Taarifa Muhimu kutoka TARURA, Ulipaji wa ada za maegesho kidigitali

kunena

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
506
711
TARURA inawafahamisha wananchi wote kuwa maegesho yaliyo katika hifadhi za barabara yanatozwa ada ya maegesho, hivyo ni wajibu wa mtumiaji wa maegesho kuhakikisha analipa ada ya maegesho mara atumiapo maegesho hayo.

Mwananchi unashauriwa kuangalia kama unadaiwa ada ya maegesho kupitia “App” ya “GePG” na “TeRMIS” ambazo unaweza kupakua kupitia “Play Store” au kupitia tovuti ya “www.termis.tarura.go.tz” kwa kuweka namba ya usajili wa chombo cha moto ili kufahamu kiasi unachotakiwa kulipa baada ya kutumia maegesho au piga *152*00#, bonyeza 4 (Nishati, madini na usafiri) 2 (TARURA), 2 (Angalia deni TeRMIS) weka namba ya chombo cha moto kisha utapata ujumbe mfupi wenye deni na kumbukumbu namba ya kulipia.

Kumekuwa na changamoto kadhaa kutokana na upya wa mfumo huu ambao TARURA tunaamini kadri ya muda unavyosonga mbele watumiaji wa maegesho yaliyo katika hifadhi ya barabara watauelewa maana ni mfumo rafiki na wa uhakika.

TARURA tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya Habari,
tunapenda kuwajulisha wananchi kuwa hakuna wizi wowote unaofanywa UNAPOTOZA ada ya maegesho kwa njia ya kidigitali kwani fedha hiyo inapelekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya serikali kupitia GePG.

Wala hakuna anayetozwa ada ya maegesho nje ya maegesho halali ndani ya hifadhi ya barabara kwani mfumo wa sasa una taarifa zote za magari yanayotumia maegesho ndani ya hifadhi ya barabara na unaweza kupata taarifa hizo kwa kujaza fomu maalum ya kuomba taarifa hizo kwa kufika katika ofisi ya TARURA iliyokaribu nawe.

TARURA inatambua taarifa za watumiaji wa maegesho kuwa ni SIRI na BINAFSI hivyo hatujaweka kipengele cha eneo (location) kwenye ankara kwa sababu za kiusalama kwani si kila mtumiaji wa chombo cha moto angependa taarifa za eneo alilokuwepo kujulikana. Mwenye mahitaji ya taarifa za aina hii atatakiwa kufuata utaratibu ulioelekezwa hapo juu.

Mwananchi unapaswa kufahamu kuwa ni wajibu wako kulipa ada ya maegesho mara utumiapo maegesho, TARURA itaendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali ili kuhakikisha elimu ya utaratibu wa malipo kidigitali inafikia idadi kubwa ya wananchi na kuwawezesha kufanya malipo ya ada za maegesho kiurahisi kupitia mitandao ya simu na benki.

LIPA ADA YA MAEGESHO KWA AJILI YA MABORESHO YA BARABARA ZETU
 
mtatukamua hadi kodi za kutema mate kwenye hifadhi za barabara

Mi nashangaa watu wako kimya wakati miaka mitano tulikuwa tunajinasibu kuwa tumetekeleza inamaana ule utekelezaji ulikuwa wakuuzamisha kabisa Uchumi kiasi kwamba sasa tunategemea kodi za uzalendo na parking kweli hii nchi tuliyoambiwa ni dona kantri.
 
Nyambafu niliwekewa risiti maeneo ya kariakoo maandishi yamepauka balaa namba hazisomeki.mpaka mwanangu wa darasa la tano alipofanikiwa kunisomea na kufanikiwa kulipa.hakikisheni mashine zenu zinaprit vizuri ndo mtoe risiti

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom