Taarifa muhimu toka kamati tendaji ya CUF kwa watu wote

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
TAARIFA KUHUSU KIKAO CHA KAMATI YA UTENDAJI YA TAIFA YA THE CIVIC UNITED FRONT(CUF - CHAMA CHA WANANCHI) KILICHOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU YA CUF ILIYOPO VUGA, ZANZIBAR TAREHE 2 FEBRUARI, 2017

Kamati ya Utendaji ya Taifa ya The Civic United front (CUF - Chama Cha Wananchi) imefanya kikao chake cha kawaida katika ofisi ndogo ya makao makuu iliyopo Vuga, mjini Zanzibar tarehe 2/2/2017. Kikao hicho kimeongozwa na Katibu Mkuu wa Chama, Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye kwa mujibu wa Katiba ya Chama ndiye Mwenyekiti wa kikao hicho.

Kikao kilihudhuriwa na wajumbe wote halali wa kikao hicho waliopaswa kuhudhuria isipokuwa Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Wanawake CUF (Taifa), Bi. Fatma Kalembo ambaye ni mgonjwa.

Kikao hicho kilipokea na kujadili kwa kina ajenda kadhaa ikiwa ni pamoja na kupitia na kuthibitisha mikhtasari ya vikao vilivyopita na yatokanayo na vikao hivyo, Taarifa ya wizi wa fedha za ruzuku ya Chama, Taarifa rasmi kuhusu uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar na Uchaguzi wa Madiwani katika Kata 20 za Tanzania Bara uliofanyika tarehe 22/2/2017, Taarifa ya hali ya kisiasa nchini, na ajenda kuhusu programu ya ujenzi na uimarishaji wa chama kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Baada ya mjadala wa kina wa ajenda hizo, Kamati ya Utendaji ya Taifa imefikia maamuzi yafuatayo;

1. Kuhusu wizi wa fedha za ruzuku ya Chama;

Kamati ya Utendaji ya Taifa imeipongeza Bodi ya Wadhamini ya The Civic United front (CUF - Chama Cha Wananchi) kwa hatua ilizozichukua kukabiliana na wizi huo uliofanywa kwa lengo la kukihujumu chama kwa mashirikiano kati ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, Benki ya NMB na mtu anayeitwa Ibrahim Lipumba na genge lake. Kamati ya Utendaji ya Taifa inaunga mkono maamuzi ya Bodi ya Wadhamini ya kuazimia kuchukua hatua za kisheria haraka na kuhakikisha kuwa wahusika wote wa wizi huo wanafikishwa katika vyombo vya sheria.

2. (a) Kuhusu Uchaguzi mdogo wa Ubunge wa Jimbo la Dimani Unguja, Zanzibar:

Kamati ya Utendaji ya Taifa inawapongeza na kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wa jimbo la Dimani, wanachama, na viongozi wa CUF wa ngazi mbalimbali kwa kujitolea kwa hali na mali kufanikisha kampeni za uchaguzi wa jimbo la Dimani kwa kiwango cha hali ya juu kulikowafanya CCM kukata tama. CCM walijua wamekataliwa na wananchi wa Dimani na kwa hivyo kuamua kutumia vyombo vya dola kulazimisha ushindi usiokuwepo. Kamati ya Utendaji ya Taifa inawataka wananchi na wanachama wote kutokata tamaa kwani CCM imejiaibisha yenyewe na kudhihirisha kwamba imepoteza mvuto na sasa haina uwezo wa kushinda uchaguzi wowote Zanzibar bila ya kutumia nguvu za vyombo vya dola. Hali ilivyokuwa Dimani imethibitisha tena maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 ambapo walikigaragaza vibaya Chama cha Mapinduzi(CCM) hadi wakaona hawana njia zaidi ya kuufuta uchaguzi kwa njia za haramu zisizokubalika na wala kuwa na nguvu za kikatiba na Sheria.

Kamati ya Utendaji ya Taifa inawapongeza na kuwashukuru viongozi wote wa vyama rafiki katika UKAWA wakiwemo Mheshimiwa Edward Lowassa (Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA na Waziri Mkuu mstaafu), Mheshimiwa Salum Mwalimu (Naibu Katibu mkuu Chadema - Zanzibar), Mheshimiwa Tundu Lissu, (MB), Mheshimiwa Said Kubenea (MB), Mheshimiwa Janet Fussi, Mheshimiwa Kombo Hamad (NCCR) na viongozi wa vyama vyengine kwa ushirikiano wao katika uchaguzi huu na kushiriki moja kwa moja katika mikutano ya kampeni na mashauriano mbalimbali kufanikisha ushindi wa CUF na wananchi wa Jimbo la Dimani katika uchaguzi huu. Tunapenda kuwahakikishia kuwa CUF, ikiwa ni Taasisi makini na imara, itaendeleza ushirikano huu na kamwe haitayumbishwa na vibaraka wachache wanaotumiwa na Serikali ya CCM kuvunja umoja wa vyama vyetu ambao umekuwa na manufaa makubwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na ni tishio kwa uhai wa CCM kuendelea kuiongoza Tanzania.

2. (b) kuhusu Uchaguzi wa Kata 20 za Tanzania Bara uliofanyika tarehe 22/1/2017;

Wananchi wameonyesha wazi wazi kuwa wameichoka CCM ambapo mbali na kushinda kata nyingi, idadi ya kura za wapinzani zimeongezeka kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kwa upande wa CCM kura zimeshuka sana. Hii ni dalili tosha kuwa Watanzania wamechoshwa na CCM na sera zao za kitapeli na zisizotekelezeka. Aidha, uchaguzi umejidhihirisha wazi kuwa vyama vya upinzani makini vina kila sababu ya kuunganisha nguvu ya pamoja ili kuishinda CCM na kuhakikisha kuwa kwa pamoja tunapambana na vibaraka wanaotumiwa na serikali ya CCM kutaka kujinufaisha binafsi na kuacha lengo kuu lenye maslahi mapana ya kufanya MABADILIKO makubwa ya mifumo ya uendeshaji nchi kwa manufaa ya watanzania wote.

3. Kuhusu Taarifa ya Hali ya Kisiasa nchini;

(a) Kamati ya Utendaji ya Taifa imesikitishwa na hali ya kuyumbishwa kwa uchumi wa nchi kunakofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano na kusababisha hali mbaya ya maisha kwa Watanzania kwa kusitisha ajira, kuvuruga mfumo wa biashara na wafanyabiashara, thamani ya dola kupanda na shilingi kuporomoka, kutokuheshimiwa kwa misingi ya demokrasia na chaguzi huru na haki kulikopelekea nchi nyingi za washirika wa maendeleo (wahisani) kusitisha kutoa fedha za kusaidia miradi ya maendeleo katika bajeti kuu ya serikali, kauli za dharau na kejeli zilizotolewa na Rais Magufuli kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera na kitendo cha Serikali ya CCM kuzitumia fedha za rambirambi zilizotolewa na Watanzania na nchi marafiki kinyume na matarajio na namna ilivyokusudiwa.

(b) Kitendo cha Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Magufuli kuhujumu vyama vya upinzani kufanya shughuli zake za kisiasa kwa mujibu wa Katiba za nchi na sheria ya vyama vya siasa nchini, kuwafunga jela wawakilishi wa wananchi kwa hila na njama za kutaka kudhoofisha wapinzani akiwemo Mbunge wa Kilombero, Mheshimiwa Peter Lijualikali, pamoja na kumnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mheshimiwa Godbless Lema kwa mashtaka yanayodhaminika kisheria, ukiukwaji wa haki za binaadamu na uminywaji wa haki za kidemokrasia nchini ni jambo linalohitaji kupingwa na kila mpenda amani na maendeleo ya nchi yetu.

