Taarifa mheshimiwa Spika

Nondoh

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
298
478
Kwanza kabisa napenda kusema Mimi sio mfuatiliaji Sana wa Bunge, lakini Mara chache nilizopata kufuatilia nimejifunza machache likiwemo suala la utoaji taarifa hasa pale mbunge/waziri/spika anapoona mtoa mada anapotosha jamii. Huomba kitu cha spika kumkatisha mtoa mada Na kutoa ufafanuzi juu ya ukweli Ili kuepuka upotoshaji...

Ikumbukwe suala la Tundu Lissu kutibiwa mheshimiwa Spika Job Ndugai alilitolea ufafanizi baada ya clip ya Mbunge Godbless Lema kuzagaa ikituhumu Lissu kutopatiwa msaada.

Mh. Spika akiongea kwa hisia kali alilitolea ufafanuzi Na kudai wabunge, yeye, mawaziri Na viongozi WA serikali wanatibiwa humu humu nchini Na referral ikitolewa Muhimbili basi Ni India Hospital ya Apolo ambayo alikiri serikali kuwa Na mkataba nayo.

Siku ambayo mh. Spika Ndugai anatolea ufafanuni waziri WA Afya alikuwepo bungeni Na aliyasikia yote, hakunyoosha mkono wala kuomba kitu cha spika atolee ufafanuzi kuhusu matibabu ya Wahe. akiwemo Lissu, kwa tafsiri hiyo alikubaliana Na mh. Spika, Na Hilo tukaamini ndio tamko la serikali Na inapaswa kuwa hivyo.

Leo mh. Ummy Mwalim waziri WA afya ametolea maelezo tofauti Na ya spika aliyotoa. Baada ya kuisikiliza clip nimejiuliza maswali mengi Sana bila kupata majibu. Sijui tumuelewe yupi Spika au W/afya

Je kwanini hakutoa ufafanuzi tangu siku ya kwanza hadi hali ya hewa kuwa worse ndio atoe ufafanuzi?

Au ndio matokeo ya barua ya Jana kutoka Chama cha wanasheria WA England/Wales imechafua hali ya hewa

Ufafanuzi unahitajika nani yupo sahihi? Kama spika alikuwa sahihi kwa nini w/afya anakiuka taratibu? Kama spika hakuwa sahihi kwanini w/afya alimwacha spika aendelee kupotosha taifa?

Clips:
Waziri wa Afya:

Spika Ndugai:
 
Back
Top Bottom