Taarifa: Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassimu Majaliwa Afanya Mazungumzo na Mbunge wa Viti Maalumu Mheshimiwa Esther Matiko

MAGALEMWA

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
6,314
2,000
Kwani kwenye kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020 walikuwa wanamunadi Ndugai? Si walikuwa wakimunandi Bw. Tundu Lissu hadi kupelekea Tundu Lissu kupata angalao kura million moja? Bila nguvu za hawa akina mama hata yule Mheshimiwa wa ubwabwa angalipata kura zaidi yake. Shukrani ya punda siku zote ni mateke.
Free stupidity
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,972
2,000
Kwani cdm ni kamati kuu peke yake na maamuzi yake ni ya mwisho? Wakina mama hao wameyakataa mauzi hayo na wamekata rufaa kwa baraza kuu. Wanasubiri maamuzi ya baraza kuu. Na hilo baraza kuu lisipofuta maamuzi ya kamati kuu, watakataa na kukata rufaa kwa mkutano mkuu wa cdm ambao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho kwenye chama kwa mjibu wa katiba ya chama hicho. Hata kama nao mkutano mkuu utakubaliana na maamuzi ya baraza kuu, bado kwa mjibu wa sheria za nchi wanaweza wakakataa uamuzi huo na kukata rufaa mahakama kuu. Mahakama kuu nayo ikatokea ikakubaliana na maamuzi ya mkutano mkuu wa cdm bado wanaweza kukataa na kukata rufaa mahakama ya rufaa ambao ndiyo wenye maamuzi ya mwisho.

Ni mchakato mrefu (a long process) kumfukuza mtu ubunge. Kosa wanalotuhumiwa nalo si la jinai. Hivyo wakihukumiwa kwenye ngazi za chini na kukata rufaa kwa ngazi inayofuata mambo yanabaki status quo- yaani utekelezaji wa maamuzi unasimama kusubiri maamuzi ya ngazi inayofuata. Hata kwenye tuhuma za jinai kubwa hususani za mauuaji ya kukusudia (murder) ambayo hukumu yake ni kunyongwa hadi kufa, huwa ni hivyo hivyo. Mtuhumiwa akishahukumiwa kunyongwa na mahakama ya chini ambayo huwa ni makakama kuu akishakata rufaa mahakama ya rufaa kuhusu hukumu hiyo, basi huwa hanyongwi bali anasubiri maamuzi ya mahakama ya rufaa. Hata kama mahakama ya rufaa (ya majaji 3) wakakubaliana na hukumu ya mahakama kuu bado mtuhumiwa anaweza kukata rufaa kwenye mahakama ya rufaa ya majaji watano - for review. Nao hao wakikubaliana na mahakama ya rufaa ya majaji watatu bado mtuhumiwa ana nafasi ya mwisho ya maamuzi ambayo ni kwa raisi wa jamhuri ya muungano ya tanzania.

Hivyo wakati tunasubiri huo mchakato mrefu wa utaratibu, kanuni na sheria za kumfukuza mbunge kwa tuhuma za kukiuka maadili ya.chama chake, wabunge hawa wanaendelea kuwa wabunge halali wa jamhuri ya muungano wa tanzania tupende au tusipende.

Unataka niyarudie na mimi nipigwe ban. Kwani hukuyaona hapo juu? Hiyo sehemu iliyotajwa kwani huwa ni ya wazi kama kichwa na pua au ni ya nguoni?

Hakuna anayekataa kuwa ni wabunge, ili sio kupitia cdm bali mamlaka ya spika fullstop.
 

Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,662
2,000
Mazungumzo hayo muhimu yamefanyika leo Februari 10,2021 Bungeni Jijini Dodoma.

Mhesh Esther Matiko ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chadema na kabla ya hapo alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime.

Chanzo: : Ofisi ya Waziri Mkuu


View attachment 1699196
Hivi ni kwanini mamlaka mbalimbali za utoaji habari wanawatambulisha hawa wabunge kuwa ni wa Chadema wakati hicho chama kimetangaza hadharani kwamba siyo wanachama wao tena?
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
49,873
2,000
PRO wa PM naona ameishiwa hata matukio hata kusalimiana imegeuka kuwa ni habari.
 

Dr Akili

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
4,160
2,000
Hakuna anayekataa kuwa ni wabunge, ili sio kupitia cdm bali mamlaka ya spika fullstop.
Walipitia cdm mlango wa nyuma. Mmeshindwa kulinda milango yenu na fensi (kama ipo) yenu. Akina mama wale wakawazidi ujanja, wakapita mlango wa nyuma. Katibu mkuu wenu akawawekea saini kwenye documents alizodhani ni za dili la kupiga pesa, kumbe zilikuwa documents za kupeleka NEC kama wateuliwa wa ubunge wa viti maalum! Siku documents hizo zitakapotolewa hadharani chama chenu kitapasuka vipande vipande. Na hapo utakuwa ndiyo mwisho wa chama chenu. Tuta wamisi sana!
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,972
2,000
Walipitia cdm mlango wa nyuma. Mmeshindwa kulinda milango yenu na fensi (kama ipo) yenu. Akina mama wale wakawazidi ujanja, wakapita mlango wa nyuma. Katibu mkuu wenu akawawekea saini kwenye documents alizodhani ni za dili la kupiga pesa, kumbe zilikuwa documents za kupeleka NEC kama wateuliwa wa ubunge wa viti maalum! Siku documents hizo zitakapotolewa hadharani chama chenu kitapasuka vipande vipande. Na hapo utakuwa ndiyo mwisho wa chama chenu. Tuta wamisi sana!

Huu utoto uliiongea hapa kampelekee mkweo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom