ni kiasi gani kama siyo millioni 300??? Sijui wanaogopa nini wakati akina Sumaye na Mwinyi walisharipotiwa kuwahi kutumia zaidi ya hizo (500 million) about 10 years ago. So what is 300 million now??? Afadhari wangekaa kimya!!

  Huo mkakati wa kuinua kilimo mara tatu na kucreate ajira 450,000 in 20 years na mashaka nao!!!That could be done in 5 years with serious government. Tuliona Malawi walivyoweza ndani ya miaka 5 ya kwanza ya Bingu kabla madudu ya Kiafrika hayajamwingia akilini kama kawaida ya viongozi wetu!!
   
 5. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Well said Ikulu kwa ufafanuzi mzuri na uliojitosheleza. Hili gazeti la Tanzania Daima limeisha kosa mwelekeo na hii inatokana na hasira za Mhariri wao kupelekwa mahakamani. Mie huwa silisomi tena hili gazeti kwani limejaa ushabiki wa kisiasa kuliko weledi wa uandishi. Additionally, ni gazeti la mbowe, unategemea litakuwa fair kwenye uandishi?. Tanzania Daima tumewachoka na habari zenu za uzushi na uzandiki

 6. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  THUBUTU! Wanajua ni kweli tupu! Kusahihisha kiswahili/lugha katika hoja nzito kama hiiinaonyesha jinsi mwandishi huyu alipania kubishia tu! Lakini tangu lini ikawa na jukumu la kupambana na yanayoandikwa kwenye magazeti? Ikulu of all places ianze kubishana na kila gazeti, makubwa.

  Swali kuu kwa msemaji wa Ikulu: Je hio miradi inayodaiwa kutokana na ziara za Raisi isingepatikana kama Raisi asingekwenda huko? Je ni lazima aende yeye mwenyewe, kwa nafsi ya JK?

  Je, ni sahihi kweli kuacha madaktari/nchi kwenye giza kuu katika haya ya afya na kusafiri? Mbona angeweza kuwakilishwa na Makamu. Tena nasikia ule mkutano hauhusu Nchi zote bali ni nchi za Ulaya!

  Maskini Raisi wangu, hana washauri makini!
   
 7. melxkb

  melxkb JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye nyekundu ni mpango utakaotelekezwa.........?? Basi si huo mpango wauache tu!!!, nilifikiri wao kwa kuwa ni waandishi wa ikulu hawakosei spellings.  [​IMG] By PapoKwaPapo [​IMG]
  Gazeti laTanzania Daima la jana, Jumatano, Januari 25, 2012, kwenye ukurasa wake wakwanza limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Ndege ya JK utata:Iko nje kwa miezi miwili. Serikali yakwama kuilipia.”

  Miongoni mwa yaliyoandikwa kwenye habari hiyo ni pamoja na “Ukata unaiokabili Serikali umesababisha kukwama kuilipia ndege hiyo maalum ya Rais…Ndege ya Rais mahususi kwa ajili ya safari za namna hiyo imezuiliwa nje baada ya Serikali kukwama kulipia gharama za matengenezo yake…Kutokuwepo kwa ndege hiyo, kumesababisha Rais Kikwete na ujumbe wake wa watu 14, ulioondoka nchini jana kwenda Davous, nchini Sweden kuhudhuria mkutano wa dunia wa uchumi, kuondoka na ndege ya Shirika la Ndege la Qatal”.

  Limeendelea Gazeti hili la Tanzania Daima kudai kuwa kwa sababu ya kutokuwepo kwa ndege hiyo ya Rais gharama za safari hiyo ya Rais zimeongezeka na ziara hiyo ya Raisya siku nne kuhudhuria mkutano huo itagharimu kiasi cha shilingi milioni 300.Aidha,Gazeti hili linadai kuwa mkutano huo hauna tija kwa taifa, kwamba Rais Kikweteamehudhuria mikutano hiyo mara nyingi lakini hakuna faida iliyopatikana kwataifa.

  Kwa hakika,maandishi na kauli hizi za ovyo na zisizokuwa za kweli za Gazeti la TanzaniaDaima zinalenga kuupotosha umma wa Tanzania bila sababu za msingi na hivyokuusababishia umma chuki isiyokuwa na msingi kwa Rais. Katika kuuelezea ummaukweli wa safari hiyo ya Mheshimiwa Rais Kikwete tunapenda kutoka ufafanuziufuatao:

  Kwanza, kama tulivyoeleza, kwa usahihi, katika taarifa yetu kwa vyombo vya habari janajioni, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekwenda katika mji/kijiji chaDavos, nchini Uswisi kuhudhuria Mkutano wa World Economic Forum (WEF) unaoanzaleo. Rais Kikwete hakuwenda katika mji wa Davous, nchini Sweden kamalinavyosema Gazeti hili. Aidha, Rais Kikwete na ujumbe wake umesafiri kwa ndegeya Shirika la Ndege la Qatar na siyo Qatal kama linavyoripoti Tanzania Daima.

