Taarifa kwa wananchi na wafanyakazi wote wa hospitali ya taifa muhimbili

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765

Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi ya tarehe 23 Juni 2012.

Baada ya tathmini hiyo, Bodi ya Wadhamini imeagiza yafuatayo:(i) Madaktari waliopo kazini waendelee na kazi kama kawaida;(ii) Madaktari waliogoma warejee kazini kutii amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.(iii) Madaktari waliopo likizo warejee kazini mara moja. Utaratibu wa kufidia likizo na nauli zao umeandaliwa. (iv) Uongozi wa Hospitali uwachukulie hatua za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea kutokuhudhuria kazini na kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za kazi;(v) Uongozi wa Hospitali ufute mara moja ‘rotations’ za Madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo (interns); na(vi) Uongozi wa Hospitali uwapange (re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo kwenye maeneo yaliyoathirika wakati huu wa mgomo

Aidha, Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla. Vilevile, Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na subira na waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na maadili ya taaluma zao.

_________________Dkt. Gabriel UpundaKAIMU MWENYEKITIBODI YA WADHAMINI

Kiganyi, JF.
Mwanzo - wotepamoja.com
 
Hapo sasa kazi kwa madaktari, "ukisimama mchale, ukikimbia mchale"
 
Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi ya tarehe 23 Juni 2012.

Baada ya tathmini hiyo, Bodi ya Wadhamini imeagiza yafuatayo:(i) Madaktari waliopo kazini waendelee na kazi kama kawaida;(ii) Madaktari waliogoma warejee kazini kutii amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.(iii) Madaktari waliopo likizo warejee kazini mara moja. Utaratibu wa kufidia likizo na nauli zao umeandaliwa. (iv) Uongozi wa Hospitali uwachukulie hatua za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea kutokuhudhuria kazini na kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za kazi;(v) Uongozi wa Hospitali ufute mara moja ‘rotations' za Madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo (interns); na(vi) Uongozi wa Hospitali uwapange (re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo kwenye maeneo yaliyoathirika wakati huu wa mgomo

Aidha, Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla. Vilevile, Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na subira na waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na maadili ya taaluma zao.

_________________Dkt. Gabriel UpundaKAIMU MWENYEKITIBODI YA WADHAMINI

Kiganyi, JF.
Mwanzo - wotepamoja.com

Sasa naona hii serikali yetu ya chama cha Sisiem inatumia nguvu kuhusu hili sakata la madaktari. Kweli tutafika namna hii?

Sasa naanza kupata picha kwa nini hii nchi iko kama kichwa cha mwendawazimu. Badala ya kutatua tatizo, serikali ya CCM inatumia maujanjaunja kufunika kombe. Huu ni mtindo wa kizamani. Hizi body, mara waajiri walikuwa wapi wakati huduma za afya zinaanza kudorora? Ningekuwa na uwezo ningeifutilia mbali hii bodi maana imekuwa kipofu kwa muda mrefu wakati mambo yanaanza kuaharibika.

Na hata kama madaktari watarudi wote kazini haitabadilisha ukweli kwamba hospitali hazina vitendea kazi wala dawa. Wagonjwa wanalala chini, hakuna dawa, hakuna x-ray sasa hawa watu wa boda boda wanaogongwa kila siku watatibiwa vipi? kwa ramli?

Kwa nini hatuko realistic, au serikali inadhani kukubali (hata kama ni nusu) ya madai ya madaktari itaonekana dhaifu?
 
Hadi 2015 tutakutana na mambo mengi sana watanzania, tutajuuuuuta kuchagua kiongozi kwa kuangalia tabasamu na sio uwezo wa kuongoza. Combination ya JK na Pinda ni janga la kidunia, sijui nani huwa anamshauri mwenzie?? Eti hizo ndio cream za Taifa tumezipa nafasi za juu kabisa kutuongoza, what a Joke.
 
ni aibu mtanzania leo hii kutibiwa na madaktari kutoka india kwani hakuna madaktari hapa africa mpaka wakachukue madaktari huko uarabuni
 
Viongozi wa Tz walio kuwa wamezoea ramli za kina shehe Yahaya Mh! Vasco kila akiongea utaskia ndugu wananchi, hao wanao jiita Bodi ya wakurugenzi eti tarifa kwanachi ,Kujikomba. Wa Tanzania wenzangu hawa watu tuliwapa madaraka wametubip mara zote hizi kwa nini tuwapigie japo mara moja tu watuachie nchi yetu?
 
Hapo sasa ndio madaktari watakapo anza kugawanyika. Wakigawanyika tu watakuwa wamesaliti wenzao wenye msimamo na damu ya mwenyekiti wao ulimboka itakuwa imeenda bure. Pamoja na yote madaktari wafanye maamuzi ya pamoja, wasigawanyike hata kama ni kuendelea kutoa huduma.
 
Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ilikutana tarehe 28 Juni 2012 kujadili na kutathmini hali ya utendaji na utoaji wa huduma hivi sasa katika Hospitali. Imebainika kwamba utoaji huduma umeathirika kutokana na mgomo wa baadhi ya madaktari unaondelea kwa takriban wiki moja sasa tangu ulipoanza Jumamosi ya tarehe 23 Juni 2012.

Baada ya tathmini hiyo, Bodi ya Wadhamini imeagiza yafuatayo:(i) Madaktari waliopo kazini waendelee na kazi kama kawaida;(ii) Madaktari waliogoma warejee kazini kutii amri ya Mahakama Kuu Kitengo cha kazi, kwa mujibu wa Kifungu Na. 76 (1) na (2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004.(iii) Madaktari waliopo likizo warejee kazini mara moja. Utaratibu wa kufidia likizo na nauli zao umeandaliwa. (iv) Uongozi wa Hospitali uwachukulie hatua za kinidhamu wafanyakazi wote watakaoendelea kutokuhudhuria kazini na kufanya kazi bila sababu za msingi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za kazi;(v) Uongozi wa Hospitali ufute mara moja ‘rotations' za Madaktari waliopo kwenye mafunzo kwa vitendo (interns); na(vi) Uongozi wa Hospitali uwapange (re-deploy) Madaktari na Madaktari Bingwa waliopo kwenye maeneo yaliyoathirika wakati huu wa mgomo

Aidha, Bodi ya Wadhamini inawashukuru sana madaktari na wafanyakazi wote ambao wameendelea kuwahudumia wagonjwa wetu na wananchi kwa ujumla. Vilevile, Bodi ya Wadhamini inawasihi madaktari na wafanyakazi wote wawe na subira na waheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizopo pamoja na maadili ya taaluma zao.

_________________Dkt. Gabriel UpundaKAIMU MWENYEKITIBODI YA WADHAMINI

Kiganyi, JF.
Mwanzo - wotepamoja.com

hapo kwenye red karibu hosp zote wanawafukuza interns, hapa narejea kauli ya MR President katika hotuba yake "Kwa madaktari interns, wanahatarisha maisha yao kwani hawatapata cheti cha kudumu wakishiriki mgomo usiokuwa halali. Lazima watafakari sana kwa hayo wafanyayo"...
 
ili Document iwe valid sahihi ya mtoa document iwepo! Sasa mbona hakuna signature? Hizo ni propaganda tu hakuna bodi iliyokaa wala nini! SOLIDARITY FOREVER Drs!!!
Hakuna mtu kurudi hiyo J3!
 
Yan hii nchi ya ajabu sana..wakati watanzania hawajapatiwa ufumbuzi wa masuala ya msingi juu ya madaktari kugoma ili kuboresha mazingira ya kazi ...viongozi wenu wanajiandaa kucheza mechi ya wabunge wa Simba na Yanga halafu Rais wenu ndo refa...Tanzania bwana kweli kichwa cha mwendawazimu...

Inaniuma sana..source mizambwa
 
Back
Top Bottom