Taarifa ya gazeti la MwanaHalisi juu ya Ben Saanane na uhalisia wa mambo

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
Wiki jana nilieleza jinsi CHADEMA ilivyojihusisha na matukio fulani katika taifa hili ili kupata huruma ya kisiasa ndani na nje ya nchi (angalia baada ya andiko hili). Nikaeleza kuwa sakata la kupotea kwa Ben ni mpango ulioratibiwa na CHADEMA ila walikosea mikakati yao. Nikasema, ni aibu kwa Ben na chama na maisha ya kisiasa kutumia mbinu za kupakazia watawala.

Sahizi gazeti la Mwanahalisi limeibuka na taarifa za kuonekana kwa Ben (Utata mpya msaidizi wa Mbowe)na kuanza kumpakazia kama kuwa anatafuta umaarufu wa kisiasa na vyeo kwa mbinu za mkato. Mimi nasema si mbinu za mkato za Ben ila mbinu za makato za CHADEMA ndo zimeingia inzi. Hakika wangefanikiwa serikali ya awamu hii ingepata kashfa kubwa na CHADEMA kuonekana mashujaa wa kuogopwa.

Kwa sasa ni ukweli usiopingika kuwa Ben hatutakuwa naye tena katika nyanja za kisiasa.

Amejiahibisha kutumika na imekuwa aibu kwake ya maisha. Hataonekana tena. Watu wengi walisema ajitokeze mwenyewe na aseme. Hakujitokeza pengine akiaminishwa kuwa chama kinatafuta mbinu mbadala za kumtoa huko alikofichwa. Bahati yake ni kuwa hajauawa!! Na kweli wangemuua kabisa!!!!

Maana kikubwa ni kusafisha taswira ya chama na si mtu. Tunajua mengi yaliyoratibiwa na CHADEMA na mwisho waliooneka mashujaa wa kutekeleza miradi hiyo walitoswa na wamebaki mashati tu mitaani

Vijana tujifunze aina ya siasa tunazozifanya. Tusitumiwe na watu ili tuonekane mashujaa wakati hatujui kesho yetu.

Ben ametoa taarifa halisi ya CHADEMA na haitafutika.

Hizi ni uzi nilizoleta wiki jana.

Jini limetoka katika kibuyu nani wa kulirudisha?

Tumekuwa tukiaminishwa kuwa Serikali imekuwa inahusika na matukio ya utesaji watu, hasa wenye mrengo tofauti na watawala. Ni kitu kilichotumika kwa miaka mingi.
kilitokea kwa Ulimboka, Kibanda, Mawazo, Mlinzi wa Mbowe, Mwenyekiti wa CDM wilaya ya Temeke na wengine.

Kila serikali ilivyiojaribu kueleza mazingira ya matukio, haikuaminika kwa kusema lazima watakuwa wamehusika.

Lakini wajuvi wa mambo waliwahi sema kuwa CHADEMA imekuwa inatumia matatizo ya Watanzania kubomoa taifa na si CCM. Mfano, mpango mingi ya CHADEMA haijakuwa ya kupingana na CCM zaidi ya kupingana na serikali na mipango yake.

Wakati madaktari wamegoma, wenyewe walichukulia kama tukio la watu kuchukia serikali na watawala wake. Walimteka Ulimboka na kumetesa. Mwisho waliandika katika magazeti yenye mrengo wa kipinzani kuelezea walivyonasa mawasiliano ya maofisa wa Ikulu kumteka Ulimboka. Na hii imetumika kwa wote, isipokuwa kifo cha Kamanda Mawazo.

Nikiwa natafakari nikaona kuwa upinzani unaoonyeshwa na CHADEMA ya sasa ni tofauti na miaka ya nyuma. Ni chama kilichokaa kishari zaidi.

Kimekuwa kikundi cha waasi wanaopingana na serikali na si vyama vingine vya siasa. Wanatumia nguvu kubwa kuaminisha watu kuwa Tanzania imeangukia katika utawala wa kiimla na hakuna haki wala watu kusema. wanataka kusema ukisema kitu Tanzania unauawa. wanataka kufananisha serikali hii na yaliyotokea katika Iraq ya Sadam.

Kilichooneka kwa sasa ni kuwa CHEDEMA walikosea steps wakaangukia pua bila kujua malengo yao yatawageukia.

Jini limetoka katika kibuyu nani wa kulirudisha?
Sakata la kupotea kwa kijana mwenzetu Ben 8 linaweza kuwa doa kubwa kwa chama na maisha yeke kama anafanya maigizo

Sakata la kupotea kwa kijana mwenzetu Ben 8 linaweza kuwa doa kubwa kwa chama na maisha yeke kama anafanya maigizo.

Nasema hivi kwa sababu maisha yake yako mikononi mwake na si mwa chama.

Ben ni kijana na kama yuko mahali ajitokezee na aseme. Chama kisitoe matamko kwa kufurahisha jamii ili kuonyesha umma kuwa serikali inateka watu. Kama kimehusika na hili kama wengi wanavyoona, kiseme kabisa kilikosea steps za kunadi hili tukio.

Ajitokeze kokote aliko ili maisha yake yawe ya kuaminika katika jamii.
 
So what? Waambieni Jamaa wamkamate Kubenea au watumie taarifa yake kama input kwenye intelijensia yao Maana walisema wanakaribisha Taarifa kutoka kwa watu.

Ungeuelekeza uzi huu kwa jamaa wa Intelijensia incase hawajaona bado taarifa ya Kubenea.
 
Ben anatafutwa. Taifa la Tanzania linamtafuta. Huyu anasema Ben hajapotea. Ben amejificha.
Kwa nini hili jambo, kuambiwa kwamba Ben amejificha, linaonekana kuwaudhi sana Bramo na Ngonepi?
Tunaabiwa Balali hajakufa. Tunaabiwa Kanumba hajakufa
Michael Jackson tunaambiwa yupo Canada.
Kwa hiyo habati kama tukizipata,lazima zichunguzwe.
 
Back
Top Bottom