Taarifa muhimu kinachojiri kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge Bunda Mjini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
TAARIFA MHIMU KINACHOJIRI KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE BUNDA MJINI

Kutoka mahakamani baada ya wakili msomi na mwanasheria Mkuu wa Chadema Mh.Tundu Lissu kumhoji Shahidi wa PILI kuhusu malalamiko yao juu ya makosa yaliyojitokeza katika uchaguzi mkuu 25 oct 2015.

Leo upande wa Mawakili Wa Serikali wawili (second respondent and Third respondent) kama watetezi wa serikali(Mkurugenzi) wamemhoji shahidi huyo na kujiridhisha,kidogo nitoe Briefly explanation kilicholeta utata.......

Nikwamba baada ya Mawakili wa serikali kumhoji ndugu shahidi kuhusu idadi ya matokeo waliyoyapata kutoka kwenye vituo 190.Swali lilikuwa je mlipata taarifa ya matokeo kutoka kwenye idadi ya vituo vingapi?

Shahidi alizunguka sana,kukwepa swali wakili akaomba Mh.jaji amuamuru shahidi kujibu swali na ndipo shahidi alijibu kuwa walipata matokeo kutoka vituo vyote 190.

Wakili alimuuliza kwa kumkumbusha kuwa jana shahidi wa KWANZA alipoulizwa swali hili hili na Wakili msomi Tundu Lissu alijibu kuwa walipata matokeo kutoka kwenye vituo 199.sasa swali je kati ya Shahidi wa KWANZA na wewe(WAPILI) nani muongo? au nani ameidanganya mahakama?

Shahidi(WAPILI) alijibu kuwa yeye alivyopata na mimi nilivyopata taarifa hiyo ni tofauti kwani tuko vyama tofauti yeye ni (DP na mimi ni CCM).

Wakili wa serikari akauliza kwa hiyo mnamaanisha kuwa kiapo chenu ni batili kwani kiapo chenu kinaonesha maombi yenu ni mamoja,na shahidi wa KWANZA hakuleta maombi mapya sasa unaposema eti yeye (shahidi wa kwanza) alijibu kwa kuwa yeye ni DP na wewe ulijibu kwakuwa wewe ni CCM kwa lugha lahisi mnamaanisha kwamba mnakisaliti kiapo chenu?

Shahidi HAPANA hatukisaliti Mh.Jaji.

Wasikilizaji (Laughing) Wakacheka kwa pamoja (kwamshangao)

Wakili wa serikali akaomba ruhusa kwa Jaji akaketi kwenye kiti.

Baadaye mawakili wake(Wakili Wa Mashahidi) wakasimama wakamuuliza (SHAHIDI)maswali machache kama kumbrashi-brashi lakini hoja zao hazikuwa za mashiko Sana kwa sababu Tundu lissu wakili msomi alikuwa amemuhoji jana kwa vifungu halali vya sheria hivyo mawakili wa upande wa WASIRA walikubaliana na Tundu Lissu..

Whistle.......Lissu anawanong'oneza na mawakili wa MASHAHIDI halafu wanacheka huku wakitingisha vichwa ishara ya ukubali wa hoja zake.

Mh.Jaji amesitisha mpaka Siku ya kazi tarehe 10 Mwezi Huu (wa kumi) mwaka 2016.
 
Mzee tangu enzi za Nyerere Upo, enzi za Mwinyi upo, enzi za nkapa upo, za kikwete upo bado unataka na za JPM.... hapana kapumzike mzee wetu.... inatosha.... umekula vya kutosha... kwa hali hii vijana sio taifa la leo wala kesho wala kesho kutwa.... unataka vijana wawe taifa la lini?
 
Mzee anataka kurudi kwenye Halmashauri ya Bunda kuzipa ufisadi wa mradi wa Maji.Ule mradi wa Maji wa Bunda mwaka 2015 walimpeleka Mizengo Pinda na Prof Maghembe akiwa Waziri wa Maji,kufika pale wakaahidi kuwa ndani ya week mbili maji yatakuwa yanamwagika Bunda Mjini na vitongoji vyake.

Ni mradi wa mabilioni ya shilingi,lkn tender ya mradi ule alipewa Mtoto wa Mzee Wassira anaitwa Kambalage Steven Wassira,mpaka leo hajaleta maji na mradi ulishamalizika.Maji Bunda mjini hakuna sbb walikomba pesa za mradi ili wafanyie kampeni.Nguvu zote hizi za kuweka kesi,ni kupoteza watu maboya ili muda uishe.

Mzee pumzika,inatosha sasa Ubunge,kama Maji Bunda mradi umedoda,Unataka kurudi kufanya nini??Toke enzi za Nyerere mpaka sasa bado tu hujapata mtaji?
 
tuhuma hizi lazima zimudedishe aisee
 
Wasira ni msomi na mkweli,hawezi fanya kazi na JPM.
Aachane na hiyo mambo bila kujali kuwa atashindwa au kushinda kesi
 
Bora kaenda tundu lissu,mawakili wa mwanza wengi hawana weledi,ona kamanda mwalimu naibu katibu mkuu alivyosota rumande simiyu,

kuna haja kwa mawakili wa mwanza.kuonyesha uwepo wao kwenye fani ya sheria,wapowapo tu.kama dona la jela.

mikoa.hiyo inaongoza kwa mambo mengi ya hovyo,lakini hatuwasikii wakifanya public interest litigation,wamezoea kesi za mihogo tu
 
Wasira ni msomi na mkweli,hawezi fanya kazi na JPM.
Aachane na hiyo mambo bila kujali kuwa atashindwa au kushinda kesi
mbona mtukufu anasema yeye ni msema kweli mpenzi wa mungu,na anatoa moyoni kule kwenye pistoni zinazosukuma damu(sijui kama tunafikiri roka.moyoni au kichwani)
 
Wassira angerudi tuu Bunda na kushirikiana na Bulaya ambaye ni kijana kuleta Maendeleo ingekuwa jambo la heshima sana.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa nn unamuita Wakili Msomi?Kwani mtu anapata hadi leseni ya kufanya kazi ya uwakili asiwe msomi?
Kuna wakili sio msomi?
 
Back
Top Bottom