4. Kuhusu programmu ya ujenzi na uimarishaji wa chama Tanzania Bara na Zanzibar:

Katika hatua na mikakati ya kuimarisha Chama, Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Taifa kimeandaa programu ya ujenzi na uimarishaji wa Chama kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar. Kamati inawaomba Watanzania kuendelea kukiunga mkono chama cha CUF kukabiliana na changamato zilizopandikizwa kwa lengo la kuhujumu juhudi za ukombozi wa nchi yetu kisiasa, kiuchumi, na kijamii. Kamati inawataka wananchi, wanachama na viongozi wa CUF kushiriki kwa upana katika program hizo za chama ili kuendelea kupata elimu muhimu ya haki za msingi za kila mwananchi na kuhamasika kudai haki sawa kwa wananchi wote ikiwemo madai ya kupata Tume Huru za Uchaguzi nchini kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

MWISHO:

The Civic United Front (CUF - Chama Cha Wananchi) na viongozi wake kinawahakikishia Watanzania wote kuwa kitaendelea kusimamia maslahi mapana ya Taifa letu na kushinda changamoto za kupandikizwa zenye lengo la kutaka kukihujumu Chama na mfumo wa demokrasia nchini. Kamati ya Utendaji ya Taifa inawahakikishia wanachama na Watanzania wote kuwa CUF ni taasisi yenye viongozi imara na makini, tunajua na ndivyo ilivyo kuwa hakika itashinda mapambano haya ya ndani na nje ya Chama na itaibuka ikiwa CUF imara zaidi na CUF yenye nguvu zaidi.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa na:

Kamati ya Utendaji ya Taifa
The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi)

Joran Lwehabura Bashange
K/Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara
na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi CUF-Taifa
Tarehe 3 Februari, 2017
 
Mkubali mkatae NCHI HII HAKUNA UPINZANI TENA.......haiwezekani miaka nenda rudi VIONGOZI WA UPINZANI NI WALE WALE na hii ndio inayopekea mpaka UPINZANI UNAPOTEA NCHI HII kwanini ninasema hivi....
ninasema hivi nikiwa na maana ya kwamba hakuna kitu muhimu sana katika maendeleo kama kuruhusu FIKRA MPYA NA MAWAZO MAPYA kutoka kwa watu wengne hapa namaanisha HIVI VYAMA PINZANI VIONGOZI WAO WOTE WALIOPO WAKUBALI KUWAJIBIKA KWA KUACHIA Mdaraka na kuruhusu WATU WENGNE WAONGOZE na ndicho tunachokiona kwa CCM sasa.....IMEKUJA SAFU MPYA KABSA ambayo mpaka imepelekea UPINZANI KUFA na kuonekana kama MATAPELI FULANI na CCM kuonekana kama ndio mkombozi wao..........Chaguzi ndogo zilizofanyika ni kipimo tosha kabsa kuthibitisha hili NA WAPINZANI WANABAKI WANA LIA LIA ETI CCM inatumia DOLA.....sasa kama inatumia dola kwanini mnaendelea kushiriki hizi CHAGUZI na mnatumia kodi za watanzania kwenye CHAGUZI ambazo mnajua kabsa mwisho wa siku CCM itarumia DOLA na kushinda????
\hivi tukisema nyie ni majizi mnatumia kodi zetu kupitia RUZUKU sivyo ndivyo tutakuwa tumekosea????
Na itakuwa vipi kama tukisema MNAJUA KABSA HAMNA TENA MVUTO kwa wananchi kwa sasa na mnabaki mnasingizia DOLA kama DEFENCE MECHANISM ya kuendelea KUWA MAJIZI YA ruzuku yetu?????
 
Eti anawapongeza akina EL, CUF mmejimaliza. Mnaopenda mabadiliko anzisheni chama kipya vilivyopo vimeshindwa
 
Kipengele cha 2a kinathibitisha Tanzania hakuna upinzani, wanachama, wapenzi na mashabiki wa upinzani wanapoteza mda.

Yaani wamejadili matokeo ya uchaguzi wa Dimani ambao walishinda(kwa maelezo yao) ila CCM ikatumia vyombo vya dola kuwapoka ushindi, wakaishia hapo na kupongeza akina Lowasa, Lissu n.k. kwa kushiriki kwenye kampeni, kweli?
Mnawakatisha tamaa watu wanaowaamini.
 
Leo CUF wanatoa tamko linalo msema mwenyekiti wao wa muda mrefu kwa lugha ya "mtu anaeitwa ..... Lipumba na genge lake"!!. Siamini kama lugha hii inatoka kwenye chama kikongwe kama CUF.
 
Mkubali mkatae NCHI HII HAKUNA UPINZANI TENA.......haiwezekani miaka nenda rudi VIONGOZI WA UPINZANI NI WALE WALE na hii ndio inayopekea mpaka UPINZANI UNAPOTEA NCHI HII kwanini ninasema hivi....
ninasema hivi nikiwa na maana ya kwamba hakuna kitu muhimu sana katika maendeleo kama kuruhusu FIKRA MPYA NA MAWAZO MAPYA kutoka kwa watu wengne hapa namaanisha HIVI VYAMA PINZANI VIONGOZI WAO WOTE WALIOPO WAKUBALI KUWAJIBIKA KWA KUACHIA Mdaraka na kuruhusu WATU WENGNE WAONGOZE na ndicho tunachokiona kwa CCM sasa.....IMEKUJA SAFU MPYA KABSA ambayo mpaka imepelekea UPINZANI KUFA na kuonekana kama MATAPELI FULANI na CCM kuonekana kama ndio mkombozi wao..........Chaguzi ndogo zilizofanyika ni kipimo tosha kabsa kuthibitisha hili NA WAPINZANI WANABAKI WANA LIA LIA ETI CCM inatumia DOLA.....sasa kama inatumia dola kwanini mnaendelea kushiriki hizi CHAGUZI na mnatumia kodi za watanzania kwenye CHAGUZI ambazo mnajua kabsa mwisho wa siku CCM itarumia DOLA na kushinda????
\hivi tukisema nyie ni majizi mnatumia kodi zetu kupitia RUZUKU sivyo ndivyo tutakuwa tumekosea????
Na itakuwa vipi kama tukisema MNAJUA KABSA HAMNA TENA MVUTO kwa wananchi kwa sasa na mnabaki mnasingizia DOLA kama DEFENCE MECHANISM ya kuendelea KUWA MAJIZI YA ruzuku yetu?????
Daaah! Haya mkuu
 
Stupid reasoning capacity

Whoever has ideas that differ from yours he has stupid reasoning capacity. You are ready to change your words each minute according to the environment and expect others to trust you.
 
Whoever has ideas that differ from yours he has stupid reasoning capacity. You are ready to change your words each minute according to the environment and expect others to trust you.
Kindly help me in this!Party chairman resigned at his own will plus the fact that party elites and clerics asked him not to resign for the betterment of the party! he didn't allow even to listen to them went ahead voluntary resigning , he resigned now after one good year out of office came back and a null his resignation,please just help even with only one example any leader or any other of this kind who decided to go back to his position after one year of voluntary resignation! Shall salute you if you can mention one
 
Hivi Hawa CUF ya Seif Wana akili kweli?
Unaibiwaje Fedha ambazo hamjawahi kuzipokea?

Wao walipaswa kuilalamikia Serikali kwa kutowapa Ruzuku sio kuibiwa Ruzuku!

Huwezi kuibiwa kitu ambacho hukimiliki!

Wao Kama hawamtambui Lipumba na Lipumba ndio kaingiziwa Fedha walitakiwa waikabe Koo Serikali kwa kutowapa Fedha watu wanaostahiki lakin wakisema Wameibiwa maana yake walishamilikishwa tayari
 
Wanaoelewa zaidi kama babu Duni walikimbia zamani sana katika siasa za kudanganyana.

Matamko kama haya hayatakiwi yawafikie watu wanaoelewa zaidi ya vikao vyao vya kula hela.

Hakuna mantiki wala uwezo wa kushawishi wanaojua kuwa CUF imekufa kifo cha mende, chali, mbendembende!!!
 
Back
Top Bottom