Chademakwanza
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 6,346
- 1,871
CHADEMA kinawataka wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na viunga vyake kuwa na subira ya kutambulishwa rasmi kwao Katibu Mkuu wa Chama, Dkt. Vincent Mashinji aliyechaguliwa na Baraza Kuu wiki iliyopita jijini Mwanza.
Aidha, Chama kinawaomba wadau, wanachama, marafiki na washabiki kujiandaa kutoa ushirikiano kwa Katibu Mkuu wakati akijiandaa kuanza kazi rasmi na kwamba kinatambua shauku na hamu kubwa waliyonayo ya kutaka kutambulishwa rasmi kwa Mtendaji Mkuu wa Chama, ila wavute subira kuruhusu kukamilika kwa maandalizi na taratibu nyingine za kiofisi.
Aidha, ombi la Uongozi wa Chama wa Dar es Salaam Kuu la kutaka kumpokea na kumtambulisha rasmi Dkt. Mashinji, Jumapili Machi 20, 2016 katika Viwanja vya Zakiem, Mbagala limeshindikana kutokana na mwingiliano wa ratiba za chama na shughuli nyingine zinazomhitaji Katibu Mkuu.
Umma utajulishwa tarehe rasmi ya tukio la utambulisho wa Katibu Mkuu, kupitia uongozi wa chama wa Dar es Salaam Kuu.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA