Taarifa: PCCB Mtuhumiwa Wenu Huyoooo Amekimbia! Mkamateni Jamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa: PCCB Mtuhumiwa Wenu Huyoooo Amekimbia! Mkamateni Jamani!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndebile, Mar 19, 2012.

 1. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Huyu ni mfamasia wa jiji la Mwanza Bw. Edward, kwa wiki sasa yupo chini ya uchunguzi kuhusu ubadhilifu wa mali ya umma, uchunguzi ambao pia PCCB wanashiriki.

  Janja anayoifanya mtuhumiwa kuna uwezekano mkubwa akawaachia koti, tangu majuzi mfamasia huyo anachakachua Issue Voucher za vifaa na madawa ili ionekane kweli alisambaza vifaa tiba na dawa katika vituo vya afya na zahanati za jiji kumbe sio kweli. Taarifa za uhakika ni kwamba kituo cha afya X wamemkatalia mbinu yake chafu baada kutaka wachakachue issue voucher za tangu 2010, kituo Y wamekubali na kituo Z tangu asubuhi ya leo mfamasia huyo amekuwa akipiga simu kuomba mtunza dawa wafanye uharibifu huo.

  MY TAKE: Mtandao wa wizi wa vifaa na dawa hapa jiji ni mpana, kuanzia mganga mkuu, mratibu wa Mpango wa kupambana na Ukimwi n.k. Nenda vituo vya afya vyote vya jiji hakuna vitenganishi vya kupima Ukimwi tangu juni 2010 wakati hospitali za mkoa, Mwananchi, Jeshi zina vifaa vya kumwaga, dawa mseto za malaria vituo vya jiji kuna zile za watoto tu (ambazo hazina soko) za watu wazima hakuna, mzigo unapelekwa Congo na Edward anafahamika jiji zima kama 'Wakala' wa dawa mseto.

  Kama uchunguzi wenu PCCB unalenga kukagua vitabu tu, mmeliwa nenda vituoni muone wagonjwa wanavyotaabika. Hakina Edward ndio kiini cha mgogoro kati ya serikali na madaktari.
   
 2. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Network search,,,,
   
 3. g

  gosam New Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  afadhari mwanza hata kuna uchunguzi,kwingine huku ndo miungu watu mpaka pccb wanabaki kuomba ofa viti virefu
   
 4. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,542
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Michezo ya namna hii ipo sana karibu kwenye kila sekta . Watu wengi sana kwenye maofisi mbali mbali wanaiba sana , siyo serikalini, mashirika binafsi. Viwandani , kwenye NGO's ,mashulen na sehem mbali mbali hi michezo ipo sana. Ukitazama karibu kila mtanzania mwenye kazi anaishi zaidi ya kipato chake halali . Unafikiri wanatoa wapi hela ya ziada ya kufanya hivyo ? Ndio maana unakuta mtu amemaliza chuo na kuanza kazi lakini ndani ya miaka 3 unamkuta ana nyumba 2 na magari kadha . Watanzania wengi sana wanapenda hela ya fasta mno .
   
 5. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Sioni kama PCCB wako well trained kwenye maswala ya uchunguzi. Kwa kiasi kikubwa ni hangover ile ile ya Jeshi la Polisi. Bado wanachukua muda mrefu sana kwenye uchunguzi na hilo linatoa mwanysa kwa watuhumiwa kuharibu ushahidi
   
 6. hengo

  hengo JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I hate thieves,ikithibitika adhibiwe ipasavyo na washiriki wake wote
   
 7. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  ndo maana drs waliwakatalia kwenye mazungumzo. Wanajua madudu wanayoyafanya yanayosababisha wagonjwa kukosa dawa. Walipofika kwenye kikao wakaanza kuwapiga vijembe madaktari pamoja na kanali wa jeshi wa nursing. Hawa jamaa huwa wanafanya hivi makusudi wakijua lawama zote zitaishia kwa madaktari maana ni wananchi wachache sana wanaojua kuna watu wanaitwa wafamasia. Ndo maana hata pinda aliropoka kwamba madaktari wanamwibia dawa zake.
   
 8. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hivi kazi za pccb si kupamba na kuchochea rushwa? Sasa wataweza kumkamata jamaa wakati wanakula naye? Kuna utofauti wa hawa jamaa na tiss?
   
 9. Ndebile

  Ndebile JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 3,631
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna kutoelewana wenyewe kwa wenyewe,wazi wametofautiana wakaamua kulipuana tu.
   
 10. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Ndio maana wafamasia hawawezi kugoma, japo wanapata mshahara mdogo sana kulinganisha na madaktari ila wanajua namna ya kufanya topup kulingana na kazi zao.
   
Loading...