Taarifa toka NEC ya CCM - Yaridhia mabadiliko ya Katiba ya CCM

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,556
29,640
Taarifa kwa vyombo vya habari

Utangulizi:
Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi imefanya kikao chake maalum chini ya mwenyekiti wake wa taifa dr. Jakaya mrisho kikwete tarehe 12.02.2012. Katika kikao hicho halmashauri kuu ya taifa pamoja na mambo mengine imeamua;

Kufanya marekebisho ya katiba ya ccm ya 1977, toleo la 2010 na kanuni zake.

Halmashauri kuu ya taifa imeridhia marekebisho ya katiba ya CCM ya 1977, toleo la 2010 hivyo kubadili namna ambavyo wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa inavyopatikana.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM watakuwa katika makundi yafuatayo:-
(a) ngazi ya taifa
wajumbe 10 kutoka tanzania bara
wajumbe 10 kutoka tanzania visiwani
(b) wajumbe 10 wa kuteuliwa na mwenyekiti wa CCM taifa
(c) wajumbe wanaoingia kwa nafasi zao.
(d). Wajumbe wanaotoka kwenye vyombo vya uwakilishi
i. Wanaochaguliwa na bunge 10 (bara 8, zanzibar 2)
ii. Wanaochaguliwa na blw 5 (zanzibar 5)
(e). Wajumbe wanaochaguliwa kutoka wilayani.-221
wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa waliochaguliwa kupitia wilaya watakuwa ni viongozi wa kazi za muda wote ili kuweka wazi zaidi wajibu wa wajumbe hao wa kuwa karibu na wanachama na kushughulikia shida zao.
(f). Wajumbe toka kwenye jumuiya za chama
i. Wanaochaguliwa na uwt 15 (bara 9, zanzibar 6)
ii. Wanaochaguliwa na uvccm 10 (bara 6, zanzibar 4)
iii.wanaotokana na wazazi 5 (bara 3, zanzibar 2)

Aidha halmashauri kuu ya taifa imeamua kuwa viongozi wakuu wastaafu ngazi ya taifa waundiwe baraza la ushauri.
Baraza hilo litakuwa na wajumbe wafuatao:-
• marais wastaafu wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambao walikuwa wenyeviti wa ccm taifa.
• marais wastaafu wa zanzibar ambao pia walikuwa makamu wenyeviti wa ccm taifa.
• makamu wa mwenyekiti wa ccm taifa wastaafu.

Baraza litakuwa na kazi ya kutoa ushauri kwa chama cha mapinduzi na serikali zinazoongozwa na ccm, kwa madhumuni hayo hayo katika jambo mahsusi. Wajumbe wa baraza hilo wanaweza pia kualikwa ama wote au mwakilishi wao kuhudhuria vikao vya chama ngazi ya taifa.
Imetolewa na:

Nape M. Nnauye.
Katibu wa NEC wa itikadi na uenezi


 
Naona lengo ni kuwafungia wastaafu nje na sidhani kama hili ndo litakuwa suluhisho la matatizo na anguko la chama.
 
Bravo jk ilikua ni muda muafaka kuleta mabadiliko ya katiba ya ccm ili kwenda na wakati
 
Pongezi kwenu wana CCM, mabadiliko haya ni mwafaka katika kipindi hiki ili kukinusuru chama katika uchaguzi wake wa ndani na hata uchaguzi mkuu 2015
 
asante sana kwa taarifa

hili la marais lilisemwa na Mwana halisi CCM walikuja juu na kudai hakuna kitu kama hicho leo yametokea

i;a huu ulipaswa uletwe na akina Rejeo, ritz, FF Malaria Susu etc
 
Nahisi kuna dalili za kushughulikiana. Na kushughulikiana huku ndio mwanzo wa mwisho wa Chama tawala. Masikini CCM sijui kama itapita salama kwenye uchaguzi ndani ya chama mwaka huu. Manake watu wanajipanga ili wawe na nafasi ya kuteuliw 2015. Naona kama CCM wanatoana macho.
 
asante sana kwa taarifa

hili la marais lilisemwa na Mwana halisi CCM walikuja juu na kudai hakuna kitu kama hicho leo yametokea

i;a huu ulipaswa uletwe na akina Rejeo, ritz, FF Malaria Susu etc
Hata gazeti la Rai lilisema na Nnape akasema analipeleka kwa pilato kuwa hakuna kitu kama hicho.
 
Ni kama wamechoka kusikia ushauri wa wastaafu. Hawa CCM wanajiona ni much know.
 
Mh! Mabadiliko yamekaa kama C.C.M. kitatawala milele!

Marais,spika na waziri mkuu wasipotoka C.C.M. ina maana chama kitakosa washauri na wajumbe,na hivyo kuwa na idadi pungufu ya wajumbe!

Pia inaonekana wamekubali kuendelea na utaratibu wa rais na mwenyekiti kuwa mtu mmoja,kwa vile kama sivyo,rais hasipokuwa mwenyekiti,hawezi kuwa mshauri kwa chama!!
 
Haya ni maandalizi ya Dk (i.e.dikteta) kumsimika mtu wake 2015..
 
ndiyo tuseme wameamua kushughulika na kundi la Mkapa kwa style hii

tumemwona mwenyekiti akikerwa 'eti anasingiziwa' kumpora madaraka Pinda na kundi hili

kwa kuanzia akamwachia waziri mkuu zigo la madaktari afe nalo mwenyewe

pili ameamua kudeal na kundi hili, baada ya kujitahidi kusafisha masalia kule tiss
 
Ni suala jema sana, lakini mimi bado sijaona ukubwa wa impact yake na outcome yake katika maslahi mapana ya Chama na UMMA kwa ujumla. Kinachowakwaza wananchi wengi zaidi ni utendaji dhaifu wa Serikali ya CCM. Hivyo kama mngeamua kucapitalize kwenye utendaji wa serikali na uwajibikaji nadhani mngejiongezea credit zaidi.

Kikubwa zaidi ya yote, ni ule ufungamanisho uliopo baina ya chama na Serikali. Kwa hiyo mapungufu ya serikali, hayawezi kutenganishwa na chama, (kwani watendaji walewale wa chama ndio mawaziri wa serikali, sasa suala la chama kuiagiza serikali ni usanii mtupu). Sasa chama kitasimama vipi upande wa wananchi wananchi wanyonge, ambao ndio wapiga kura?. Mimi nilidhani mabadiliko haya yangeendana na kutenganisha kofia za Chama na Serikali (kama walivyofanya wenzenu wa ANC)
 
Wakitenganisha mawaziri wactokane na vyama matumizi yatakuwa makubwa na tutaanza tena kulalamika na huo tena utakua ni mwanzao mwingine wa matumizi mabaya ya pesa za umma,,na kwa mfano wa ANC ikumbukwe South A,,,ni nchi yenye nguvu kubwa sana kiuchumi so hata bajet yake inaruhusu...sisi hatuwezi km walimu tu na ma docta imekua timbwili la asha ngedere je huko so ndo watatumaliza kabisa na hii nusu drip ya maji iliyobaki
 
Back
Top Bottom