Mfalme wa Genge
Senior Member
- Mar 30, 2018
- 190
- 224
Taarifa ya CAG imesema hakuna upotevu wa Trilioni 1.5 kama inavyodaiwa na watu wachache wenye nia ya kupotosha na hata Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa ufafanuzi kuwa hakuna tofauti ya makusanyo na mapato ya Serikali katika Mfuko Mkuu kwa mwaka wa 2016/2017 isipokuwa mkanganyiko uliotokana na baadhi ya taratibu ambazo hazikuwekwa vizuri na watu wa fedha.
Ripoti hii imekuwa pigo kwa CHADEMA kwa kuwa walijipanga kusambaza waraka katika balozi mbalimbali zilizopo nchini kuishutumu Serikali kwa ubadhirifu wa fedha.
Wapinzani hawa chini ya kiongozi wao Zitto Kabwe wameandaa waraka unaoonyesha upotevu wa Trilioni 1.5 na wanapanga kuutumia kuwashawishi Nchi HISANI kupitia balozi zao zilizopo hapa nchini kwamba pesa walizoipatia Serikali kwa ajili ya maendeleo zimetumiwa kufanya mambo mengine ikiwemo kuwanunua wapinzani hivyo Tanzania isipewe misaada.
Waraka huo tayari umeshaletwa Jijini Dar na Katibu Mkuu wa BAWACHA, GRACE TENDEGA na kukabidhiwa kwa Katibu wa Mambo ya Nje CHADEMA Ndugu JOHN MREMA ili aanze kuusambaza rasmi katika balozi hizo.
Hii inaendelea kuonyesha kuwa baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakishirikiana na ZITTO KABWE hawaitakii mema nchi yetu kwa kuwa wamekuwa wakihangaika na Mataifa ya nje usiku na mchana kuihujumu nchi wakifikiri wanamkomoa MAGUFULI kumbe wanatukomoa watanzania kwa ujumla wetu.
Tabia hii ya viongozi wa CHADEMA kwa kushirikiana na Zitto Kabwe kudhani kuwa watanzania ni wajinga ifikie mwisho sasa. Watanzania wa leo wameamka na wapo pamoja na Rais MAGUFULI na ndiyo maana hata baadhi ya wafuasi wa CHADEMA wameamua na kusema hapana sasa inatosha kwa upuuzi huu na mbinu za kijinga zenye kila aina ya hila zinazoendelea kufanywa na kundi hilo.
Shime watanzania bila kujali tofauti za itikadi zetu na kwa namna yoyote ile tusimame kwa umoja wetu kupinga hili kwani Rais wetu ana mipango mizuri kwa maendeleo ya watanzania wote na Taifa kwa ujumla wake.
VIVA MAGUFULI, VIVA TANZANIA
Na Steven Joseph