Taarifa rasmi: Nimeamua kujivua ukristo ukatoliki na ukristu wote kwa mara ya pili

Status
Not open for further replies.
Kumbe bado unaitukuza Ijumaa Kuu wakati imeletwa na katoliki! Waislam hatuna haja na taarifa yako maana hukua miongoni mwetu. We ambia watu wako inatosha. Nyie MNA dini zenu na sisi tuna Dini yetu.
 
Naomba niwe mkusunya sadaka... Na michango yoyote itakayo jitokeza kwa taarifa au kushtukiza
 
TAARIFA RASMI: NIMEAMUA KUJIVUA UKRISTO UKATOLIKI NA UKRISTU WOTE KWA MARA YA PILI.

Niliwahi kutamka kipindi cha nyuma na leo nimeona ni vyema nirudie kauli yangu Mimi Deogratius Kisandu. Mara ya kwanza nilijivua na baadae nililrejea tena, leo najivua rasmi na kujitoa kabisa katika imani ya Kikatoliki na Ukristu wote.

Na hivyo nimeamua kuanzisha Dini yangu mpya itakayoitwa “DINI YA UZALENDOPATRIOTIZM RELIGION’’ na itaongozwa na Kitabu Kitakatibu kitakachoitwa “DOGUMA Takataifu au DOGUMA Sanifu’’.

Naiwe mwisho leo kudhalilishwa kisa Dini za Kikoloni maana mpaka sasa sina imani tena na Dini zote zilizoletwa na Mkoloni Mweupe. Dini yangu itakuwa Dini ya Dunia nzima kwa mtu Mweusi na mtu mweupe.

Taarifa hizi ziwafikie Wakristo wote Duniani na Waislamu wote Duniani,na ifahamike kuwa mimi sijawahi kuwa Muislamu wala Mubhudha wala Dini za Jadi wala dini ya Freemanson zaidi ya kuwa Mkristo Mkatoliki, hivyo sasa Mimi ni MZALENDO na Wazalendo tunaishi Kizalendo.

Nakala imfikie Baba Mtakatifu wa Kanisa Katoliki Duniani: PAPA Fransis na Kadinari Pengo wa Tanzania na MUFTI wa WAISLAMU Tanzania.Nawakaribisha wote katika Dini yetu Mpya. Na nina watakieni IJUMAA KUU njema.

Wenu katika;

Utukufu wa Mungu Mtukuka.

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU

30 MACHI 2018
Kumbe ulikuwa mkiristu! Inawezekana mimi sikuwepo kwenye kikao ulichojitambulisha kuwa umeingia ukiristu.
 
Alipokuwa mkatoliki alikashifu upadre na kuuacha akaenda mbali Zaid kuponda madhehebu mengine, na wapo waliomsapoti Leo yanayotokea Sina haja ya kuyasemelelea.

Tambua ya kuwa Mtu mmoja anapomfanyia ubaya mwenzako jua ipo siku Hata Wewe Ule ubaya anaweza kuja kukufanyia.

Wakati Fulani nilipanga chumba sehemu sasa mpangaj mwenzang akawa anahama kwa sababu alishindwa kumalizia kodi ya pango, Baba mwenye nyumba akachukua mapazia wakati Yule mpangaj anahama pasipo mpangaj kujua, likewise mimi pia nahama baada ya kumaliza mkataba wangu, Kwangu akachukua ndoo kadhaa

Hivyo jua mwenzako anapofanyiwa ubaya jua Hata Wewe anaweza kuja kukufanyia, kama Deo aliweza kuponda wengine Leo sishangai akiponda alipokuepo.

NAWASILISHA
 
none sense! ukiamua kuacha dini acha na imani yako, sio lazima umtangazie kila mtu
 
1 kwa1 naungana na wewe na Mimi nipo mbioni kuchomoka mapema kabsa,pia nimegundua kua tunapo Fanya maombi ni sehemu ya kuwatukuza mababu wa dini zao na vizazi vyao vya wale walio tuletea Dini zao toka ughaibuni,na kubadilishwa majina na kupewa majina ya falme za uko kama,john,peter,Joseph,elizabert nk, hali ya kuwa majina yetu ya asili yenye karama nyingi toka kwa mababu zetu yamepigwa bench kama,CHOWERO,SAMNYANI,SAMADIKULI,MMBIGO,MWAKAJANAGA,MWAIPOPO,UNYANGO,KABWEDA,MKASANGA,MKUDE,BANZI,MWENDA,MCHOPA,LUKWANGULE,MANGI,nk Mimi naungana na wewe askofu mkuu kuanzia tarehe01/04/2018 narudi kwenye Dini hiyo yenye maono ya pekee kua muumini wa MZALENDO rasmi amen...!!
 
TAARIFA RASMI: NIMEAMUA KUJIVUA UKRISTO UKATOLIKI NA UKRISTU WOTE KWA MARA YA PILI.

Niliwahi kutamka kipindi cha nyuma na leo nimeona ni vyema nirudie kauli yangu Mimi Deogratius Kisandu. Mara ya kwanza nilijivua na baadae nililrejea tena, leo najivua rasmi na kujitoa kabisa katika imani ya Kikatoliki na Ukristu wote.

Na hivyo nimeamua kuanzisha Dini yangu mpya itakayoitwa “DINI YA UZALENDOPATRIOTIZM RELIGION’’ na itaongozwa na Kitabu Kitakatibu kitakachoitwa “DOGUMA Takataifu au DOGUMA Sanifu’’.

Naiwe mwisho leo kudhalilishwa kisa Dini za Kikoloni maana mpaka sasa sina imani tena na Dini zote zilizoletwa na Mkoloni Mweupe. Dini yangu itakuwa Dini ya Dunia nzima kwa mtu Mweusi na mtu mweupe.

Taarifa hizi ziwafikie Wakristo wote Duniani na Waislamu wote Duniani,na ifahamike kuwa mimi sijawahi kuwa Muislamu wala Mubhudha wala Dini za Jadi wala dini ya Freemanson zaidi ya kuwa Mkristo Mkatoliki, hivyo sasa Mimi ni MZALENDO na Wazalendo tunaishi Kizalendo.

Nakala imfikie Baba Mtakatifu wa Kanisa Katoliki Duniani: PAPA Fransis na Kadinari Pengo wa Tanzania na MUFTI wa WAISLAMU Tanzania.Nawakaribisha wote katika Dini yetu Mpya. Na nina watakieni IJUMAA KUU njema.

Wenu katika;

Utukufu wa Mungu Mtukuka.

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU

30 MACHI 2018
Nikweli kama dini ya katoliki huitaki yupo Yesu acha kukata tamaa ninaweza kukusaidia umjue Mungu wa kweli
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom