Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 5,897
- 10,358
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UZINDUZI WA KAMPENI YA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA MAADILI KUHUSU KUJENGA NA KUKUZA MAADILI, HAKI ZA BINADAMU, UWAJIBIKAJI, UTAWALA BORA NA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA
10 NOVEMBA, 2016
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) amezindua Kampeni ya Kitaifa inayohusu Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambanao dhidi ya Rushwa. Uzinduzi huu umefanyika leo tarehe 10 Novemba, 2016 katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya TAKUKURU, Makao Makuu jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maadili Kitaifa kwa mwaka 2016.10 NOVEMBA, 2016
Wakati anazindua kampeni hii Mhe. Kairuki alisema “Kampeni hii ya mwezi mmoja ambayo itakuwa endelevu imezinduliwa kwa lengo la kutafsiri kwa vitendo dhamira ya dhati ya Serikali
ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupiga vita vitendo vya rushwa, uzembe, ufisadi, matumizi mabaya ya fedha za umma, ukiukaji wa sheria, kanuni na taratibu ili kuimarisha misingi ya maadili, uwajibikaji na utawala bora nchini. Hivyo, Kampeni hii ya Kuhamasisha uzingatiaji wa Maadili, Haki za Binadamu, Utawala Bora na kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa ni mojawapo ya juhudi za Serikali za kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi kuikataa rushwa, kuwa waadilifu na kutambua haki zao.”
Shughuli nyingine zitakazofanyika ni katika kipindi cha kampeni ni Midahalo, Matembezi ya Hiari na kutoa huduma kwa umma. Aidha, Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Maadili na Haki za Binadamu ni tarehe 10 Desemba, 2016.
Taasisi hizo zinazoratibu kwa pamoja maadhimisho ya siku ya Maadili na Haki za Binadamu ni ; Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa Umma (ES); Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU); Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (POPSM); Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT); Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG); Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).
Mhe. Waziri ametoa wito kwa jamii nzima kutumia fursa hii kupata elimu kuhusu masuala ya Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji na Utawala Bora pamoja na kufahamu jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali katika kudhibiti rushwa.
Imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya Maadhimisho
Valentino Mlowola-Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
Kwa niaba ya Taasisi zinazoratibu Maadhimisho
10/11/2016
Valentino Mlowola-Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
Kwa niaba ya Taasisi zinazoratibu Maadhimisho
10/11/2016