Taarifa nilizopata juu ya chaguzi za CCM; ni hatari kwa nchi hii

Tatizo wanalipwa kidogo sana!! Kumbuka mtu bwege anachaguliwa kuwa madarakani kwa miaka 5!
Bora hao wanaopata hata hicho kidogo, kuna wengine hawapati kabisa.

Mi ngekuwa nazipata nisingechukua chini ya milioni 20 kwa kichwa iwe diwani, mbunge.

Wapuuzi hao wakiisha chaguliwa hawaonekani na hawakamatiki na hujiona wajanja na wenye akili sana.
 
Habari nzito sana hizi. Nakupongeza kwa kuibua hizi tuhuma na kama unavyosema umepiga simu maeneo mbalimbali ya nchi yetu.
Nashauri wewe na wengine wote wenye taarifa mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kupatikana kwa ushahidi, watoe ushirikiano kwa vyombo husika. Isiishie tuu kutuhumu na kusema huku.

Niwahakikishie taarifa nzuri na stahiki zitasaidia sana kuwabaini wale wote waliojihusisha kutoa na kupokea rushwa. Itasaidia sana hatua stahiki kumchukulia.
 
Unataka atawale masikini ili iweje sema mfumo ubadirike namna ya kuwapata hao wajumbe au idadi iongezeke, mashart ya wagombea yaongezeke sio kila mtu anaweza kugombea.
Mtu apimwe kwa ubora wake hivi mtu mtoa rushwa akipata uongozi sikunakuwa na conflict of interest na utendaji uharibiwe kisa rushwa imagine unahonga upate uongozi then zibatokea tender zinahtaji watu Bora wewe unatafta watu wako less qualified vile wamekuhonga huoni hyo tender ka ni masilahi ya taifa kazi itaharibika.
Mtu yoyote apite kwa vigezo na utendaji na sio kwa vile alitoa rushwa, kwanza kwanini utoe rushwa huko bungeni Kuna biashara gani utakayofanya ili urudishe fidia.
Maana watoa rushwa wengi hawana vigezo na rushwa hupofusha Mambo mengi na ndio maana Africa tuko hapa kisa rushwa kwa watu wasio na vigezo.
Rushwa hufanya watu wanunue haki zao wakati wangetakiwa wapate free.
Hyo kusema viongozi maskini wa Nini mbona Nyerere hakuonga mahali, akaongoza mapambano wa Uhuru wa Tanganyika, kina Mkapa, Mwinyi, hii tabia ya kupata viongozi kisa rushwa ka taifa tutavuna tulichopanda.
 
Nimeona clip ikisemekana ni waziri wetu wa elimu akiwa ndani ya gauni la kitenge akiwezesha wajumbe nje ya geti.
Natafuta habari za mzee wetu aliyezaliwa Kilosa, tuone umahiri wa sheria ulimuongozaje.
Hadi mama wa elimu naye aliwapa wajumbe Cha juu mbona hii ni hatari, Bora warudishe ile wanachama wote sehemu husika kupigia majina matatu yaliyo rudishwa kiuwazi kabisa.
 
Wengi waliopata kura chache ni wale ambao hawakuhonga I wish hii tabia ikomeshwe Mara moja bila hivo maskini watabaki watawaliwa tu
Hii ni hatari. Mamlaka inatakiwa ichukue jukumu maana hii inaweza kuingia hata kwenye sekta nyingine kama ajira. Inaweza kulenga vijana wa chama fulani ambao katika mchujo wenye pesa au ndugu watanufaika. Siasa itawaliwe tu na wa chama fulani na ajira chama hicho hicho tena kwa rushwa tutatokea wapi.
Angalia vyuoni huko vijana wanahamasihwa kujiunga uvccm eti ni fursa kwao. Fursa gani.
Kuna watu wanataka kumharibia rais wakifikiri wanamfurahisha. Walaaniwe.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Nawaomba mnisome hapa:
Mchakato wa kutafuta wagombea ndani ya CCM umeibua mambo mengi ambayo ni vizuri kuyajadili. Muhimu ni kuelewa kwamba kwa mpangilio wa vyombo vya uasalama na ukubwa wa CCM, bado kitakuwa ndicho chama kitakachoongoza nchi hii kwa miongo ijayo. Tatizo langu ni ukomavu na njia potofu zinazotumika kupata viongozi. Njia hizi zinasambaza uozo na mfumo mbovu ndani ya nchi hii.

Nimewasiliana na watu mbali mbali: Nimepiga simu Kusini kabisa Nanyumbu, nikapiga simu kaskazini Ukerewe na Kyerwa, nikapiga simu magharibi kigoma kaskazini na Buhigwe, nikarudi mashariki Dar na Mkuranga. Hapo katikati nikaongea na Manyoni magharibi na Singida Kaskazini. Sehemu zote hizo rushwa ilitumika kuwapata wagombea wa Ubunge na sasa kuna mipango maalumu ya jinsi ya kuwapata madiwani.

Mambo yako hivi; viongozi wa CCM ktk majimbo haya niliyoyataja, yaani wenyeviti wa Wilaya na makatibu wao wamejipanga ili kila wakati wafaidike na pesa za serikali kupitia halmashauri. Wanachopanga sasa hivi ni kujihakikishia nani awe Diwani, nani awe mbunge na ktk hao nani ateuliwe kuwa M/kiti wa halmashauri. Wazoefu ktk uchaguzi wametoa pesa kwa weneyviti na makatibu wao ili kuwalainisha na kuwasaidia kuwaelekeza hawa tunaowaita ’wajumbe.’

Kutokana na mpangilio huo, Viongozi wa CCM wanajihakikishia njia ya kupata pesa za halmashauri. Hii ni moja ya mbinu ambayo imewasambaratisha wagombea ambao huenda wana mipango na malengo mazuri ya majimbo yao. Hawatakiwi! Kwa haraka utaona kama ni tatizo la CCM lakini ni tatizo kwa wananchi wote wa nchi hii. Je, rais au Mkiti wa CCM analifahamu hili. Je anaamini atawasimamia? Sisi tunataka mfumo na siyo kusimamiwa kwa vitisho. Kwa mtindo huu, hatutapata mfumo.
Toeni mauchafu yenu, shida yenu ni kudhani mnaimiliki hii nchi,

Kama ccm wataleta wagombea wala rushwa kwa Nini usihamasishe wapiga kura kuwakataa na kupigia wagombea wa vyama vingine? Ili tuwe na bunge na serikali ,opposition, na raisi opposition
 
Nilikuwa nimetembelea mkoa wa Kilimanjaro tarehe 1 hadi 5 Juni. Rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea huko. Mmoja kati ya hao watia nia alipita kila tarafa kuonana na wajumbe wa tarafa na alimwaga milioni 25 kwa wajumbe kila tarafa wagawane. Alikuwa anatamba kuwa nitaona mgombea atakayeruka huo mlima wangu. Rafiki yangu haamini katika rushwa. Aliambulia kura 3 japo kweli ndiye anakubalika. Kigogo mtoa rushwa ndiye alipata kura nyingi. Taarifa ziko takukuru tunangoja matangazo kutoka vikao vya ndani.
Kwa hali hii; bunge litaendelea kuwa kundi la washangiliaji na wasifiaji.
 
Hii ni hatari. Mamlaka inatakiwa ichukue jukumu maana hii inaweza kuingia hata kwenye sekta nyingine kama ajira. Inaweza kulenga vijana wa chama fulani ambao katika mchujo wenye pesa au ndugu watanufaika. Siasa itawaliwe tu na wa chama fulani na ajira chama hicho hicho tena kwa rushwa tutatokea wapi.
Angalia vyuoni huko vijana wanahamasihwa kujiunga uvccm eti ni fursa kwao. Fursa gani.
Kuna watu wanataka kumharibia rais wakifikiri wanamfurahisha. Walaaniwe.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Ni hatari Sana rushwa jinsi zilivo tawala si ipo siku watauza nchi kwa mabeberu kisa kupewa pesa nyingi. Hii rushwa ya kupata viongozi ni hatari Sana Hawa ndo watunga Sheria ndio wanaopitisha Sheria mbovu ka za madini kisa walipewa Cha juu.
Hamna taifa lililoendelea kwa kuendekeza Wala rushwa humu duniani, zaidi ya viongozi waliokuwa na maono ya kuwavusha na kuweka mipango ya maendeleo, Sasa Hawa wa rushwa wasio na vigezo Wana kipi Cha ku offer. Naipenda China ukila rushwa ni kunyongwa tu. Hii tabia ikiendelea italeta Makundi kwenye jamii mwishowe kuwe na struggle of power Kati ya wenye nacho na wasio nacho.
Rushwa ni adui wa haki, taifa na maendeleo
 
Kwa hali hii; bunge litaendelea kuwa kundi la washangiliaji na wasifiaji.
Wakiwa bungeni kila kitu ndio Kuna vitu vya hovyo tu wanapitisha, siku hayo masilahi ya ubunge na kiinua mgongo vikipunguzwa ka watumishi wengine ndio tutapata watu wazalendo kwelikweli
 
Nasikia na ndugu yetu wa Ilala katembeza 100000 kwa wajumbe ka njugu.
CCM na rushwa ni samaki na maji
 
Ni hatari Sana rushwa jinsi zilivo tawala si ipo siku watauza nchi kwa mabeberu kisa kupewa pesa nyingi. Hii rushwa ya kupata viongozi ni hatari Sana Hawa ndo watunga Sheria ndio wanaopitisha Sheria mbovu ka za madini kisa walipewa Cha juu.
Hamna taifa lililoendelea kwa kuendekeza Wala rushwa humu duniani, zaidi ya viongozi waliokuwa na maono ya kuwavusha na kuweka mipango ya maendeleo, Sasa Hawa wa rushwa wasio na vigezo Wana kipi Cha ku offer. Naipenda China ukila rushwa ni kunyongwa tu. Hii tabia ikiendelea italeta Makundi kwenye jamii mwishowe kuwe na struggle of power Kati ya wenye nacho na wasio nacho.
Rushwa ni adui wa haki, taifa na maendeleo
Hivi kwani mabeberu ni lazima wawe na rangi nyeupe? Je ni lazima wawe wa kutoka ughaibuni yaani ulaya na Marekani? Kwa nini wale wezi wa Epa wasiwe ni mabeberu? Kwanini wale waliopitisha mikataba mibovu wasiwe mabeberu? Tunawatafuta mabeberu kumbe tunao hapahapa. Yaani baadhi ya wabunge wetu ni mabeberu wakubwa. Hata ndani ya chama kileee cha siasa wamejaa tele.
Au labda mnielimishe kuwa mabeberu ni nani?
 
Beberu ni mtu yoyote anayeenda kinyume na masilahi ya walipa Kodi, Kuna mabeberu wa nje na mabeberu wa ndani Sasa Hawa wa ndani mabeberu weusi ndio hatari kwa mstakabali wa nchi maana wanatafta madaraka kwa kuhonga Sasa wakiwa mjengoni ndio kuuza nchi mazima. Na Hawa mabeberu weusi ndio wameifikisha nchi hapa tulipo
 
Nchi imeoza, hapa tatizo si watia nia, tatizo ni wajumbe,
Nionavyo, Wajumbe ni watu wa kuonea huruma tu! Hawa ni watu wanaoishi bila mshahra, bila posho kwa miaka 5. Na pia elimu ndogo. Wanapojikuta mbele ya mtu mwenye pesa, hawana maamuzi ya akili. Wanaostahili kulaumiwa ni viongozi wa wilaya. Katibu na Mkiti, wanakuwa na bei ndogo sana!
 
Unakifahamu unachokiongea ndugu? Au unataka kumharibia Mheshimiwa Mkundi?
Uliponishambulia nilijiuliza kama kweli naonea watu maana kipindi hiki ni cha kujenga makundi. Nimefunyua tena kujua huyo unayemtetea ana nguvu gani. Taarifa niliyopewa ni hii; nguvu pekee anayoitegemea ni kulazimisha matokeo. Ni Mbunge ambaye anapopewa kura, huwa anahamia Sengerema kwa maisha yake ya kila siku. Hakuna chochote anachokiita ni mali yake ndani ya Ukerewe. Wapiga kura (siyo wajumbe) Hawana hamu naye! Mbaya zaidi ana maadui aliowapata baada ya kuhama chama. Nguvu ya ziada nje ya taratibu inatakiwa ili aweze kupitishwa kuwa mbunge.

Kwa uongozi hadi leo taarifa zinatufikia kwamba bado wanapanga nani agombee udiwani wapi na baadhi ya wajumbe wanaitwa kurekebisha maoni yao. Upo? Hiyo ndo CCM.
 
Nionavyo, Wajumbe ni watu wa kuonea huruma tu! Hawa ni watu wanaoishi bila mshahra, bila posho kwa miaka 5. Na pia elimu ndogo. Wanapojikuta mbele ya mtu mwenye pesa, hawana maamuzi ya akili. Wanaostahili kulaumiwa ni viongozi wa wilaya. Katibu na Mkiti, wanakuwa na bei ndogo sana!
Ndio maana kumbe democracy ikiruhusiwa Sana Kuna watu waelewa mdogo wataharibu kwa mtindo huo, na hata hao makatibu ndo walio organize rushwa
 
Back
Top Bottom