Taarifa: Mwongozo wa Utoaji Mikopo ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF)

SongambeleEN

Member
Mar 23, 2013
25
12
Ndugu wanajamvi,

Kwa wale wanaopenda kufuatilia shughuli za Bungeni watakuwa wameshamsikia Mh. Waziri Gaudensia Kabaka akitangaza juu ya jitihada za Serikali kuzalisha ajira laki sita, hususani kupitia miradi ya vijana ambao watapatiwa mikopo ili kukidhi mahitaji ya miradi yao. Jambo hili pia lilijadiliwa humu kupitia thread hii, Ajira laki sita kwa vijana zina maanisha kujiajiri vijana kaeni tayari kwa fursa hii

Kwa kutambua information gap iliyopo baina ya vijana na Wizara, Taasisi yetu iliamua kufuatilia suala hili ili vijana wengi wenye nia na malengo ya kujiajiri waweze kutumia fursa hii kutimiza malengo yao na kushiriki kikamilifu katika Uchumi wa nchi yao. Pamoja na jitihada nyingine, ajira hizi zinategemewa kuzalishwa kwa kutumia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF) unaosimamiwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Mfuko huu ulianzishwa mwaka 1993, chini ya kifungu namba 17(1) cha The Exchequer and Audit Ordinance (Cap 439) No 21 of 1961, lengo likiwa ni kuwasaidia vijana ili wapate mikopo yenye masharti nafuu. Kutokana na mapungufu yaliyokuwa yamejitokeza awali, na ili kuufanya mfuko huu uwe endelevu, Serikali imeamua kuanzisha utaratibu mpya ambao umeanza kutumika rasmi mwezi Aprili, mwaka 2013. Masharti hayo mapya yanapatikana katika nyaraka tulizoambatanisha.

Walengwa
Vijana wenye umri kati ya miaka 15-35

Riba
Asilimia kumi kwa mwaka (10%)

Mikopo itatolewa kupitia Saccos za Vijana. Kwa Maelezo zaidi pitia nyaraka hizo ambazo tumeambatanisha.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    86.4 KB · Views: 911
  • image.jpg
    image.jpg
    374.4 KB · Views: 922
  • image.jpg
    image.jpg
    141.4 KB · Views: 822
  • image.jpg
    image.jpg
    133.4 KB · Views: 747
  • image.jpg
    image.jpg
    145.3 KB · Views: 659
  • image.jpg
    image.jpg
    223 KB · Views: 647
Mikopo hii, ni tofauti na mikopo mingine kutoka kwenye mabenki ya kibiashara kwani haihitaji Dhamana, kitu ambacho kimekuwa kikiwakwamisha vijana wengi wanaotaka kuanzisha miradi mipya.
 
kikundi cha wati wangapi kinatakiwa? uhusiano na saccos inakuaje hapo?

hata mimi sijaelewa hapo, na SACCOS zitachaguliwa chache, so kuna vijana hawataweza kupata hata kama wana mawazo mazuri ya biashara
 
Back
Top Bottom