Taarifa nilizopata juu ya chaguzi za CCM; ni hatari kwa nchi hii

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
1,523
2,000
Nawaomba mnisome hapa:

Mchakato wa kutafuta wagombea ndani ya CCM umeibua mambo mengi ambayo ni vizuri kuyajadili. Muhimu ni kuelewa kwamba kwa mpangilio wa vyombo vya uasalama na ukubwa wa CCM, bado kitakuwa ndicho chama kitakachoongoza nchi hii kwa miongo ijayo. Tatizo langu ni ukomavu na njia potofu zinazotumika kupata viongozi. Njia hizi zinasambaza uozo na mfumo mbovu ndani ya nchi hii.

Nimewasiliana na watu mbali mbali: Nimepiga simu Kusini kabisa Nanyumbu, nikapiga simu kaskazini Ukerewe na Kyerwa, nikapiga simu magharibi kigoma kaskazini na Buhigwe, nikarudi mashariki Dar na Mkuranga. Hapo katikati nikaongea na Manyoni magharibi na Singida Kaskazini. Sehemu zote hizo rushwa ilitumika kuwapata wagombea wa Ubunge na sasa kuna mipango maalumu ya jinsi ya kuwapata madiwani.

Mambo yako hivi; viongozi wa CCM ktk majimbo haya niliyoyataja, yaani wenyeviti wa Wilaya na makatibu wao wamejipanga ili kila wakati wafaidike na pesa za serikali kupitia halmashauri. Wanachopanga sasa hivi ni kujihakikishia nani awe Diwani, nani awe mbunge na ktk hao nani ateuliwe kuwa M/kiti wa halmashauri. Wazoefu ktk uchaguzi wametoa pesa kwa weneyviti na makatibu wao ili kuwalainisha na kuwasaidia kuwaelekeza hawa tunaowaita ’wajumbe.’

Kutokana na mpangilio huo, Viongozi wa CCM wanajihakikishia njia ya kupata pesa za halmashauri. Hii ni moja ya mbinu ambayo imewasambaratisha wagombea ambao huenda wana mipango na malengo mazuri ya majimbo yao.

Hawatakiwi! Kwa haraka utaona kama ni tatizo la CCM lakini ni tatizo kwa wananchi wote wa nchi hii. Je, rais au Mkiti wa CCM analifahamu hili. Je anaamini atawasimamia? Sisi tunataka mfumo na siyo kusimamiwa kwa vitisho. Kwa mtindo huu, hatutapata mfumo.
 
MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
3,737
2,000
Umeitaja Ukerewe na wakati huu niko huku. Hapa Ukerewe siyo siri. Mambo yako wazi kabisa. Kilichofanyika na kinachoeleweka kwa watu wa hapa ni kwamba. Mbunge aliyehamia CCM hakubaliki.

Kura za maoni amepita na haijulikani jina litarudi au hapana. Lakini kupita kwake ni rushwa kwa kusaidiwa na viongopzi wa CCM wa Wilaya; Mkiti, Katibu, PCCB na usalama wa Wilaya, wote walipigwa milioni 5 kila mtu.

Siku ya uchaguzi kila mjumbe akarushiwa 70 kwenye simu yake. Niambie mtu wa aina hiyo au mfumo wa aina hiyo utatuletea nini. Yaonekana ni nchi nzima ndo mfumo uliotumika.
 
mavela

Senior Member
Oct 1, 2014
148
225
Umeitaja Ukerewe na wakati huu niko huku. Hapa Ukerewe siyo siri. Mambo yako wazi kabisa. Kilichofanyika na kinachoeleweka kwa watu wa hapa ni kwamba. Mbunge aliyehamia CCM hakubaliki. Kura za maoni amepita na haijulikani jina litarudi au hapana. Lakini kupita kwake ni rushwa kwa kusaidiwa na viongopzi wa CCM wa Wilaya; Mkiti, Katibu, PCCB na usalama wa Wilaya, wote walipigwa milioni 5 kila mtu.

Siku ya uchaguzi kila mjumbe akarushiwa 70 kwenye simu yake. Niambie mtu wa aina hiyo au mfumo wa aina hiyo utatuletea nini. Yaonekana ni nchi nzima ndo mfumo uliotumika.
Unakifahamu unachokiongea ndugu? Au unataka kumharibia Mheshimiwa Mkundi?
 
mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
4,166
2,000
Lila na Fila Havitengamani
Nilikuwa nimetembelea mkoa wa Kilimanjaro tarehe 1 hadi 5 Juni. Rafiki yangu mmoja alikuwa anagombea huko. Mmoja kati ya hao watia nia alipita kila tarafa kuonana na wajumbe wa tarafa na alimwaga milioni 25 kwa wajumbe kila tarafa wagawane.

Alikuwa anatamba kuwa nitaona mgombea atakayeruka huo mlima wangu. Rafiki yangu haamini katika rushwa. Aliambulia kura 3 japo kweli ndiye anakubalika. Kigogo mtoa rushwa ndiye alipata kura nyingi. Taarifa ziko takukuru tunangoja matangazo kutoka vikao vya ndani.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
54,686
2,000
Umeitaja Ukerewe na wakati huu niko huku. Hapa Ukerewe siyo siri. Mambo yako wazi kabisa. Kilichofanyika na kinachoeleweka kwa watu wa hapa ni kwamba. Mbunge aliyehamia CCM hakubaliki. Kura za maoni amepita na haijulikani jina litarudi au hapana. Lakini kupita kwake ni rushwa kwa kusaidiwa na viongopzi wa CCM wa Wilaya; Mkiti, Katibu, PCCB na usalama wa Wilaya, wote walipigwa milioni 5 kila mtu.

Siku ya uchaguzi kila mjumbe akarushiwa 70 kwenye simu yake. Niambie mtu wa aina hiyo au mfumo wa aina hiyo utatuletea nini. Yaonekana ni nchi nzima ndo mfumo uliotumika.
Sasa mtu anatoa rushwa hivyo, akipata ubunge hizo hela zake atazirudisha vipi?

Bungeni kuna biashara gani?
 
gTurn

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
455
500
Ccm hawafai kabisa mim nimeshiriki hizi mambo za kura za maoni mwaka huu 2020..sijui kwa miaka mingine ila kwa mwaka huu nauhakika rushwa nimeshuhudia mwenyewe 100% kwakweli pesa imetembea na tusitegemee viongozi waadilifu lazima watarudisha chao..hapo ndio deals zitatembea
 
Kipangaspecial

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
10,991
2,000
Nawaomba mnisome hapa:
Mchakato wa kutafuta wagombea ndani ya CCM umeibua mambo mengi ambayo ni vizuri kuyajadili. Muhimu ni kuelewa kwamba kwa mpangilio wa vyombo vya uasalama na ukubwa wa CCM, bado kitakuwa ndicho chama kitakachoongoza nchi hii kwa miongo ijayo. Tatizo langu ni ukomavu na njia potofu zinazotumika kupata viongozi. Njia hizi zinasambaza uozo na mfumo mbovu ndani ya nchi hii.

Nimewasiliana na watu mbali mbali: Nimepiga simu Kusini kabisa Nanyumbu, nikapiga simu kaskazini Ukerewe na Kyerwa, nikapiga simu magharibi kigoma kaskazini na Buhigwe, nikarudi mashariki Dar na Mkuranga. Hapo katikati nikaongea na Manyoni magharibi na Singida Kaskazini. Sehemu zote hizo rushwa ilitumika kuwapata wagombea wa Ubunge na sasa kuna mipango maalumu ya jinsi ya kuwapata madiwani.

Mambo yako hivi; viongozi wa CCM ktk majimbo haya niliyoyataja, yaani wenyeviti wa Wilaya na makatibu wao wamejipanga ili kila wakati wafaidike na pesa za serikali kupitia halmashauri. Wanachopanga sasa hivi ni kujihakikishia nani awe Diwani, nani awe mbunge na ktk hao nani ateuliwe kuwa M/kiti wa halmashauri. Wazoefu ktk uchaguzi wametoa pesa kwa weneyviti na makatibu wao ili kuwalainisha na kuwasaidia kuwaelekeza hawa tunaowaita ’wajumbe.’

Kutokana na mpangilio huo, Viongozi wa CCM wanajihakikishia njia ya kupata pesa za halmashauri. Hii ni moja ya mbinu ambayo imewasambaratisha wagombea ambao huenda wana mipango na malengo mazuri ya majimbo yao. Hawatakiwi! Kwa haraka utaona kama ni tatizo la CCM lakini ni tatizo kwa wananchi wote wa nchi hii. Je, rais au Mkiti wa CCM analifahamu hili. Je anaamini atawasimamia? Sisi tunataka mfumo na siyo kusimamiwa kwa vitisho. Kwa mtindo huu, hatutapata mfumo.
Mwanaccm hasiyeshiriki vitendo vya Rushwa ana harufu za umamluki.
Maccm na rushwa ni chanda na pete.
 
Mimi.

JF-Expert Member
Sep 7, 2011
1,307
2,000
Shida ni kuwa wenye hela ndo itakuwa kigezo Cha kuwa kiongozi kwahyo wasio na hela na uwezo hawatapata nafasi hyo ni hatari Sana, Sasa huyo mtoto wa jaji ndio kinara wa rushwa

Kwa kweli ni Kinara kama ameweza kutoa million zote hizo

Watoto wa maskini hawezi kuonga na wengi ndio wanakua wana qualifications zote za kushinda tatizo pesa
 
Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,774
2,000
Nawaomba mnisome hapa:
Mchakato wa kutafuta wagombea ndani ya CCM umeibua mambo mengi ambayo ni vizuri kuyajadili. Muhimu ni kuelewa kwamba kwa mpangilio wa vyombo vya uasalama na ukubwa wa CCM, bado kitakuwa ndicho chama kitakachoongoza nchi hii kwa miongo ijayo. Tatizo langu ni ukomavu na njia potofu zinazotumika kupata viongozi. Njia hizi zinasambaza uozo na mfumo mbovu ndani ya nchi hii.

Nimewasiliana na watu mbali mbali: Nimepiga simu Kusini kabisa Nanyumbu, nikapiga simu kaskazini Ukerewe na Kyerwa, nikapiga simu magharibi kigoma kaskazini na Buhigwe, nikarudi mashariki Dar na Mkuranga. Hapo katikati nikaongea na Manyoni magharibi na Singida Kaskazini. Sehemu zote hizo rushwa ilitumika kuwapata wagombea wa Ubunge na sasa kuna mipango maalumu ya jinsi ya kuwapata madiwani.

Mambo yako hivi; viongozi wa CCM ktk majimbo haya niliyoyataja, yaani wenyeviti wa Wilaya na makatibu wao wamejipanga ili kila wakati wafaidike na pesa za serikali kupitia halmashauri. Wanachopanga sasa hivi ni kujihakikishia nani awe Diwani, nani awe mbunge na ktk hao nani ateuliwe kuwa M/kiti wa halmashauri. Wazoefu ktk uchaguzi wametoa pesa kwa weneyviti na makatibu wao ili kuwalainisha na kuwasaidia kuwaelekeza hawa tunaowaita ’wajumbe.’

Kutokana na mpangilio huo, Viongozi wa CCM wanajihakikishia njia ya kupata pesa za halmashauri. Hii ni moja ya mbinu ambayo imewasambaratisha wagombea ambao huenda wana mipango na malengo mazuri ya majimbo yao. Hawatakiwi! Kwa haraka utaona kama ni tatizo la CCM lakini ni tatizo kwa wananchi wote wa nchi hii. Je, rais au Mkiti wa CCM analifahamu hili. Je anaamini atawasimamia? Sisi tunataka mfumo na siyo kusimamiwa kwa vitisho. Kwa mtindo huu, hatutapata mfumo.

Bahati mbaya Ni kwamba hata Mwenyekiti wa chama ameotia huko huko, anajuwa kuwa alikuwa anatumia njia gani ili kupita kwenye Kura za maoni. Kwa hiyo msitegemee jipya. Aliyepata Kura nyingi ndo anayeensa kuwa mgombea.
 
cariha

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
14,094
2,000
Kwa kweli ni Kinara kama ameweza kutoa million zote hizo

Watoto wa maskini hawezi kuonga na wengi ndio wanakua wana qualifications zote za kushinda tatizo pesa
Wengi waliopata kura chache ni wale ambao hawakuhonga I wish hii tabia ikomeshwe Mara moja bila hivo maskini watabaki watawaliwa tu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom