Taarifa ya BBC ikizungumzia maendeleo ya ujenzi wa reli (SGR)

wakati mwingine huwa napata mashaka sana na akili yako mkuu. sijui huwa unataka sie tujue na kufahamu nini? katika nchi ambayo vifo vya mama na mtoto vinaongezeka kila siku unasemaje kuna maendeleo? katika nchi ambayo mtu akiingiza pesa za kigeni anahelelezwa sawa na yule anayeingiza madawa ya kulevya unasemaje kuna maendleo? katika nchi ambayo serikali inakandamiza wakulima wao kama wale wa korosho unasemaje kuna maendleo? kwenye nchi ambayo hata kubadilishana mawazo tu ni kosa wewe unaitaje kuna maendleo? leo hata ukiwa bar unaogopa kuzungumza kwa hofu ya kupotea unaitaje pana maendleo!?
maji hakuna, elimu duni, wanaofaulu hawaendi vyuo vikuu nk
acha kutuviza akili zetu kama ulivyoviza ya kwako na kubali kujingishwa hata kusifia yasiyokuwepo.
serikali yyte makini hujali maendleo ya watu wake sio vitu
 
Nyie watu akili zenu sijui zikoje! Kila siku ni kuwaita wenzenu ni vibaraka wa wazungu ila habari ikitangazwa na vyombo vya hao hao wazungu mbio mbio kuja kuileta JF. Nyie watu vipi?
 
tumenunua sawa ma drimulaina swala lililobaki ni namna ya uendeshaji management ujanja wa ku compete na tulio wakuta ktk biashara n.k

vinginevyo mtabaki na maendeleo ya vitu visivyoweza kufukia madeni mliyo nayo visivyoweza kuinua pato la mtu mmoja mmoja
visivyo weza rudisha heshima ya shilingi yetu dhidi ya dola visivyomfaidisha muuza nyanya au maziwa kwenye baiskeli kule geita na chato yake
Watanzania kwa maneno na kukatishana tamaa !! Likipita hili linazushwa jingine. Mlianza na "Ahadi hewa hizi, hilo haliwezekani" Kuona hela zimelipwa, "Ndege zenyewe mtumba.." tukawekewa na mi serial number hapa!! watalaam wa mtandaoni wakatafsiri minamba hiyo kuchwa kutwa. Imebuma wameanza "Gharama za kwenye lami na angani..." limebuma kwa kushikwa pabaya na mi figure yenu, limezuka jingine "kumbe hata ruti za masafa hawana ni safari za ndani..." mmeumbuka safari za ndani ni mazoezi kwa marubani kabla ya kuanza safari za nje mnakuja na hili sasa!!! "uwezo wa kushindana na wenzetu...!!" Siku zinaenda tutafika tu.
 
Tunapiga kelele sana kwa mafanikio kidogo. Tusipende kuridhika na vitu vidogo.

Tujifunze kwa Wakenya. Wananunua ndege kwa idadi kubwa bila kelele. Wanajenga viwanda vikubwa na vingi maradufu ya Tanzania lakini hawapigi kelele. Wamejenga flyovers zisizo na hesabu lakini hawapigi kelele.

Kushangilia na kujisifu sana kwa mafanikio madogo husababisha kuridhika kwa madogo, na huwezi kutafuta makubwa maana unaamini uliyoyafanya ni makubwa sana.
 
wapinzani wanataka kutuaminisha kuwa maendeleo ni kitendo cha serikali kugawa fedha kama njugu kwa wananchi wake; hayo ndiyo maendeleo ya mtu mmoja mmoja kwa tafsiri Yao.

Ila wanasahau kwamba; miundombinu imara ni kichocheo cha maendeleo na pia ni kipimo cha ustaarabu kwa jamii yoyote
 
povu jingiiii baavichaa bana mna kazi kwa kweli awamu hii mtapinga na kupiga domo sana tu....hao BBC wakiikosoa serikali mnakuja huku mbio mbio mkijisifia eti wenye akili wameongea haya sasa na hili pia wenye akili wameongea...
 
Tunapiga kelele sana kwa mafanikio kidogo. Tusipende kuridhika na vitu vidogo.

Tujifunze kwa Wakenya. Wananunua ndege kwa idadi kubwa bila kelele. Wanajenga viwanda vikubwa na vingi maradufu ya Tanzania lakini hawapigi kelele. Wamejenga flyovers zisizo na hesabu lakini hawapigi kelele.

Kushangilia na kujisifu sana kwa mafanikio madogo husababisha kuridhika kwa madogo, na huwezi kutafuta makubwa maana unaamini uliyoyafanya ni makubwa sana.
absolutely true- nchi hii lazima ijielekeze kwenye export. Tujivune kwamba tunazalisha korosho nzuri zinazogombaniwa duniani, Kahawa nzuri yenye sifa duniani, maua mazuri yenye jina kubwa kwenye soko la Ulaya, Samaki wanaokidhi viwangi vya usalama wa vyakula duniani, ngozi first class, Vivutio vya utalii vitunze na services wanazopata watalii ni up to standard, tuzalishe nguo nzuri kutokana na pamba na tuweze ku- export duniani kote, tuzalishe mafuta ya kula kwa kutumia mbegu za alizeti na mawese yenye ubora wa kimataifa na kuuza duniani kote. Tukifanya haya yote tunaweza kujisifu
 
Tunapiga kelele sana kwa mafanikio kidogo. Tusipende kuridhika na vitu vidogo.

Tujifunze kwa Wakenya. Wananunua ndege kwa idadi kubwa bila kelele. Wanajenga viwanda vikubwa na vingi maradufu ya Tanzania lakini hawapigi kelele. Wamejenga flyovers zisizo na hesabu lakini hawapigi kelele.

Kushangilia na kujisifu sana kwa mafanikio madogo husababisha kuridhika kwa madogo, na huwezi kutafuta makubwa maana unaamini uliyoyafanya ni makubwa sana.

Unaweza leta ushahidi kuonesha Kenya imewahi kununua NDEGE? KQ imezongwa na hasara kibao MPAKA kuwaomba wakopeshaji madeni yageuzwe kuwa hisa, halafu wewe ndiyo unasema ni mfano.
Umeona Ethiopian Airways huwa haipati hasara. Wale ndo tunapaswa kuwaiga.

Hizo unazoongea ni hekaya.
 
Baki kama ulivyo na uamini kuwa Wakenya wanapewa bure au wanakodi ndege zote zaidi ya 40. Lakini ufahamu tu kuwa KQ ndiyo shirika pekee linaloenda miji yote mikuu ya Afrika.

Sijaongelea kama wanapata hasara au faida lakini wanatekeleza miradi mikubwa bila kelele. Sisi miradi midogo inageuka ndiyo hotuba ya kika mahali na ya kika kiongozi.

Daraja moja (crossover) la TAZARA tunataka tuonekane tumefanya tendo kubwa sana wakati nchi nyingine wanajenga hayo na real flovers nyingi lakini wanachukulia ni mambo ya kawaida kwa Taifa kuyafanya.
 
Do you know who is owning KQ?
And the best AIR line in Afrika?
 
Back
Top Bottom