Taarifa: Makamu wa rais, Dkt Mpango akimpa Pole Mkurugenzi Mkuu wa Usalama Aliyefiwa na Kaka Yake

UJUMBE KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN, SERIKALI, JESHI LA POLISI, VYAMA VYA CCM, CHADEMA, ACT, CUF, NA VINGINEVYO.

Sisi viongozi wa kiroho kutoka madhehebu yote ya dini nchini tupatao 24,000 kutoka Wilaya na Mikoa yote ya Tanzania chini ya Kamati yetu ya Kitaifa ya pamoja kwa Maaskofu na Mashehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, wawakilishi wao tunakutana leo kwenye Kongamano la Dua Kijiji cha Bagamoyo, kilichopo Madale, Dar es Salaam kwa ajili ya Dua.

Pamoja na kazi yetu ya kufanya Dua ya kuiombea nchi yetu na Taifa letu, wajibu wetu pia ni kuonya, kukemea vitendo viovu, kutoa ushauri muhimu kama huu wa leo kwenu ninyi tuliowataja hapo juu. Kumbukeni kuwa mbele zake Mungu Mwenyezi, aliye Mungu wa wote wenye mwili, hakuna mkubwa wala mdogo, mwenye nguvu wala dhaifu, Rais wala Mjumbe wa Nyumba Kumi. Sisi sote tunamhitaji Mungu kwa ulinzi, afya na nguvu!

Hivi karibuni, tumeshuhudia mmomonyoko mkubwa wa maadili kwa viongozi wa Serikali unaokwenda sambamba na uporaji wa mali za umma, maneno ya vitisho yasiyozingatia Sheria, umri, maadili ya uongozi, na kiburi cha vyeo. Mbaya zaidi, mambo hayo yanaligawa Taifa kwa kasi kubwa. Aidha vitendo vya kutowasikiliza wenye nchi vimerudi kwa kasi pia. Watu wanapiga kelele kulalamikia tozo kubwa kwenye Gesi na simu lakini wananchi hawajasikilizwa. Wamesema kupanda kwa Gesi kunahatarisha misitu kutokana na matumizi makubwa ya mkaa. Hili limekuwa butu kujibiwa. Hii ni ishara mbaya. Kama mwenye nchi hasikilizwi, anasikilizwa nani?

Tumesikia kauli kali zinazochochea hasira upande wa pili. Kauli hizi zinatoka kwa IGP Simon Sirro kwamba viongozi wanasiasa [wa CHADEMA] na wanachama wao wasiende Mahakamani siku ambayo Mheshimiwa Mbowe atafikishwa Mahakamani. Hili ni moja ya mambo yanayodhihirisha mmomonyoko wa maadili ya weredi wa kazi.

IGP Simon Sirro ameingilia mhimili usio wake kwani Mahakama inao utaratibu mzuri wa kutafuta eneo kubwa ili wananchi wanaofika kusikiliza wapate nafasi hiyo. IGP Simon Sirro alipashwa kushauri kwa kusema; Ndugu zangu, tupo kwenye mazingira ya ugonjwa wa Corona, hivyo tunawaomba mchukue tahadhari kwa kwenda wachache Mahakamani huku mkiwa mmevaa barakoa, badala ya kutoa matamko ya kuwaua na kuwavunja miguu.

Tumbuke Wosia wa Mwalimu Nyerere usemao: 'Moyo kabla ya Silaha'. Vitedo vyote vinavyolalamikiwa na Watanzania kuhusu Jeshi la Polisi vinatokana na kukikuka Wosia wa Mwalimu Nyerere. Ushauri wetu kwa IGP Sirro ni kuwa alirudishe Jeshi la Polisi kwa Wananchi ili liwe ni Jeshi la kulinda raia na mali zao na siyo Jeshi la kuua raia wasio na hatia na kuvunja miguu yao. Kwa kuwa yeye ni Mkristo, atakuwa anajua kwamba Mungu Mwenyezi ni Mungu wa Haki. Tazama, wote washikao upanga wataangamia kwa upanga (Mathayo 26:52). Hata wale wanaowatuma wengine kutumia silaha, watambue kuwa ipo siku ya kesho. Tunatarajia kuwa ujumbe, ushauri na maonyo haya yatazingatiwa na wote tuliowataja hapo juu.

Tunaagiza kuwa Waraka huu usambazwe ili kila Mtanzania ausome kwa lengo la kulinda ustawi wa nchi yetu.

Ni sisi Viongozi wa Dini nchini Tanzania:
Askofu William Mwamalanga
Sheikh Alhaji Abubakar Muhidin Ramadhani
Sheikh Salleh Mussa
Askofu Aizeck Mgaya Kimweri
Padre Dr. Maxwell Furahisha
 
Rest well Bisward
Pole sana kwa familia na wote walioguswa na msiba
 
Back
Top Bottom