Hilo swali halina mantiki yoyote, maana hata jibu lolote utakalopewa halitakusaidia chochote, na kumbuka hatufanyi jambo kwa sababu fulani kafanya bali kwa sababu ni muhimu na busara kulifanya
Huyo ameandika kitu asichojua kama ni kuomboleza waliomboleza siku nyingi zaidi ya tatu hizi,mimi nilikuwepo south africa kipindi hicho na maombolezo yalikua mpaka walipo zika Butiama.Kwa taarifa tu msiba wa Nyerere uliitikisa sana south africa na hata kabla hajafa Makanisa kote south africa ya watu weusi walikua wanafanya ibdada maalumu za kumuombea ili apone.Msemaji wa rais wakati huo alikua kila siku anatoa report kwa waandishi wa habari kuhusu mwalimu hali yake ilivyokua ikiendelea.Kulitokea malumbano makubwa sana ya vyombo vya habari wakati huo hasa vile vinavyomilikiwa na wazungu na vile vya waafrica.Wazungu walikua wakimponda na wengine wakipinga na kumuunga mkono sana.watu wengi waliokua wakimuunga mkono mwalimu walisema sera zake za uchumi zilishindwa sababu ya mbinu za nchi za Magharibi.
Kumbuka pia mwalimu ndiyo aliyekua mshauri mkubwa wa ANC wakati wa mazungumzo ya kumaliza ubaguzi wa rangi,kila hatua aliulizwa mwalimu na kuwaambia cha kufanya wakiwa ktk mazungumzo ya Kempton park.Hayo yote yalidhihilishwa na Rais Mbeki wakati wa moja ya ibada ya kumkumbuka Mwalimu siku Arobaini baada ya kifo chake ktk kanisa moja la katoliki mjini Pretoria. Mbeki alisema Mwalimu alikua anatuambia mambo ya kukubaliana na kukataa wakati wa mazungumzo na serikali ya makaburu. Lakini pia kumbuka kwamba ni Mwalimu aliyekua hata anawapa maagizo viongozi wa ANC kuja kupumzika ktk ktk mbuga za wanyama huko Arusha kuanzaia akina.
Hata mandela baada ya kuachana na winie alikuja kupumzika kisilisili mbugani huko Arusha na kuishi kama mtu wa kawaida na hakuna alie kua akijua pindi alipokua akitembea vijiji vya karibu.
Mbeki pia akiwa makamu wa Rais Mandela amewahi kumwambia aje kupumzika Tanzania baada ya kuomuona amefanya kazi kupumzika muda mrefu na alifanya hivyo.
Uhusiano wa Tanzania na South Africa ni mkubwa sana kama watu wengi wasivyojua vizuri.