Taarifa: Police kumbe nao hawataki hayo ya Arusha

mataka

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
286
61
Wanajf 2siwalaumu police bure kumbe nao wanachukizwa na vitendo vinavyoendelea Arusha! Mie kakangu ni polisi pale Arusha, ana nyota2 begani leo ka2ambie eti ni siku ya 3 hajalala nyumbani yupo kwenye vurugu za chadema na hakuna posho za night wala nini ila ni kuumia. Eti posho yenyewe hawaongezi, mishahara hailingani na kazi wafanyazo, makazi hafifu, marupurupu hakuna ila wakubwa huko juu ndo wanafaidi! So, akasema WAMECHOKA! Akaendelea eti wana mpango wa kufanya kitu mbaya dhidi ya serikali hii ya kifisadi hadi dunia ijue ndipo hao magamba watatambua umuhimu wa polisi na kuboresha maslahi yao! Tusubiri 2one!
 
Bora yake kajisemea ukweli wake! Hana shida na dhuluma inayofanywa kwa wananchi ila "kupunjwa" posho! Angepewa posho wala asingelalamika na angeendeleza "libeneke" kuwatwanga walala hoi!
 
zINAWEZA ZIKAWA NI HADITHI HIZI, HAWA WATU NI WATIIFU SANA KWA MABOSS WAO HAKUNA MFANO DUNIANI
 
Kama ni kweli ana nyota mbili basi hadithi yako ni ya kutunga au uliamanisha V (vii) mbili?
 
Hii stori ina ukweli ndani yake, juzi pale mahakamani mchana walikuwa wanaongelea hayo
 
Uandishi wako wa sms haufai ndani ya jf. Jaribu kuedit post yako.
 
kwenye vurugu za uchaguzi mkuu mwaka jana hao hao polisi ndio walikuwa wakituhimiza tukomae hadi kieleweke bila wao matokeo ya Nyamagana yangechakachuliwa na Lawrence Masha leo angekuwa mjengoni INAWEZA ZIKAWA NI HADITHI HIZI, HAWA WATU NI WATIIFU SANA KWA MABOSS WAO HAKUNA MFANO DUNIANI [/B][/COLOR][/QUOTE]
 
Hii hadithi yako nani kakufundisha? Na kakuambia inafundisha nini?
 
Gesi la polisi ni la ccm na wala sio chombo cha dora kipo kimaslahi zaidi... Hawa jamaa pamoja na kulala kwenye nyumba zinazolingana mabanda ya kuku au mbwa wala hawawezi kamwe kukataa amri halali ya wakubwa zao kina ritz( mabwanye, mafisi maji, wasiojali wengine wala utu wa mdanganyika, wanaotamani wadanganyika waendelee kuwa masikin, wajinga, wenye afya duni kila mara ili kulinda maslah yao na watoto wao pamoja na vibaraka wao...) wenye kupenda madaraka. Unajua vyombo vingi vya ulinzi na usalama viko kimaslai zaid tena ya yule anayekuwepo madarakan na kwa sasa nao ni chichiem.
 
Hii hadithi yako nani kakufundisha? Na kakuambia inafundisha nini?

Wakuu hii siyo hadithi bali ni ukweli kabisa.Hata mimi nina ndugu yangu alikwisha kunieleza
hilo jambo.Ndio maana sasa hivi hata wanapowatawanya wananchi hawawajeruhi sana kwa
virungu kama ilivyokuwa zamani ingekuwa hivyo ungekuta mount meru Hosp pamejaa.
 
Mwelekeo wa ukombozi wa Taifa la Tanzania upo jirani sana, Kauli aliyoitoa huyo askari iwe ndio mwamsho kwa jeshi zima la polisi.
Kuungana na Jeshi la Tanzania kuleta mabadiliko ya haraka zaidi kadri iwezekanavyo kwa kuungangana na Watanzania wote, ilo
linawezekana na lifanywe haraka. Serikali ya Ccm imeshashindwa kwani imeishaifilisi nchi, watu vijijini wanafikia kufa kwa njaa,
Serikali ya Ccm ni ya mauaji ya raia pamoja na yeyote atakayetokea kuwa muhadilifu ndani ya Ccm pamoja na serikali yake.
Tunawasikilizia hao wawili walioko India kama watarudi salama, CHADEMA na Wananchi wa Tanzanzia wanataka Jeshi na Polisi mseme
basi kwa yale mabaya yanayotokea kwenye Taifa letu na kuungana kuleta mabadiliko, na kuwakamata viongozi wote walioichakaza
nchi yetu kuwafikisha katika vyombo vya sheria na kuweka serikali ya mpito. Chama cha Ccm kipigwe marufuku na kisiwepo kabisa.
Na wakati huo Katiba mpya itaundwa, Tume huru ya uchaguzi itaundwa na mambo yote yaliyofanywa kinyume na serikali ya Ccm
yatarekebishwa, na mwisho uchaguzi huru utafanyika. Tuwe watu wa kuona mbali wakati wote, ili tuijenge nchi yetu.
 
Wanajf 2siwalaumu police bure kumbe nao wanachukizwa na vitendo vinavyoendelea Arusha! Mie kakangu ni polisi pale Arusha, ana nyota2 begani leo ka2ambie eti ni siku ya 3 hajalala nyumbani yupo kwenye vurugu za chadema na hakuna posho za night wala nini ila ni kuumia. Eti posho yenyewe hawaongezi, mishahara hailingani na kazi wafanyazo, makazi hafifu, marupurupu hakuna ila wakubwa huko juu ndo wanafaidi! So, akasema WAMECHOKA! Akaendelea eti wana mpango wa kufanya kitu mbaya dhidi ya serikali hii ya kifisadi hadi dunia ijue ndipo hao magamba watatambua umuhimu wa polisi na kuboresha maslahi yao! Tusubiri 2one!

Hasomeki huyu kama tatizo lake ni posho. Ina maana ili mradi posho anayo wana chadema wakipigwa sawa tu?
 
Wanajf 2siwalaumu police bure kumbe nao wanachukizwa na vitendo vinavyoendelea Arusha! Mie kakangu ni polisi pale Arusha, ana nyota2 begani leo ka2ambie eti ni siku ya 3 hajalala nyumbani yupo kwenye vurugu za chadema na hakuna posho za night wala nini ila ni kuumia. Eti posho yenyewe hawaongezi, mishahara hailingani na kazi wafanyazo, makazi hafifu, marupurupu hakuna ila wakubwa huko juu ndo wanafaidi! So, akasema WAMECHOKA! Akaendelea eti wana mpango wa kufanya kitu mbaya dhidi ya serikali hii ya kifisadi hadi dunia ijue ndipo hao magamba watatambua umuhimu wa polisi na kuboresha maslahi yao! Tusubiri 2one!

kwa hiyo angepata posho angewajibika kwa serikali ya ccm ipasavyo?
 
kwenye picha moja gazeti la mwananchi nimeona jinsi polisi anavyojaribu kumsaidia dk wa kweli kushuka toka kwenye karandinga. Yaani amekaa tayari tayari kumsapoti mkuu ashuke salama. Polisi wanatumika tu ila mahaba yao yameshatoka ccm
 
Mshauri huyo polis ndugu yako aje ayaanike hapa jamvin mwenyewe kama unayoyasema ni ya ukweli.
Ili atupe ufafanuz mzuri na majibu ya kina kwa maswali ya wadau
 
Back
Top Bottom