  Pili,Serikali haijakwama, kwa sababu zozote zile, kulipia matengenezo ya kawaida (routinemaintenance) ya Ndege ya Rais. Hili limefafanuliwa vizuri na ipasavyo naMtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali, Rubani Kennan Paul Mhaiki jana.Isipokuwa nivyema kuongeza kuwa matengenezo ya ndege hiyo yalimalizika juzi tu, Jumatatu,Januari 23, mwaka huu, wakati ndege hiyo ilipofanyiwa safari ya majaribio (testflight) kule Savannah, Georgia, Marekani na wala siyo miezi miwili iliyopitakama linavyodai Tanzania Daima. Hivyo, madai kuwa ndege hiyo imezuiliwa nje kwamiezi miwili sasa kwa sababu ya Serikali kushindwa kulipia gharama zamatengenezo ni porojo tu zisizokuwa na msingi.

  Tatu, nivigumu kujua Gazeti la Tanzania Daima limepata wapi habari kuwa safari hiyo yasiku nne inagharimu kiasi cha sh. milioni 300. Ukweli ni safari ya MheshimiwaRais Kikwete na ujumbe wake ni ya siku nane, kama tulivyoeleza jana, ambakoatahudhuria mikutano ya WEF na ule wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Afrika (AU)mjini Addis Ababa, Ethiopia atakapowasili Jumamosi, Januari 28, 2021.

  Hivyo, sikweli kwa Gazeti hili kudai kuwa nauli tu na matumizi ya safari ya MheshimiwaRais ni shilingi milioni 300 kwa siku nne tu.Nne, TanzaniaDaima linadai kuwa safari za Mheshimiwa Rais mjini Davos hazina tija na walafaida yoyote. Huu pia ni uongo mwingine wa dhahiri wa Gazeti hili.

  Tunapendakukumbusha faida chache tu zilizotokana moja kwa moja na Mheshimiwa RaisKikwete kushiriki mikutano ya WEF kama ifuatavyo:(a)Moja, ni kubuniwa na kupitishwa kwa Mpango Kabambe wa Uendelezaji Kilimokatika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania wa Southern Agricultural Growth Corridorof Tanzania (SAGCOT) uliozinduliwa wakati wa WEF mwaka jana.

  Mpango huuutakaotekelezwa kwa pamoja na sekta binafsi na sekta za umma kwa kushirikishaSerikali ya Tanzania, Mashirika ya Kimataifa, Makampuni ya Kimataifa unalengakuleta faida zifuatazo:
  (i) Uwekezaji wa kiasi cha dola za Marekanibilioni 3.4 katika kilimo cha Tanzania na kuongeza uzalishaji wa kilimo hichomara tatu katika miaka 20 ijayo.
  (ii)Kuchochea uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara kwenye eneoya hekta 350,000.
  (iii)Kutengeneza kiasi cha ajira 420,000 za kudumu.
  (iv)Kuwatoa kwa namna ya kudumu kiasi cha watu milioni mbili katikaumasikini.
  (v)Kuleta usalama wa kudumu wa chakula kwa kuhakikisha kinapatikana chakulacha kutosha kwa Tanzania na nchi za jirani.
  (vi)Kuboresha miundombinu ya umwagiliaji, barabara, reli, nishati na bandarikatika eneo lote la Mradi wa SAGCOT.(vii) Kuwahakikishia wakulima masoko ya mazao yao,kuwawezesha kupata dhana za kisasa, na kuwaanzishia mifumo ya kisasa yaumwagiliaji.
  (viii)Kuingizia wakulima mapato ya kiasi cha dola za Marekani bilioni 1.2 kilamwaka. (Kiasi cha dola za Marekani milioni 50 zinaendeleakuingizwa katika mfuko wa uanzishwaji wa Mpango wa SAGCOT utakaotelekezwa kwakuanzia katika maeneo ya Sumbawanga (Rukwa), Ihemi na Ludewa (Iringa),Kilombero (Morogoro), Mbarali (Mbeya), na Rufiji (Pwani)(b)

  Pili, ni uwekezaji kabambe wa kiasi cha dolaza Marekani milioni 20 katika mfumo wa upakuaji wa mbolea kwenye Bandari ya Dares Salaam unaofanywa na Kampuni ya Yara International, moja ya makampunimakubwa zaida ya uzalishaji wa Kampuni ya Yara International, moja yamakampuni makubwa zaida ya uzalishaji wa mbolea duniani.
  Yara International ni mmoja wa washirika wakubwakatika SAGCOT na uwekezaji wake unalenga kuhakikisha kuwa Tanzania na hatamajirani wanapata mbolea ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha kilimo.

