Taarifa rasmi ni kuwa Clatous Chama ataendelea kukosa michezo ya Simba

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,291
5,410
Baada ya tetesi nyingi ikiwemo kuelezwa amekosana na kocha wake, taarifa nyingine za ndani zinaeleza kuwa kiungo fundi wa Simba, Clatous Chama hataonekana kwenye mechi wala mazoezini kwa mwezi mmoja kutokana na kuwa majeruhi.

Chama ambaye alikuwa akilipwa mshahara wa Tsh. Milioni 50 kwa mwezi akiwa Berkane, hajaonekana mechi kadhaa tangu alipotolewa katika kipindi cha kwanza katika mchezo dhidi ya Yanga.

Amekosa michezo dhidi ya Namungo FC Ruvu Shooting hali iliyoongeza tetesi kuwa amekorofishana na kocha wake, Pablo Franco.

Inaelezwa kuwa Chama anasumbuliwa na maumivu ya mguu wa kulia chini kwenye maungio ya ugoko na eneo la kukanyagia (Enka), iliyokuwa ikimsumbua tangu alipokuwa anacheza Berkane ya Morocco.

Licha ya kutokuwa fiti, alicheza mchezo dhidi ya Yanga na alijitonesha majeraha.

Alipoulizwa kuhusu kukaa nje, Chama amesema kweli anasumbuliwa na majeraha.

Kwa sasa anatakiwa kupumzika kwa muda wa mwezi mmoja akitakiwa kutocheza mechi wala kufanya mazoezi, hivyo anatarajiwa kuikosa michezo ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, Azam FC, Geita Gold, KMC, pia dhidi ya Pamba mnamo Mei 14 katika Robo Fainali ya ASFC.


Source: Mwanaspoti
 
Back
Top Bottom