TAARIFA: RADA, Fedha Uswisi, CHADEMA na Orodha ya Mafisadi

Tumaini Makene

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
2,642
6,070

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinarudia kutoa mwito kwa Rais Jakaya Kikwete kutumia mamlaka yake ya kikatiba kuagiza kukamatwa kwa watuhumiwa wote wa ufisadi wa RADA ambao CHADEMA imewataja kwa nyakati mbalimbali ikiwemo katika orodha ya mafisadi (list of shame) tarehe 15 Septemba 2007 katika Uwanja wa Mwembeyanga.

CHADEMA kinatambua kwamba kuachwa kwa mafisadi bila kuchukuliwa hatua kamili za kisheria na mali zao kufilisiwa kunafanya taifa kuendelea na ufisadi ikiwemo ule wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Richmond na sasa tuhuma mpya za ufisadi kwamba kuna vigogo wenye kiasi cha bilioni 303 kwenye akaunti Uswisi ambazo zinadaiwa kuwekwa na makampuni ya madini, mafuta na gesi asili.

Kutokana na sheria za usiri za Uswisi; CHADEMA kinaitaka Serikali inayoongozwa na CCM kuwasiliana na Serikali ya nchi hiyo ili kuanza mchakato wa kuwezesha mahakama za nchi hiyo kutoa ruhusa kutolewa kwa taarifa zote kuhusu wenye akaunti hizo na makampuni yaliyoweka kiasi hicho cha fedha ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania na Sheria za Kimataifa.

Izingatiwe pia kwenye orodha ya mafisadi CHADEMA iliwataja pia kwa majina viongozi wa serikali ambao waliingia mikataba ya kifisadi ya madini na rasilimali nyingine za taifa; kutolewa kwa taarifa hizo za benki za nje kutathibitisha ukweli na pia kubainisha watuhumiwa wengine zaidi.

Wakati huo huo; CHADEMA kinaitaka Serikali inayoongozwa na CCM kuzingatia mpango kati yake na Serikali ya Uingereza kupanga matumizi ya fedha kiasi cha Tshs. 72.3 billioni za RADA zilizorejeshwa baada ya kubainika zilizochotwa kifisadi na Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza.

CHADEMA kimeshangazwa na uamuzi wa serikali inayoongozwa na CCM kubadilisha mpango wa kujenga nyumba za walimu; kinyume na mpango huo wakati huu ambapo serikali iko katika mgogoro na walimu kutokana na kutowatimizia madai yao ya msingi ikiwemo nyongeza ya mishahara, kulipa madeni na kupunguza kodi kwenye mishahara.

CHADEMA inaitaka serikali kukumbuka kwamba mpango huo ulikuwa moja ya ushahidi muhimu uliotolewa Mahakamani kumshawishi Jaji kutoa uamuzi wa kuridhia makubaliano kati ya SFO na BAE kwamba fedha hizo zingetumika Kununua vitabu 4.4 milioni kwa ajili ya wanafunzi, vitabu 192,000 Kwa ajili ya walimu kufundishia, madawati 200,000, kujenga nyumba 1,196 za walimu wa shule za msingi vijijini, kujenga vyoo 200,000 kwenye shule za msingi.

CHADEMA imeguswa pia na taarifa kwamba zabuni ya kuchapa vitabu hivyo imetolewa kwa kampuni ya Kampuni ya Kiingereza ya Oxford University Press hali ambayo itafanya sehemu kubwa ya fedha hizo kurejea huko huko Uingereza; hivyo CHADEMA inaitaka serikali kuweka mfumo wa kuhakikisha fedha hizo kwa sehemu kubwa zinatumiwa katika viwanda vya uchapishaji vya hapa nchini ili kuchangia katika uchumi wa nchi.

Imetolewa na:

John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
25 Juni 2012

 
Do not expect miracles from this government under CCM. These are some of alerting Indicators why we really need change in the system.
 
Hawa jamaa bila kuteremka mabarabarani hawawezi kutuelewa, Hapa ishu ni nani wa kumfunga paka kengere
 
system iliyopo haifai ni lizima iondolewe serikali kiziwi na kipofu tena dhaifu ya ccm haiwez kumkamata chenge cha kusikitisha wanakaa nae meza kuu hapo ndipo utaamin kwamba serikali ni kipofu tena kiziwi kama haitoshi ni dhaifu
 
safi sana Mnyika, safi sana chama changu...hakika najivunia kuwa kwenye chama makini chadema..
 
Emphasizing emphasizing emphasizing...
Serikali ya CCM inabidi utumie saikolojia ya kitoto....kurudia rudia maneno na kutilia mkazo na msisitizo, hii safi sana hakuna kuwaacha wapumue. Wakilala wasikie RADA, wakiamka wasikie EPA, wakiwa wanapiga msosi wa makuku KIWIRA wakienda chooni haswa wakati wa kutoa kubwa MEREMETA n.k
Kuiba mnaiba lakini amani ya kuenjoy mali zetu hamtaipata......
 
...Ukisikia kushikwa pabaya ndo hii ! Dhaifu katumia fweza safari ya kwenda kukagua miche ya nyanya Brasil na kuongea na Maximo aje afundishe timu yake na Rz1.
Usijeshangaa wakienda kutembeza bakuli wakahesabu visima vya Sabodo kuwa vimejengwa na fweza za mabaki ya rushwa ya rada (ambayo ilizimika ili dege la kubebea twiga na kuro litue na kupaa !!)
 
Wewe Makene juzi ulipost habari zako za uongo kuhusu Simbachawene, kwanini hujatoa tamko kuomba radhi?
Na habari zako haziaminiki tena. Acheni kuzusha mambo.
 
Wewe Makene juzi ulipost habari zako za uongo kuhusu Simbachawene, kwanini hujatoa tamko kuomba radhi?
Na habari zako haziaminiki tena. Acheni kuzusha mambo.

Habari yako mkuu!! Hiyo habari ya Simba chawene sijaiona ila kwenye habari hii ni kitu gani cha uzushi? Hao viongozi wa CCM hawajajiwekea fedha huko Uswisi?
 
Nasisitiza tena na tena na tena, jamani raisi wetu ni dhaifu hayo mnayotaka ayatekeleze hayawezi jamani, kama mnabisha subirini basi muone.
 
Mbona sijaelewa kitu hapo, yaani Rais akamate wale mafisadi wa ile list of shame? kama sijasahau na Rais mwenyewe alitajwa, je naye ajikamate? Mbona Chadema hapo mmefuka.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
Nyie kaeni pembeni watu wafanye kazi. Nendeni kwenye mihadhara yenu uko wapi sijui!
Wengi wenu hamna kazi nyie, mnabwabwaja maneno tu ili mpate kula(ra?).
 
Back
Top Bottom