  (c)Tatu, mikutano ya WEF ni shughuli moja inayomwezesha Kiongozi wa Nchikukutana na kufanya mazungumzo na wakubwa wote duniani – wawe wa siasa, wabiashara, wa uchumi, wa uwekezaji, wa kijamii – katika jitihada zake zakuitangaza Tanzania kama kituo muhimu cha uwekezaji.

  Katika sikutatu zijazo, kwa mfano, Mheshimiwa Kikwete miongoni mwa watu wengine atakutanana Bwana Bill Gates wa Bill&Bellinda Foundation, Naibu Waziri wa Uchumi,Nishati na Kilimo wa Marekani Bwana Robert Hormats, Rais wa Benki ya DuniaBwana Bob Zoellick, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Australia Bwana Kevin Ruud, Mkuuwa Shirika la Misaada ya Maendeleo la Marekani Bwana Raj Shah, MtendajiMkuu wa Benki ya ABSA Bi. Maria Ramos, na Waziri Mkuu wa Thailand Bi. YingluckShinawatra.

  Tunapendakumalizia kwa kusisitiza, kwa mara nyingine tena, kuwa ni vyema Gazeti laTanzania Daima lijiridhishe na usahihi na habari zake kabla ya kuzichapishakama inavyoelekeza misingi mikuu ya uandishi wa habari na weledi wa kazi hiyo.Uandishi wa habari za uongo unaleta hofu na kuanzisha uzushi usiokuwa na sababuzozote miongoni mwa wananchi na hiyo siyo kazi ya uandishi wa habari.

  Imetolewa na:
  Kurugenzi ya Mawasilianoya Rais,
  Ikulu, DAR ES SALAAM.
  25 Januari, 2012
   
 8. Ishaka

  Ishaka Member

  #8
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 1, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Yetu macho, tutashuhudia mengi! Mungu atusaidie watanzania.
   
 9. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kauli za Ikulu zinazua maswali zaidi ya ya majibu badala ya kujibu hoja wanakimbilia vitu rahisi ambavya havibadili ukweli na kutupa picha halisi ya upande wa pili wa shilingi.
  Shirika la Ndege la Qatal au Qatar linabadili nini katika safari ya Rais?katika mji/kijiji cha Davos, wa Davous, nchini Sweden kina badili nini?Hapa gazeti lilikua na lengo la konyesha matumizi ya fedha yanayotumika wakati serikali imetumia pesa nyingi kunua ndege hiyo wakati haitumiki ipashwavyo.Taarifa ya Ikulu isingekimbilia kufafanua typing error badala yake ingejibu hoja.Kiasi gani cha pesa kimetumika kwa ziara hiyo,kiasi gani kimetumika kwa matengenezo ya ndege hiyo,lini ilikwenda na lini itarudi lini na imgharimu kiasi gani?Haya ndio majibu tulikua tunayahita na sio porojo.Nini anafanya Davos tunafuatili kupitia vyambo vya habari mbalimbali.Tulitegemea Ikulu kutoa kauli kuhusu hali ya mgomo wa madaktari ambapo walalahoi wanateseka na kupoteza maisha.

 10. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  There is an ample evidence to discharge Tanzania Daima's owner with incitement and subsequently ban the paper from business. We can't continue with this kind of journalism where everyone publishes what goes through their mind without logical evaluation of what the outcome might be. The liberty of expression is the primary human right but Editors should know better where exactly to draw the line.
   
 11. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Bigup Tz daima kwa ku2pa ukweli even if magamba wa ikulu wanajaribu kupotosha, ukweli ni kwamba hii ni serikali legelege.
   
 12. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hii mbona tulisha ijadili sana
   
 13. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  in connection na hapo pekundu, Inamaana ikulu wamegeuka editors wa magazetyi????????????????????????????????
   
 14. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  And where exactly to draw the line madam/ Mr. editor of editors?
   
Loading...