Taarifa: Rais Kikwete aagiza bendera kupepea nusu mlingoti kwa siku tatu za maombolezo ya Kitaifa y

"Our AFRICA has lost her greatest son" says MpigaKelele.


"Afrika tumempoteza Mwanaafrika mahiri akiwa ni mmoja ya wale waliopigania uhuru wa Waafrika kwa dhati. Uwepo wake hapa duniani nina imani umejenga kujiamini kwa waafrika wengine mahiri kuisaidia Afrika wakati wowote, ni jukumu letu waafrika kuhakikisha waafrika wenzetu wenye umahiri kuisaidia Afrika kuwapa nafasi na kuwaunga mkono wakati wote.

Mungu twaomba umlaze mahali pema peponi, Mwanaafrika Nelson Mandela.

Mungu ibariki Afrika.Amen." imesemwa na MpigaKelele
 
Kuna mijitu humu iko so negative. Hamuwezi kuelewa Mandela ni mtu wa aina gani kwa Afrika na dunia hata ingekuwa siku saba dunia imepoteza mtu muhimu sana
 
kwani jk amerudi? jk mtu wa misele, kwani watawala wajifunze kutoka kwa mkuu kuwa wawe wanatibiwa nchini mwao!
 
Wangeweka siku tatu za mapumziko. Maombolezo maana yake hakuna mapumziko jamani!
 
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.

"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21. Tunaelewa machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi, mvumilivu na mstahimilivu".
Ameongeza Rais Kikwete.

Rais amemuelezea Mzee Mandela kuwa ni kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

"Mandela ni mfano bora kwa wanadamu wa jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake" .Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela mahali pema peponi".

Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.

Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee nusu mlingoti.

Imetolewa na;

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR AS SALAAM.

06 Desemba, 2013

Pamoja na majonzi yote, hapo kwenye bluu pako sawa? Naomba kuelimishwa jamani. RIP MADIBA!
 
watu kila kitu mnaona negative side of it, lini tutakuwa postive....Mandela is another level...kama Obama naye katangaza bendera nusu mlingoti nchini kwake why not Tanzania....tuacheni kuona kila tamko la serikali sio la maana...kuna yakubeza na kukaa kimya...Mandela ni shujaa anayetambulika na kukubalika duniani kote na itabaki kuwa hivyo....

unajidanganya sana kufikir Marekan wanamwombolezea Mandela. wao wazungu wanajua Mandela aliwasaidia namna gan kuendeleza ulaji wao huku Africa. kwataarifa yako hiyo Marekan unayozungumzia ni mwaka jana tu imemwondoa Mandela katika list ya Magaidi wa taifa hilo. fikir chukua hatua.
 
Naweza kuwa najidanganya na Marekani ila sijidanganyi na the fact kuwa Mandela ni shujaa anayetambulika na kukubalika duniani....hiyo ni fact haina mjadala.
 
sasa hii wikiendi tutaifidia namna gani? hii serikali nayo bora maombolezo tungeanza jumanne
 
Kwani Nyerere alivyokufa south Africa walitangaza siku ngapi za kuomboleza?

Hata kama hawakutangaza wala kupeperusha bendera nusu mlingoti,sisi kama Tanzania ni utamaduni wetu kufanya hivyo,tulimsaidia kuingia ikulu na kupata uhuru na tutaendelea kukamilisha safari yake ya mwisho hapa duniani kwa kushiriki ktk msiba wake.
 
Marekani na Uingereza wametangaza siku 3 za maombolezo pia.

wajinga kumbe ni waafrika,kuna watu mia mbili wamekuja na roho zao za korosho kupinga kwanini bendera itakuwa nusu mringoti kwa siku tatu
 
Hilo swali halina mantiki yoyote, maana hata jibu lolote utakalopewa halitakusaidia chochote, na kumbuka hatufanyi jambo kwa sababu fulani kafanya bali kwa sababu ni muhimu na busara kulifanya
Kwani Nyerere alivyokufa south Africa walitangaza siku ngapi za kuomboleza?
 
Wanaita HİTMA....Na kwenye hitma shurti ubwabwa uwepo. Kula Ubwabwa ni sunna sheikh...Tena utapata swawabu 25 ukiusomea dua kabla hujala. Swawabu hutiririka zaidi ukila kwa mikono na shurti la kula kwa mkono ukae TAHİYATU!!
Takibiiiiiirr

Acha kubeza imani za wenzako na km hujui sema ufahamishwe sio kudandia gari kwa mbele ......... Mkubwa ww
 
Unadhani mtu akikutusi nawe unarudisha tusi vile vile?

Waliomboleza mpaka sikunya mwisho alipozikwa Butiama! walianza siku za kwanza ambazo zilikua sawa na Tanzania,halafu Mbeki akaongeza mpaka siku aliyozikwa butiama.
 
mwandishi wa habari wa Rais Msaidizi? semantically correct,
grammatically incorrect!

sahihi ni "mwandishi wa habari msaidizi, ofisi ya rais"
......kumalizia na rais msaidizi implies rais ndiye msaidizi , the implication that we have senior president
Ila sidhani kama yeye ni mwandishi wa habari msaidizi ofisi ya rais, maana ofisi ya rais inahusisha ofisi nyingi sana
 
Back
Top Bottom