Taarifa kwa Watanzania waliopo Afrika Kusini

steve_shemej

JF-Expert Member
Nov 26, 2015
1,092
1,433
Kumekuwa na huu walaka unaosambaa raia wa SA wamepanga kuandamana siku ya Tare 29 mwezi huu

Wanaandamana kiss wageni na wametoa malalamiko yao kma unavyoona pichani ingawa watanzania hatujatajwa lakini tuwe makin

Kwakuwa itakuwa jumamos mjitahdi mkae majumbani jmaa wameomba kibari wamenyimwa ila wamepanga kuandamana hata bila kibari

So muwe makini
FB_IMG_15985552604770304.jpeg
 
Naona wengi tunachangia kwa hisia ila hili suala tuliangalie kwa pande mbili.


Je, sio sisi tuliowaunga mkono wanasiasa waliopiga kelele sualala makampuni ya wachina kuleta hadi wafagizi katika utawala wa JK?

WaSouth wanahaki kutetea nchi yao...ndiyo nitakubali ni wavivu.

Lakini hawa watu nchi yao ilishagawanwa. Walianza wazungu walichowabakizia sisi waafrika wenzao tumekimaliza.

Sema wanakosea saana namna ya kuwapinga whamiaji. Lakini, nayo serikali haina mikakati ya kueleweka ya kumaliza tatizo jambo ambalo hupelekea hawa jamaa kujichukulia hatua mikononi.
 
Tanzania walikua wanalia kwamba wakenya wanachukua ajira zao japo sidhani kama wanafika hata elf 50 hapo kwetu . South Africa ina wageni zaidi ya milioni 5 ambao wanagombania nao ajira,huduma za afya,elimu pamoja na makazi,.Hakuna nchi ya kiafrika inayo host wageni wengi kama hii na wana haki ya kulalamika kwani covid-19 imepoteza ajira za watu milioni 3 na zaidi.
 
SA ina watu wengi wasiohitajika uko. Kuwa mweusi kama wao sio tiketi ya kupeleka mikojo yako kule. Yani wao walihangaika kupigania nchi yao kisha sisi tukatumie huduma za afya, ajira,elimu na biashara zao. Wao watulee sisi?

Kila mtu abaki kwake ajenge nchi yake, kama kwenu hakuna ajira ukikimbilia SA nao unafanya wakose ajira hivo wana haki ya kukukataa.
Mimi naunga mkono madai yao ila njia zao nazikataa. Kwanza serikali imekaa kizembe katika suala hili. Mnalalamika nini wakati hata Kikwete alirudisha Wanyarwanda.
 
Kwa hili nawaunga mkono, ambacho huwa natofautiana nao ni lile suala la kuvamia na kuchoma moto biashara za wageni wakati wao hawana uwezo wa kufahamu ikiwa wageni husika wapo kihalali au hapana!

Kinyume chake, ukiangalia maelezo yao kwa kiasi kikubwa wanazungumzia WAHAMIAJI HARAMU. Sasa nyie mnaowapinga hao jamaa; ni nchi gani duniani ina-entertain Wahamiaji Haramu?!

Tanzania tunaruhusu Wahamiaji Haramu?!

Hivi hatujawahi kuwatoa Wanyarwanda na Warundi kwa viboko kule Kanda ya Magharibi kwa sababu tu waliingia nchini bila kufuata sheria, sasa how come mnataka S. African iwe ndo taifa la "cha wote" mnalotaka watu waende bila kufuata taratibu?

Nasikia, narudia; nasikia kwamba hata kwa Mtanzania, mathalani ukitoka sehemu moja kwenda nyingine within Tanzania, basi unatakiwa kule kwenye makazi mapya, basi mjumbe afahamu ujio wako... kwamba mtaani kuna "mkazi mpya"!

Sasa ikiwa hata ndani ya nchini yenyewe inashauriwa ukihamia makazi mapya basi mjumbe wa pale afahamu ujio wako, how come tena mtake kuingia nchi zingine bila kufuata taratibu wakati hata ndani ya mipaka yenu tu mnatakiwa kujitambulisha?!
 
Hivi hiyo illegal immigrants maana yake nini ?
Ni mtu yeyote anayeingia nchi nyingine bila ya Visa na/au Passport, na wakifika nchi husika wana-settle bila ya kuwa na vibali.

Yaani mtu unaondoka zako Dar kwenda Durban kama unavyoenda Morogoro!

Na kwavile umeingia bila vibali basi maisha yako kwa kiasi kikubwa yatakwepa kupitia mkondo rasmi! Kwa mfano, kama unafanya biashara, huwezi kwenda kukata leseni ya biashara kwa sababu unajua ukiulizwa passport yako ipo wapi, hutaweza kutoa!

Ukiajiriwa, utaajiriwa kimagumashi na wala work permit hautakuwa nayo kwa sababu hauna vibali halali vya kuishi nchi husika!!

Sometimes, unakuta mtu kaingia nchi husika kihalali lakini anaishi kiharamu!!

Kwa mfano, hususani kwa mbele; mtu unaenda zako say nchi X na Visitor Visa ya miezi 3 lakini unatokomea huko huko wakati visa yako imesha-expire!

Kwa Watanzania waliopo SA; unakuta mtu kaenda na passport kama kawaida lakini passport ime-expire au imepotea na bado haja-renew!
 
Miafrika inaroho mbaya sana na mibaguzi kuliko jamii yoyote duniani sema umaskini ndio unawakwamisha kufanya ubaguzi wa moja kwa moja
Huu ndio ukweli. Umaskini unaficha true colour ya waafrika.
 
Back
Top Bottom