Taarifa ya awali toka BAVICHA Mkoa wa Mbeya juu ya maandamano na kongamano la kumpongeza Tundu Tundu

king Davidson

JF-Expert Member
Feb 9, 2017
252
1,063
BAVICHA Mkoa wa Mbeya inataraji kuratibu maandamano ya kumpongeza Mwanasheria mkuu wa Chadema na mbunge wa Singida Mashariki *Mhe.Tundulisu* kwa jitihada na juhudi zake za miaka mingi katika kupigania uhai wa rasilimali za Taifa letu .Maandamano na kongamano yana nia njema ya kumtia moyo na kuwakumbusha wabunge wote wa Bunge la Jamhuri la Muungano kuwa wanajukumu kubwa na la msingi katika kusimamia rasilimali za Taifa.
Historia inampendelea Mhe.Lisu kwamba hakusubili kwanza awa Mbunge ili apambane na wizi wa Rasilimali za Taifa,ameanza tangu miaka ya 90.

Mbali ya Mhe.Lisu BAVICHA itatumia mwanya kumtangaza *Mhe.David Kafulila* kama sehemu ya vijana shujaa waliotumia nafasi zao bila uoga katika kupambana na uhujumu uchumi wa Taifa hili.
Jambo hili limethibitika Leo ambapo TAKUKURU imewafikisha Mahakamani Ndugu .Regemalila na Seth ambapo Kafulila aliibua ufisadi wao katika Bunge lililopita ,ingawa ni wazi kwamba alipitia misukosuko mingi katika kuifikia hatua hii.
Viongozi wa Dini,asasi za kiraia na watu mbali mbali wataalikwa pia kwa utaratibu utakao undaliwa.

Kwa vyovyote iwavyo, hii ni tasfiri njema kwamba hata sisi vijana tulio nje ya Bunge tunayo nafasi kwa kutumia taaluma zetu tunayo nafasi ya kupambana katika kulinda urithi wa Taifa letu.

BAVICHA mkoa wa Mbeya itaketi katika vikao vyake mapema wiki hii ili kuanda utaratibu na namna nzuri ya kuratibu zoezi hili ili i liwe na manufaa mapana zaidi kwa jamii ya Kitanzania na hususani Wakazi wa Mkoa wa Mbeya ,Na kwamba ni matarajio yetu kuwaalika *Mhe.Lisu* na *Mhe.Kafulila* ili kupokea pongezi za BAVICHA Mbeya na kwamba kwa nafasi hiyo watafanya mawasilisho ya Maada mbalimbali ili kuujuza umma namna njema ya kupigania rasilimali za Taifa.
Pia viongozi wa Dini,asasi za kiraia ,mamlaka za serikali na watu mbalimbali wataalikwa.

Ni imani yetu kuwa tutaungwa mkono na kila mzalendo wa Taifa hili.

Imetolewa na,
*Mbughi, Gwamaka S*
Katibu BAVICHA Mkoa wa Mbeya
June,19 2017
 
SAFI SANA Nawapongeza WAZALENDO WANCHI YETU kwa kuandaa KONGAMANO.

kwenye kongamano ITAKUWA POA SANA MAKAMANDA WAKITAJA ile "list of shameless" Iliyotolewa mwembe Yanga iwe faida kwa kizazi hichi na kijacho pia kumkumbusha MH. RAIS kulifanyia kazi sakata la RICHMOND.
 
kwani hao askari wataowapiga wanakaa wapi si mitaani, waache wawapige, wati wataanza cheza na familia zao kama kule visiwani
 
Back
Top Bottom