Taarifa muhimu kwa waliokata tiketi za kufanya Umrah Ramadhan huko Makkah.

Sideeq

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
2,422
433
Kuanzia Shaaban mosi (jana) wizara ya Hajj imeamua kuwa viza zote zitakazotolewa kuanzia Shaaban zitakuwa na validity ya siku 14 tu na si zaidi ya hapo.

Hii ni kupunguza msongamano utakaosababishwa na upanuzi wa eneo la Mataaf ambao umeziacha hoteli nyingi zikivunjwa

Kwa wale walio- book tiketi za Ramadhani nzima hakikisha unabadilisha tiketi mapema au kama ina refund chukua uanze upya kwa sababu hakuna shirika la ndege litakaloruhusu mwenye kufanya Umrah apande ndege akiwa na tiketi inayozidi ukaazi wa zaidi ya siku 14, hii ni kutokana na maagizo waliyopewa na authorities vinginevyo watakabiliwa na faini kubwa.

Muelekeo upya wa kupata viza unaonekana namna hii: ukisharuhusiwa kupewa viza basi pasi itagongwa muhuri wa viza ndani ya siku 14 (hii ni kazi ya ubalozi), mwenye kufanya Umrah akishakugongewa viza inabidi asafiri ndani ya siku 14, akifika makkah anatakiwa atoke ndani ya siku 14 hivyo kanuni hii inajulikana kama 14-14-14.

...zaidi wasiliana na wakala wako.
 
Back
Top Bottom