Elections 2010 Taarifa na takwimu uchaguzi wa Tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,855
34,312
Watanzania walipiga kura tarehe 31 Oktoba 2010. Uchaguzi huo ulikuwa muhimu kwa nchi hiyo hasa kwa kuwa chama tawala hakijawahi kutolewa madarakani tangu ilipopata uhuru mwaka 1961. Yafuatayo ni baadhi ya maswala muhimu yanayohusu uchaguzi wa Tanzania 2010.


Tanzania ina idadi kubwa kiasi gani ya wakazi?
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia takwimu za mwaka 2008, Tanzania ina wakazi wapatao milioni 42. Umoja wa Mataifa ulikadiria mwaka 2009 kuwa Tanzania ilikuwa na wakazi milioni 43.7.
Watu wangapi walijiandikisha kupiga kura?
Tume ya uchaguzi ya Tanzania ilitangaza kuwa watu waliojiandikisha kupiga kura ni milioni 19, lakini waliojitokeza kupiga kura walikuwa takriban milioni nane au asilimia 42.
Je watanzania walipiga kura siku gani?
Siku ya kupiga kura ilikuwa tarehe 31 Oktoba 2010
Kampeni zilianza lini?
Kampeni za uchaguzi wa Tanzania zilianza Agosti 31, na kumalizika tarehe 30 Oktoba 2010.
Kuna wagombea wangapi wa kiti cha Rais?
Kwa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulikuwa na wagombea saba, vile vile katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar kulikuwa na wagombea saba pia.
Tanzania ina majimbo mangapi ya uchaguzi?
Kwa Tanzania na Bara na Zanziba kuna jumla ya majimbo ya ubunge 239
Je Rais na wabunge hukaa madarakani kwa miaka mingapi?
Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Rais huchaguliwa na kuwepo madarakani kwa muda wa miaka mitano kabla ya uchaguzi mwingine kufanyika. Sheria hiyo hutumika kwa wabunge na madiwani.
Jina kamili ni nini?
Nchi hii hutambulika kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa shughuli rasmi.
Je Tanzania ukubwa wa nchi kiasi gani?
Tanzania ina ukubwa wa kilometa za mraba 945,087.
Lugha Rasmi ni zipi?
Lugha zinazotumika kwa shughuli rasmi ni Kiingereza na Kiswahili.
Dini kubwa ni zipi?
Ingawa kuna dini nyingine ndogo ndogo, idadi kubwa ya watanzania ni wakristu na waislamu.

Chanzo: BBC Swahili - Habari - Taarifa na takwimu uchaguzi wa Tanzania
 
Back
Top Bottom