Taarifa muhimu kwa wateja wote wa ma bank nchini

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
8,314
13,277
kufuatia hatua ya serikali ya kutunga sheria ya kuzuia utakasaji fedha ya mwaka 2006,benki zinawajibika kisheria kudai na kuhifadhi rekodi na taarifa kamili za wateja wao.hivyo mnatakiwa kwenda ktk mabenki kuboresha taarifa zenu kabla ya tarehe 1 march,japo kuna ma benki mengine hadi tarehe 16 march,ukishindwa kwenda akaunti yako itafungwa.yote hiyo ina lengo la kutimiza kanuni isemayo"mfahamu mteja wako"(KYC).unakwenda na kitambulisho chochote kile.kazi kwenu wadau usije ukaenda kuchomoa vijisenti una ambiwa a/c imefungwa itakuwa balaa.
 
Inakuwaje kama nilifugua akaunti yangu Mbeya na sasahivi naishi Mtwara, na sina uwezo wa kwenda Mb kwa haraka hivyo?
 
Eti kuanzia Mwezi ujao hata Na kwenye $ huwezi kumuandikia mtu cheki ya kiasi kinachozidi $10,000, itabidi ufanye Telegraphic Transfer kama ilivyo sasa kwa Tzs.
Huu ni wizi wa kimacho macho, mkimlipa mtu kwa cheki mitachajia Tzs 300/= kama Cheque Withdraw Fees, but nkitumia Telegraphic transfer ntakatwa Tzs 10,000/- nzima kama chaji.
 
Mbona Bank zetu hawajatutangazia? Au wewe una bank ya Mpesa.

Hilo tangazo nimeliona leo makao makuu ya NBC limebandikwa kwenye mlango wa kuingilia...nadhani hata mabenki mengine yatakuwepo so,ni bora ukaenda kucheck kwenye benki zenu.
 
know your customer inatakiwa ifanyike toka mteja anafungua akaunti. Kwa benki makini, inapaswa kujua mzunguko wa kawaida wa fedha wa wateja wao.
Kiasi kwamba ukiweka pesa kuliko kawaida iwa-alert.

Pia wanapaswz kuwa na anti money laundrng form. Mfano anapodeposit kuzid mil 5 mteja anapaswa ajaze fomu, na hapo inakuwa rahisi kuwajua wateja wenye deposits kubwa, benki inaweza kuwatembelea sehemu zao za kazo/biashara, hii inasaidia hata kwenye kukopesha au kumfanya mteja kuhisi kuthaminiwa.

Ila itakapofika tar 1/3/12 wateja wanajaza fomu, then what next? Unapata uhakika gani kuwa maelezo ya mteja ni sahihi? Maana kuna watu kujilipua kwenye mabenki kwao kawaida!!!
 
c lazima uende kwenye domicile branch,nenda tawi lolote la bank yako lililokaribu nawe.

Watu wa mabenk ni wasumbufu na very arogant.mimi nilijaza hizo 4m tangu jan 11. NBC industrial branch, branch yangu niliko fungulia ni Dodoma, tangu hapo nikaambiwa wataituma na ikikamilika nitapewa taarifa. Mimi nikasafiri nikaenda mkoa mwingine ambapo ndipo office yangu ilipo. Nao wakakaa kimya. Nimepata nafasi nimekuja kufuatiliaa yaani alhamisi nimeshinda pale kuanzia asubuhi mpaka wanafumga, hakunakitu, njoo kesho mpaka leo hamna kitu.
I hate this habit of lazyness n iresponsibility.
 
Waache wafunge tuu hizo account tuone nani atapata hasara. Hawa kama wanataka lazimisha mambo namna hiyo wanataka tuu kuharibu uchumi wa nchi. Wawabane wanaokopa kwanza kwa ambao hawana madeni nao hakuna haja ya kuwa na haraka za namna hiyo.
Wakifanya ujinga watu watatumia zaidi Mpesa za nyingineza na mapato yao yatashuka sana...

Hii ni akili ndogo ya madhara yatakayopatina kwa kulazimisha mambo haraka haraka.
 
Taarifa yako ni ya msingi, ila its not official. na hilo ni Jambo ambalo haliwezekani. kwani wewe umepata wapi izi taarifa? its too hanging.
 
Back
Top Bottom