Taarifa: Rais Kikwete aagiza bendera kupepea nusu mlingoti kwa siku tatu za maombolezo ya Kitaifa y

Hilo swali halina mantiki yoyote, maana hata jibu lolote utakalopewa halitakusaidia chochote, na kumbuka hatufanyi jambo kwa sababu fulani kafanya bali kwa sababu ni muhimu na busara kulifanya

Huyo ameandika kitu asichojua kama ni kuomboleza waliomboleza siku nyingi zaidi ya tatu hizi,mimi nilikuwepo south africa kipindi hicho na maombolezo yalikua mpaka walipo zika Butiama.Kwa taarifa tu msiba wa Nyerere uliitikisa sana south africa na hata kabla hajafa Makanisa kote south africa ya watu weusi walikua wanafanya ibdada maalumu za kumuombea ili apone.Msemaji wa rais wakati huo alikua kila siku anatoa report kwa waandishi wa habari kuhusu mwalimu hali yake ilivyokua ikiendelea.Kulitokea malumbano makubwa sana ya vyombo vya habari wakati huo hasa vile vinavyomilikiwa na wazungu na vile vya waafrica.Wazungu walikua wakimponda na wengine wakipinga na kumuunga mkono sana.watu wengi waliokua wakimuunga mkono mwalimu walisema sera zake za uchumi zilishindwa sababu ya mbinu za nchi za Magharibi.

Kumbuka pia mwalimu ndiyo aliyekua mshauri mkubwa wa ANC wakati wa mazungumzo ya kumaliza ubaguzi wa rangi,kila hatua aliulizwa mwalimu na kuwaambia cha kufanya wakiwa ktk mazungumzo ya Kempton park.Hayo yote yalidhihilishwa na Rais Mbeki wakati wa moja ya ibada ya kumkumbuka Mwalimu siku Arobaini baada ya kifo chake ktk kanisa moja la katoliki mjini Pretoria. Mbeki alisema Mwalimu alikua anatuambia mambo ya kukubaliana na kukataa wakati wa mazungumzo na serikali ya makaburu. Lakini pia kumbuka kwamba ni Mwalimu aliyekua hata anawapa maagizo viongozi wa ANC kuja kupumzika ktk ktk mbuga za wanyama huko Arusha kuanzaia akina.

Hata mandela baada ya kuachana na winie alikuja kupumzika kisilisili mbugani huko Arusha na kuishi kama mtu wa kawaida na hakuna alie kua akijua pindi alipokua akitembea vijiji vya karibu.

Mbeki pia akiwa makamu wa Rais Mandela amewahi kumwambia aje kupumzika Tanzania baada ya kuomuona amefanya kazi kupumzika muda mrefu na alifanya hivyo.

Uhusiano wa Tanzania na South Africa ni mkubwa sana kama watu wengi wasivyojua vizuri.
 
I bid farewell to our role model and hero MADIBA tunafurahia maisha yako ya upiganaji na ushujaa dunia na Binguni unaenda kuketi kwenye kiti cha enzi.

Wasio waungwana hakuna sababu ya kubeza salaam za mh Rais. Msiba wa Mzee Mandela ni wa ulimwengu sasa nyie vichenchede mnauliza swala la Tanzania kwenda kwenye mazishi. Unadhan huyo ni babu yako kule kijijini amefariki anazikwa kama Ng'ombe? Serikali na nchi kwa ujumla lazima tuwe na uwakilishi wa kutosha kwenye mazishi ya mzee MADIBA. RIP Nelson Mandela
 
!
!
nikumbushwe tu kama south africa walipeperusha bendera nusu mlingoti na kuomboleza kifo cha nyerere.
NCHI ZOTE TAJIRI DUNIANI ZIMEPEPERUSHA BENDERA NUSU MLINGOTI. magazeti yote ya Newsweek na Time yameisha toa toleo maalum la mandela na maisha yake. television zote muhimu duniani zinamtangaza mandela masaa 24. kipindi hiki makampuni makubwa yote yanatengeneza kitu kiitwacho, survenir( vitu kama vikombe vyenye picha ya mndera, handcachif, viberiti vya gesi, bendera ndogo NK). watu kwa jina la mndela wanatengeneza hivi sasa mabilion ya pesa kutokana na umaarufu wa Nelson Mandela.

