Taarifa kwa Vyombo vya Habari: Riwaya ya Upako kutoka Kuzimu Sasa Inapatikana Tanzania

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
promo2.png

TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI
UJIO WA RIWAYA MPYA YA UPAKO KUTOKA KUZIMU
TOKA KWA
MWANDISHI M. M. MWANAKIJIJI
DAR-ES-SALAAM AUGUSTI 14, 2018 Inaruhusiwa kutangazwa mara moja.

Kwa ufupi: Mwandishi na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii anayetumia jina la kiuandishi M. M. Mwanakijiji anatangaza ujio wa riwaya yake ya pili iitwayo Ray Shaba: Upako kutoka Kuzimu ambayo itaanza kupatikana pote nchini kuanzia siku ya Jumatano Augusti 15, 2018. Kitabu hiki pia kinapatikana kupitia mtandao wa Amazon.Com
Dhima ya Kitabu:
Mhubiri maarufu zaidi nchini Tanzania na mmoja wa wahubiri maarufu Afrika ambaye pia amekuwa akijitangaza kuwa ni Nabii na Mtume wa Nyakati za Mwisho Askofu Mkuu Damien Ndondo anaingia kwenye anga za Mpelelezi Ray Shaba. Jina la Askofu Mkuu Ndondo linaanza kuhusishwa na matukio mbalimbali ya uhalifu wakati ambapo Ray Shaba yuko kwenye matatizo makubwa na mke wake kiasi cha kutishia ndoa yake. Kabla Ray Shaba hajajua nini cha kufanya mmoja wa waumini maarufu wa Kanisa la Askofu Ndondo anauawa mchana kweupe katikati ya Jiji la Dar-es-Salaam. Ray Shaba, akiongoza timu ya wapelelezi machachari Mohammed Nandonde na Joyce Masha wa Kikosi Maalum cha Polisi wanaingia katika mchezo wa panya na paka katika kuzuia jambo moja kugeuza dimbwi la mauaji. Nani atatoka salama hasa katika nchi ambapo Polisi wanaonekana wamepoteza weledi na siasa za ubabe zikionekana kutamalaki?
Mwandishi M. M. Mwanakijiji anasema kuhusu riwaya yake hii ya pili kuwa “ni simulizi linalojaribu kuonesha ni kitu gani kinaweza kwenda kombo pale ambapo mambo ya imani yanapoingia na kugusa uhalifu; lakini zaidi inatoa tahadhari kwa viongozi wa kisiasa na kijamii wanapokubali kuwa makuwadi wa imani za hatari”.
Akifuata nyazo za magwiji wa uandishi waliomtangulia kama Ben R. Mtobwa aliyemtambulisha Joram Kiango na Elvis Musiba aliyemtambulisha Willy Gamba, Mwanakijiji anamtambulisha Mpelelezi Ray Shaba kama sura mpya ya kizazi kipya cha wapelelezi mahiri na wenye weledi, wenye kuzingatia utaalamu, na miiko ya kazi za kipolisi. “Wasomaji watampenda Ray Shaba na timu yake, na watasubiri kwa hamu visa vyake vya kusisimua” anasema Mwanakijiji.
Hii ni riwaya ya pili ya Mwanakijiji ikifuatia ile ya Majeruhi wa Mapenzi iliyotoka miaka michache nyuma. Mfululizo wa riwaya za kipelelezi za Ray Shaba ziko mbioni. Pamoja na riwaya za Kipelelezi Mwanakijiji anajiandaa kuja na riwaya zinazojitegemea ambazo zinazidi kuonesha umahiri wake katika fani hii ya fasihi ya kiuandishi.
Kitabu hiki kinapatikana= kwa bei ya shilingi 17,500/ tu Jijini Dar-es-Salaam kwa oda maalum kupitia kwa mawakala wawili. Unaweza kulipia kwa Mpesa, Tigo au fedha Taslimu. Kwa sasa hivi kitabu hiki hakitopatikana kwenye maduka ya vitabu hadi taratibu zitakapokamilika. Kwa walioko mikoani wote wanaweza kuagiza kupigia mawakala hawa na taratibu za kuwafikishia nakala zao huko waliko zitafanyika ndani ya wiki moja. Ukishalipia kitabu kitakuwa njiani.
Bw. Paul Mpazi ambaye anapatikana kupitia simu 0763 316 402.
Unaweza pia kupata nakala yako kwa
Didah Salim
Sasy Solutions Company Limited
Magomeni Mapipa
Mtaa wa Idrisa, Nyumba Na. 51
Simu: 0655 992 874

Kwa Mawasiliano.
Paul Mpazi – CEO OZ Company
0763 316 402.
DAR-ES-SALAAM
 
View attachment 835890

Hongera sana mzee!
 
Hongera Mkuu, ntajitahidi nikinunue ila samahani naomba kuuliza nimeona umeweka jina La "Musiba' uyo musiba ndo huyohuyo wa lile gazeti la Tanzanite au?
 
nataka kuwa muandishi kama wewe,unanishauri nini..? na kipi cha kuzingatia ktk uandishi..?
 
Back
Top Bottom