Taarifa ya Dr. Mwakyembe kutokana na taarifa ya Jeshi la Polisi juu ya afya yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya Dr. Mwakyembe kutokana na taarifa ya Jeshi la Polisi juu ya afya yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paul Makonda, Feb 18, 2012.

 1. P

  Paul Makonda Verified User

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 97
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  [FONT=&amp] Dk. Harrison G. Mwakyembe (Mb), NW-UJ[/FONT]

  Dar es Salaam
  18/02/12

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


  Nimelazimika leo Jumamosi, tarehe 18 Februari, 2012 kutoa taarifa hii kwa vyombo vya habari kufuatia mkutano wa DCI Robert Manumba na waandishi wa habari jana (17/02/12) kuongelea, pamoja na mambo mengine, hali yangu ya afya na kuhitimisha, kienyejienyeji tu kuwa "sikunyweshwa sumu" ila naumwa tu ugonjwa wa ngozi bila kufafanua ugonjwa huo wa ngozi umesababishwa na nini!

  Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa "sikunyweshwa sumu" wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu;

  na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.

  Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa.

  (Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu.

  Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika). Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:

  (i) Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya "wapelelezi" ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa!

  (ii) Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo "kuanza kazi", Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza.

  (iii) Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari "wale wale" niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!

  (iv) ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya "siri" kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa magazetini ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.

  Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe. Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi?

  Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yangu au walisoma taarifa "nyingine", na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au "walisomewa"! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukidhibiti/ kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi na bila aibu: "hakulishwa sumu", "hakulishwa sumu"!

  Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung'unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.

  Tuendelee kuombeana afya na uhai ili kutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

  Mungu Ibariki Tanzania.
   
 2. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  oooooh serikali ya JK mweee kila kitu hatukielewi!
  posho imepanda mwingine anapinga
  nimenyweshwa sumu polisi wanapinga
  Hii nchi ipoipo tuu kama gari inayoendeshwa na mlevi!
   
 3. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,541
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Alikuwa wapi siku zote amekaa kimya ?
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Alikuwa India anatibiwa si unajua anaumwa!
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  haya mambo ya kufanya kazi na vyombo vya habari...................... sasa mwakyembe hapa anatafuta nini?................... huruma ya umma?.................... atulie tu aendelee na matibabu yake, ..................Mungu akipenda atamnusuru...............
   
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Usalama wa taifa la tanzania mimi nashindwa kuelewa kama ni usalama wa taifa ama usalama wa genge la mafya ya ufisadi. DCI anatoa taarifa ya Ugonjwa wa mtu kama vile imeandaliwa na mtoto wa darasa la tano tena wa shule za kata. Hebu watanzania tuache mizaha. Haitatufikisha popote.
  .
   
 7. satellite

  satellite JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  teDah!hii nchi kweli ni mafia hivi haya yanatokea kwa mbunge na naibu waziri tena msomi ss sie wananchi kajamba nani itakuaje?si ndo tunauliwa then ushahidi unapotezwa kabisa,mi ni mpenzi mkubwa sana wa kuangalia series za kijasusi nilidhani ni fiction yale matukio ya viongozi wanayafanya na kuficha ukweli kwa gharama yeyote ile na ukiingilia mambo yao wanakushughulikia balaa.hizi nguvu za umafia wanazipata wapi?pole sana kamanda wa kyela hayaa mambo yana mwisho wake
   
 8. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mungu hatalala atakulinda na kukuvusha kwenye majaribu.
   
 9. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Du hii Kali ... Nchi hii si salama tena...
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Feb 18, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mnamuua mtu hamsemi ukweli mnataka atulie duuu hiii nchi raisi sana kuiongoza aiseee!
   
 11. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kwani wao polisi wamefanya kazi na yeye Mwakyembe! Mlango alopitia wao ndo anaopitia! Anza na Manumba na mwema ndo umshambulie Mwakyembe! Kweli kichani hamna akili!
   
 12. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #12
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe ni tatizo kubwa zaidi ya hao Polisi anaowatuhumu. Kumbe anayo taarifa ya awali ya ugonjwa wake, kama mwanasheria ameshindwa nini kuitisha uchunguzi binafsi wa jinai kuhusu tatizo lake? Hata sasa baada ya Polisi kuonesha "udhaifu" katika uchunguzi wao, kwanini Mwakyembe asiombe msaada wa wataalamu wa nje waliobobea katika upelelezi wafanye uchunguzi upya? Anaogopa nini?


  Siwapendi watu walalamishi, lakini huyu amenikera zaidi na ukiwa makini hata faida ya kuwa msomi haionekani!

  ...tunakoelekea sasa tutegemee kuiona ripoti ya ugonjwa wake kwenye magazeti, kitu ambacho si kizuri sana!
   
 13. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #13
  Feb 18, 2012
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Mhhhh! Sinema inaanza au inakwisha?
   
 14. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #14
  Feb 18, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Pole sana Dr Mwakyembe, siku zote haki itatawala na dhuluma itasinyaa kwa aibu. Tumwombe Mungu akuimarishe kiafya.
   
 15. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #15
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mtu yeyote mwenye busara hakurupuki tu. Hufikiri sana na kwa kina kabla ya kuonge lolote. Hakuna jibu sahihi la swali lako ama la kamuulize mwakyembe. We jadili anayoyasema na si vinginevyo otherwise utakuw ni walewale wa kutumwa
   
 16. N

  Nipe tano Senior Member

  #16
  Feb 18, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa polisi hawapo makini na wanamasihala sana. Pole sana Dr. Mungu atakupigania na ipo siku watakusaluti
   
 17. C

  Colman Member

  #17
  Feb 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naona hili jeshi la polisi limekosa uelekeo, kwa kutetea haki za mafisadi wachache
   
 18. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #18
  Feb 18, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Haya mambo, mbona yanachanganya?
   
 19. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #19
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wamemwaga ugali nawe unamwaga mboga.
  Kumbe Manumba ni classmate wako anakuchinjia baharini ili hali Mwema ulimfundisha.
  Ama kweli zimwi likujualo halikuli ..............................
   
 20. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #20
  Feb 18, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  wenzake wamemwaga ugali yeye kamwaga mboga. ila mboga yenyewe mbona mifupa mitupu?
   
Loading...