AZAM TV mnaamanisha nini kutulazimisha kuangalia taarifa ya habari via Azam App?

Mulangila Mukuru

JF-Expert Member
Feb 24, 2010
1,945
724
Siku za hivi karibuni Azam Tv wamekuwa hawarushi taarifa ya habari ya saa mbili usiku kwa kisingizio kuwa ni sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Lakini baadae wameanza kutwambia wateja wao tuingalie Azam news via Azam app kwa wenye smart phone.

Jambo hili binafsi linanichanganya, inawezekanaje mrushe taarifa ya habari kupitia App za simu lakini kwenye TV haionekani?

Semeni ukweli kama kuna jambo mnalitafuta na si matatizo ya kiufundi.
 
Huko kwenye App ndiyo kuna channel yenye kuonesha taarifa ya habari au vp maana mie hili jambo sijalielewa?
 
Biashara ya kweli imekuwa balaa! Sasa hivi ukitaka kuona habari ya azam SAA mbili inabidi ulipie kinga'mzichako na bado utoe hela ya ziada kwenye app yao!

Hivi hawaoni uchumi wa watu sasa hivi? Hivi tcra wapo wapi?

Jamani azam TV wamepatwa na nini?
 
Taarifa ya habari Azam Two imeota mbawa, siku ya nne sasa.

Maelezo ni ...kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu.... Je, kuna mgomo? Mmefungiwa? Mitambo imekorofisha?

Tuwekeeni wazi basi wapenzi wenu. Hii ya kusema ... Ni sababu zilizo nje ya uwezo wetu..... Ni melezo yenye kuacha tashwishwi kubwa. Ni nini shida?
 
Huko kwenye App ndiyo kuna channel yenye kuonesha taarifa ya habari au vp maana mie hili jambo sijalielewa?
Kwenye king,amuzi chao matangazo yanaendelea kama kawaida ila ukifika muda wa taarifa ya habari ambayo tulizoea kuitazama kila saa mbili usiku wanaomba radhi kuwa taarifa ya habari haitakuwepo kutokana na sababu zilizo nje ya iwezo wao lakini wanatupa option ya kuingalia kupitia application ya Azam TV kwenye simu.
 
huu ni upuuzi wa kiwango cha standard gauge...hakuna sentensi inaniudhi kama hii "kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu"
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom