Taarifa kwa wanachama/wafuasi wa chadema wilaya ya lushoto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa wanachama/wafuasi wa chadema wilaya ya lushoto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbelwa Germano, Apr 24, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Apr 24, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima kwako Mkuu!

  Jana nilianzisha thread hapa JF kuhusu wanachama/wafuasi wa CDM watokao/wanaoishi wilayani Lushoto. Kwa bahati nzuri mafanikio yameanza kujitokeza kwa kupata wanachama/wafuasi 89 ambao wamenitumia majina yao na namba zao za simu kwa ajili ya kuongoza harakati za kienezi za CDM wilayani Lushoto. Aidha kuna bwana mmoja alijitambulisha kwa jina la Rashidi Shang'azi iliahidi kutuma idadi ya wanachama zaidi ya 100 waishio Dar-es-salaam (wazaliwa wa Lushoto) ambao wako tayari kuchangia chama kwa ajili ya shughuli za kuratibu shughuli za chama wilayani lushoto.

  Tunahitaji kufika maeneo mbalimbali ya wilaya yetu kuanzia soni, ubiri, ngulwi, lushoto,Kwai, Malimbwi hadi makanya n.k. Bila umoja na mshikamano wetu hatuwezi kupata mapambazuko ya kweli.

  Naamini kabisa hakuna Mtanzania asiyependa mabadiliko kwani macho na masikio sio mashahidi wa kweli zaidi ya nafsi zetu. Wanapotosha ukweli ni wale wenye maslahi binafsi, na makuwadi wa ufisadi. Naomba kutoa hamasa kwa wanachama wengine ambao wanapenda kujiunga na harakati za kujiimarisha kisiasa kwa chama chetu wilayani lushoto wawasiliane nami kwa namba 0714 311164 ili kuweza kupata majina yao na kuona ni kwa jinsi gani tunaweza kujipanga ili hatimaye mapambazuko ya kweli kwa chama chetu yaanze kujitokeza Lushoto.

  MBELWA Germano
  Mwanachama na Kamanda wa CDM
  Lushoto.

  M4C+PEOPLE'S POWER=HAKIKA TUTASHINDA!
   
 2. Mshuza2

  Mshuza2 JF-Expert Member

  #2
  Apr 24, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 4,091
  Likes Received: 1,711
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi pia ni mmojawapo! naishi huko ila kwa sasa niko Dodoma kikazi,nimefurahi kusikia kama wana CDM wapo,tubadilishe ndugu zetu wa huko lushoto.
   
Loading...