Kombo
JF-Expert Member
- Oct 29, 2010
- 1,812
- 509
Mie huu mwaka wa saba sijacheka!!!!
...na hata comment ya jenifa haikukuchekesha? Bas itabidi upelekwe India kwa matibabu zaidi! Ha ha haaa...!!!
Mie huu mwaka wa saba sijacheka!!!!
By eeka mangi
Kwani wao polisi wamefanya kazi na yeye Mwakyembe! Mlango alopitia wao ndo anaopitia! Anza na Manumba na mwema ndo umshambulie Mwakyembe! Kweli kichani hamna akili!
Mkuu unajua uchunguzi wa jinai huwa unafanywa na nani? au unakurupuka! suluhisho kwenye mambo ya hivi huwa ni uhuru wa vyombo vya ulinzi na usalama. Angalia nchi za ng'ambo kidogo. Ikibidi muwe mnatembea jamani.Mwakyembe ni tatizo kubwa zaidi ya hao Polisi anaowatuhumu. Kumbe anayo taarifa ya awali ya ugonjwa wake, kama mwanasheria ameshindwa nini kuitisha uchunguzi binafsi wa jinai kuhusu tatizo lake? Hata sasa baada ya Polisi kuonesha "udhaifu" katika uchunguzi wao, kwanini Mwakyembe asiombe msaada wa wataalamu wa nje waliobobea katika upelelezi wafanye uchunguzi upya? Anaogopa nini?
Siwapendi watu walalamishi, lakini huyu amenikera zaidi na ukiwa makini hata faida ya kuwa msomi haionekani!
...tunakoelekea sasa tutegemee kuiona ripoti ya ugonjwa wake kwenye magazeti, kitu ambacho si kizuri sana!
Mkuu, hapo kwenye nyekundu panahusika. Kama alivyosema Mwakyembe, na sio kwa sababu kasema tu bali ndivyo ilivyo kule watu wanakojua dhamana zao, wajibu wa polisi kama walinzi wa raia na mali zao, ni kutafuta ushahidi na wala sio kusubiri kupelekewa ushahidi. Kama unalikataa hilo, sitotafautisha kuwaza kwako na hili jeshi letu "tukufu".
Mwakyembe kama raia wa nchi, kama ulivyo wewe, mimi na wengineo, tungetegemea kupata ulinzi kutoka kwa polisi ambao Watanzania wote tunawalipa mishahara yao "in exchange of their duties and responsibilities". Mwakyembe kama raia na mwanasheria, pamoja na kuwa na taarifa za awali za ugonjwa wake, hana wajibu wa kuomba msaada wa wataalamu wa nje kufanya uchunguzi, kwani ni dhahiri kuwa hata baada ya yote hayo kukamilika, aende kushitaki wapi katika mfumo huu uliooza?
Tusimwone Mwakyembe tu kuwa ni msomi, tuwaone mamilioni ya Watanzania ambao si wasomi, si manaibu mawaziri, si wabunge, si matajiri...hawa waende wapi? Unataka kusema kuwa ili kutetea na kupata haki yako nchi lazima uwe msomi?
Maswali ni mengi lakini hakuna jawabu? Ikiwa Mkuu unazo, tuwekee hapa ili hata "muathirika wa mabomu ya Mbagala na Gongolamboto, mafuriko, giza la kudumu, mgomo wa madaktari..." waelewe waende wapi wakafanye upelelei ili kupata haki zao.
Je akifa na ukweli huoni itakuwa shida?Wewe bwana umesoma vema hii habari? Mwakyembe bado yupo kwenye uchunguzi na anaendelea na matibabu, uchunguzi ukishakamilika ataongea nini kinamsibu, sio akurupuke tu kama walivyokurupuka hao polisi, na sijui wanam cover nani hapo. MWakyembe alishasema akitoka India mara ya pili atazungumzia kinacho msibu.
haya mambo ya kufanya kazi na vyombo vya habari...................... sasa mwakyembe hapa anatafuta nini?................... huruma ya umma?.................... atulie tu aendelee na matibabu yake, ..................Mungu akipenda atamnusuru...............