Taarifa rasmi: Nimeamua kujivua ukristo ukatoliki na ukristu wote kwa mara ya pili

Status
Not open for further replies.

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
TAARIFA RASMI: NIMEAMUA KUJIVUA UKRISTO UKATOLIKI NA UKRISTU WOTE KWA MARA YA PILI.



Niliwahi kutamka kipindi cha nyuma na leo nimeona ni vyema nirudie kauli yangu Mimi Deogratius Kisandu. Mara ya kwanza nilijivua na baadae nililrejea tena, leo najivua rasmi na kujitoa kabisa katika imani ya Kikatoliki na Ukristu wote.

Na hivyo nimeamua kuanzisha Dini yangu mpya itakayoitwa “DINI YA UZALENDOPATRIOTIZM RELIGION’’ na itaongozwa na Kitabu Kitakatibu kitakachoitwa “DOGUMA Takataifu au DOGUMA Sanifu’’.

Naiwe mwisho leo kudhalilishwa kisa Dini za Kikoloni maana mpaka sasa sina imani tena na Dini zote zilizoletwa na Mkoloni Mweupe. Dini yangu itakuwa Dini ya Dunia nzima kwa mtu Mweusi na mtu mweupe.

Taarifa hizi ziwafikie Wakristo wote Duniani na Waislamu wote Duniani,na ifahamike kuwa mimi sijawahi kuwa Muislamu wala Mubhudha wala Dini za Jadi wala dini ya Freemanson zaidi ya kuwa Mkristo Mkatoliki, hivyo sasa Mimi ni MZALENDO na Wazalendo tunaishi Kizalendo.

Nakala imfikie Baba Mtakatifu wa Kanisa Katoliki Duniani: PAPA Fransis na Kadinari Pengo wa Tanzania na MUFTI wa WAISLAMU Tanzania.Nawakaribisha wote katika Dini yetu Mpya. Na nina watakieni IJUMAA KUU njema.

Wenu katika;

Utukufu wa Mungu Mtukuka.

DEOGRATIUS NALIMI KISANDU

30 MACHI 2018
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom