Taarifa nilizopata juu ya chaguzi za CCM; ni hatari kwa nchi hii

View attachment 1537326
Kwa CCM, rushwa ni kama hewa ya oxygen, rushwa ni uhai na bila rushwa CCM itakufa. Rushwa lazima ilindwe kwa mtutu wa bunduki. Anayepiga vita rushwa anaipiga vita CCM. Na huo ndio ukweli mchungu.

Mdogo ndani ya CCM anakula kwa mamia, wa kati anakula kwa mamilioni na wa juu kabisa anakula kwa matrilioni. Hii kwa lugha ya wana mahesabu nguli wa miaka ilee, inaitwa direct proportion.
Rushwa nchi hii ngumu sana
Rushwa watu wanatoa kila leo
Rushwa ihalalishwe tu

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
View attachment 1537326
Kwa CCM, rushwa ni kama hewa ya oxygen, rushwa ni uhai na bila rushwa CCM itakufa. Rushwa lazima ilindwe kwa mtutu wa bunduki. Anayepiga vita rushwa anaipiga vita CCM. Na huo ndio ukweli mchungu.

Mdogo ndani ya CCM anakula kwa mamia, wa kati anakula kwa mamilioni na wa juu kabisa anakula kwa matrilioni. Hii kwa lugha ya wana mahesabu nguli wa miaka ilee, inaitwa direct proportion.
Na wako tayari hata kumpoteza yeyote atakaye tangaza habari za rushwa hata kama ni mwenzao. Hawa jamaa ni zaidi ya mafisi
Screenshot_20200814-185644.jpg
 
Nawaomba mnisome hapa:

Mchakato wa kutafuta wagombea ndani ya CCM umeibua mambo mengi ambayo ni vizuri kuyajadili. Muhimu ni kuelewa kwamba kwa mpangilio wa vyombo vya uasalama na ukubwa wa CCM, bado kitakuwa ndicho chama kitakachoongoza nchi hii kwa miongo ijayo. Tatizo langu ni ukomavu na njia potofu zinazotumika kupata viongozi. Njia hizi zinasambaza uozo na mfumo mbovu ndani ya nchi hii.

Nimewasiliana na watu mbali mbali: Nimepiga simu Kusini kabisa Nanyumbu, nikapiga simu kaskazini Ukerewe na Kyerwa, nikapiga simu magharibi kigoma kaskazini na Buhigwe, nikarudi mashariki Dar na Mkuranga. Hapo katikati nikaongea na Manyoni magharibi na Singida Kaskazini. Sehemu zote hizo rushwa ilitumika kuwapata wagombea wa Ubunge na sasa kuna mipango maalumu ya jinsi ya kuwapata madiwani.

Mambo yako hivi; viongozi wa CCM ktk majimbo haya niliyoyataja, yaani wenyeviti wa Wilaya na makatibu wao wamejipanga ili kila wakati wafaidike na pesa za serikali kupitia halmashauri. Wanachopanga sasa hivi ni kujihakikishia nani awe Diwani, nani awe mbunge na ktk hao nani ateuliwe kuwa M/kiti wa halmashauri. Wazoefu ktk uchaguzi wametoa pesa kwa weneyviti na makatibu wao ili kuwalainisha na kuwasaidia kuwaelekeza hawa tunaowaita ’wajumbe.’

Kutokana na mpangilio huo, Viongozi wa CCM wanajihakikishia njia ya kupata pesa za halmashauri. Hii ni moja ya mbinu ambayo imewasambaratisha wagombea ambao huenda wana mipango na malengo mazuri ya majimbo yao.

Hawatakiwi! Kwa haraka utaona kama ni tatizo la CCM lakini ni tatizo kwa wananchi wote wa nchi hii. Je, rais au Mkiti wa CCM analifahamu hili. Je anaamini atawasimamia? Sisi tunataka mfumo na siyo kusimamiwa kwa vitisho. Kwa mtindo huu, hatutapata mfumo.
Viongozi wa CCM? Big no! Sema viongozi maana hao unaowasema wa CCM kesho wanaweza kuwa wa TADEA
 
Back
Top Bottom