Usimlinganishe Nyerere na mandela katika nani mwenye jina kubwa duniani. Nyerere, mao, Stalin, Lumumba, Lenin, Che, samora na Kim IL Sung, hawa watu wako katika group makuhani wa ukomunisti. Hawa viongozi wote niliowataja, walikuwa wanawakamata watu wasiokuwa na ajira na kuwafunga jela badala ya kuwatafutia kazi za kulipwa mishahara. nanai mtu awaheshimu hapa duniani? nani mjinga apepee bendera nusu mlingoti kwa kuomboleza vifo vyao?
hivi wewe hujagundua kuwa makuhani wa ukomunisti walikuwa na sera za ukandamizaji?
 
R.I.P Madiba, sasa ina kuwaje siku 3 zikiisha na mazishi bado? au siku ya mazishi tunafungulia tena siku ya maombolezo?
 
Pumzika kwa Amani Mzee Nelson Mandela

Jina lako litaendelea kuwa ishara ya upendo, upatanishi, uvumilivu na uaminifu.
 
Jana niliweka nyimbo za south Africa nikasikiliza siku nzima....kuna jamaa jirani akaja usiku kuazima ile cd..masikini kumbe ndio nilikuwa namuaga mzee wetu!!! I wish sasa hivi yuko na mwl nyerere pahala pema....very sad tumepoteza mtu ambae ndiye aliyekuwa amebakia mpigania haki duniani...
 
Kwani hata bendera isipowekwa kabisa kwa mwaka mzima nini kitaharibika...bendera inasaidia nini kwenye taifa zaidi ya kulitambilisha? Jaman bendera si ni kitambaa tu au kuna nini cha maana...cha msingi tunamuenzi mzee wetu mtu wa watu aliekuwa mkweli.na.mnyenyekevu
 
Aliwatetea Watu Weusi! But sio kutoka TANZANIA,sasa kwanini tunajikomba? du! ila bongo bwana! tumeanza kumfananisha BABA YETU 'NYERERE' NA BABA WA WATU 'MANDELA'
 
Ukoloni Mamboleo! Ila Mjomba Mjanja Siku alizoziweka kwa maombolezo mbona ni wkiend. mfano IJUMAA,JMOSI, mwsho JPLI, ili j3 tuendelee na ujenzi wa parokia.
 
unajidanganya sana kufikir Marekan wanamwombolezea Mandela. wao wazungu wanajua Mandela aliwasaidia namna gan kuendeleza ulaji wao huku Africa. kwataarifa yako hiyo Marekan unayozungumzia ni mwaka jana tu imemwondoa Mandela katika list ya Magaidi wa taifa hilo. fikir chukua hatua.

hoja ni kwamba bendera ya marekani nayo itapepea nusu mlingoti siku 3 km alivyoamrisha mhe rais Dr kikwete hapa tz!!
 
Mbona kifo cha Gaddafi hatukupeperusha bendera nusu mlingoti hata angalau kwa saa mbili?
 
ni ukweli usiopingika kuwa alikuwa mpigania haki za wanadamu na kujitahidi kuondoa mizizi ya ubaguzi wa rangi na kulifanya taifa lake kuwa kitu kimoja.mungu amuweke mahali pema peponi amin
 
Sioni haja kwa kuwa Mandela angekuwa mwema sana angekuja kwenye msiba wa baba wa Taifa Mwalimu Jk Nyerere.

Alisema Kuwa Haamini Kama Nyerere Ameondoka, Na Kwa Kuwa Haamini Hawezi Kuja. Akadai Kuwa Iwapo Ataiona Maiti Ya Myerere Nayeye Ni Lazima Angekufa Papo Hapo Na Kusababisha Msiba Usio Tamkika. Nafikiri Hakikosea Mkuu!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom